Jua kesho tarehe 21 Machi litaingia Ikweta, Masika kuanza

... ufasaha ni dunia itajilengesha Ikweta. The Sun is stationary.

Dunia haiwezi jilengesha ikweta Boss ilhali ikweta ipo kwenye Dunia yenyewe.

Kutokana na Dunia kujizungusha katika mhimili wake na kulizunguka jua hii itasababisha leo Jua likae Ikweta au lihame

Ikweta ni imaginary Line inayogawanya dunia katikati katika Vizio Sawa viwili, ambavyo ni Kizio cha kaskazin na kizio cha Kusini.
Kizito cha kaskazini huitwa Tropical of Cancer wakati kizio cha Kusini kikiitwa Tropical of Capricorn. Zote hizo ni latitude ambazo kazi yake ni kui-position Dunia.
Tofauti na Longitude ambayo hutumika zaidi kwenye ishu ya masaa katika Maeneo ya dunia
 
Sasa mbona unanichanganya tena boss? Umesema jua limetoka kusini linakuja ikweta leo 21/3 na septemba linarudi tena ikweta. Sasa kama halitembei huko kote linatokaje sasa?

Sasa ulitaka nisemehe ikiwa lilikuwa upande wa Kusini? Na leo lipo ikweta, na kuanzia kesho litaanza safari yake ya kuelekea kizio cha kaskazini ambapo mpaka June 20,21 litafika Kilele cha kizio cha kasikazini Tropical of Cancer 23½°

Hapo ni ishu ya lugha tuu. Wapi unachanganya boss. Maana Dunia haitakuwa Kusini wala kaskazini, isipokuwa jua ndilo litakuwa Kusini au kaskazini mwa dunia licha ya kuwa halijongei
 
Kwema!

Joto la leo likanifanya niikumbuke Jiographia ya Kidato cha Kwanza.

Leo na kesho Tarehe 20 na 21 March Jua litakuwa Ikweta baada ya kuingia katika kizio cha Kusini(southern hemisphere) Tropical of Capricorn tangu mwaka Jana September lilipokuwa pia Ikweta.

Hivyo ni kusema jua limetoke Kusini na hivi leo na kesho litakuwa Ikweta likiigawanya Dunia katika mapande mawili yaloyolingana. Kumaanisha Usiku na mchana kutakuwa Sawa na hii wanajiografia wanaiita EQUINOX Yaani usiku na mchana kulingana.
Kumaanisha kuanzia tarehe 22 masika umeanza, mvua katika baadhi ya Maeneo zitaanza kunyesha hasa kwenye wiki ya mwandamo wa mwezi katika siku kumi mpaka kumi na tano zijazo.

Jua huwa ikweta Mara mbili Kwa Mwaka,
20,21 March ambayo hutambulika Vernal Equinox ambapo Msimu wa Masika huanza, na usiku na mchana hulinganana.

pia 20,21September ambayo hutambulika kama Autumnal equinox ambapo msimu WA Vuli huanza. Pia urefu WA usiku na mchana hulinganana.

Jua Kwa sehemu kubwa ndio huongoza Hali ya hewa na tabia ya nchi.
Masuala Kama ya jotoridi, kiwango cha unyevunyevu angani, Upepo, mawingo, Mvua huratibiwa Kwa kiasi kikubwa na Jua.

Miale ya jua huchangia pakubwa.

Hata hivyo upo uhusiano wa mwezi kuandama na mabadiliko ya halo ya hewa Kwa baadhi ya Maeneo.

Endapo jua litakuwa Ikweta basi mambo Yafuatayo yanatarajiwa,
1. Ongezeko la joto Kali
2. Mlingano wa usiku na mchana.
3. Mvua kuanza kunyesha hasa siku chache kabla ya mwezi kuandama n.k.

Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza;
1. Watu kuumwa kifua na mafua kutokana na wengi kulala usiku wakiwa wamepunguza vyakujifunika, ilhali nyakati za usiku wa manane Hali ya hewa hubadilika na kuwa ya baridi. Hivyo mapafu huingia unyevuunyevu kutokana na baridi.

Tutarajie mvua Maeneo ya Dar es salaam kwani na Maeneo mengi ya Pwani kuanzia wiki hii kutokana na kutakuwa na ongezeko kubwa la unyevuunyevu angani kutokana na joto na uwepo wa bahari hivyo mvua itanyesha.

Naomba niishie hapa!!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Asante kwa kutudadavulia, lakini ni sahihi kusema jua linaingia......( Ikweta, kaprikoni, Kansa, kusini, kaskazini, nk) ilhali tunajuwa jua halitembei, na objects zingine kama sayari, nyota, vimondo, satellites, nk, ndio huzunguka jua?
 
Inaweza kuwa sahihi au isiwe sahihi.
Lengo ni Uelewa tuu unapotoa elimu ili mtu asikariri.

Kitu kutojongea haimaanishi hakuwezi kuonekana pande tofauti tofauti.

Nilicholenga ni kuwa, licha ya kuwa jua halijongei lakini Kutokana na Dunia kulizunga jua huku ikijizungusha katika mhimili wake, hii hufanya jua kuonekana limehama(ingawaje halihami) kutoka muonekano wa upande mmoja wa Dunia Kwenda upande mwingine.
 
Kwema!

Joto la leo likanifanya niikumbuke Jiographia ya Kidato cha Kwanza.

Leo na kesho Tarehe 20 na 21 March Jua litakuwa Ikweta baada ya kuingia katika kizio cha Kusini(southern hemisphere) Tropical of Capricorn tangu mwaka Jana September lilipokuwa pia Ikweta.

Hivyo ni kusema jua limetoke Kusini na hivi leo na kesho litakuwa Ikweta likiigawanya Dunia katika mapande mawili yaloyolingana. Kumaanisha Usiku na mchana kutakuwa Sawa na hii wanajiografia wanaiita EQUINOX Yaani usiku na mchana kulingana.
Kumaanisha kuanzia tarehe 22 masika umeanza, mvua katika baadhi ya Maeneo zitaanza kunyesha hasa kwenye wiki ya mwandamo wa mwezi katika siku kumi mpaka kumi na tano zijazo.

Jua huwa ikweta Mara mbili Kwa Mwaka,
20,21 March ambayo hutambulika Vernal Equinox ambapo Msimu wa Masika huanza, na usiku na mchana hulinganana.

pia 20,21September ambayo hutambulika kama Autumnal equinox ambapo msimu WA Vuli huanza. Pia urefu WA usiku na mchana hulinganana.

Jua Kwa sehemu kubwa ndio huongoza Hali ya hewa na tabia ya nchi.
Masuala Kama ya jotoridi, kiwango cha unyevunyevu angani, Upepo, mawingo, Mvua huratibiwa Kwa kiasi kikubwa na Jua.

Miale ya jua huchangia pakubwa.

Hata hivyo upo uhusiano wa mwezi kuandama na mabadiliko ya halo ya hewa Kwa baadhi ya Maeneo.

Endapo jua litakuwa Ikweta basi mambo Yafuatayo yanatarajiwa,
1. Ongezeko la joto Kali
2. Mlingano wa usiku na mchana.
3. Mvua kuanza kunyesha hasa siku chache kabla ya mwezi kuandama n.k.

Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza;
1. Watu kuumwa kifua na mafua kutokana na wengi kulala usiku wakiwa wamepunguza vyakujifunika, ilhali nyakati za usiku wa manane Hali ya hewa hubadilika na kuwa ya baridi. Hivyo mapafu huingia unyevuunyevu kutokana na baridi.

Tutarajie mvua Maeneo ya Dar es salaam kwani na Maeneo mengi ya Pwani kuanzia wiki hii kutokana na kutakuwa na ongezeko kubwa la unyevuunyevu angani kutokana na joto na uwepo wa bahari hivyo mvua itanyesha.

Naomba niishie hapa!!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mkuu, jaribu kucheki usahihi wa 20, 21 September. Kama sijakosea huwa ni 23 September.
 
Upo vizuri ROBERT HERIEL tayari mvua inanyesha pande zetu

Sasa hivi mbegu zinapaswa kuwa ardhini.
Ili kuvizia mwandamo wa mwezi wa nne, na watano mazao yawe yamekuwa kiasi cha kutosha. Ikifika mwandamo wa mwezi wa sita, baridi itakapoanza yakuzwe na umande wa Asubuhi kwani hakuwagi na mvua nyingi hivyo umande utatumika kukomazia mazao.
 
Ingawa nilikuwa master wa geography O level na A level ila sasa nishasahau hayo mambo. Kweli maisha nyoko
Hata huku kwetu masika ndo yanaisha ishia, na upepo umeshaanza kuvuma sana tu na kama mvua zitaanza kunyesha tena zitaharibu mazao yetu.
 
Kwema!

Joto la leo likanifanya niikumbuke Jiographia ya Kidato cha Kwanza.

Leo na kesho Tarehe 20 na 21 March Jua litakuwa Ikweta baada ya kuingia katika kizio cha Kusini(southern hemisphere) Tropical of Capricorn tangu mwaka Jana September lilipokuwa pia Ikweta.
'Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza;
1. Watu kuumwa kifua na mafua kutokana na wengi kulala usiku wakiwa wamepunguza vyakujifunika, ilhali nyakati za usiku wa manane Hali ya hewa hubadilika na kuwa ya baridi. Hivyo mapafu huingia unyevuunyevu kutokana na baridi'.Kwa hili la athari za kiafya nakuunga mkono asilimia100...
 
Hata huku kwetu masika ndo yanaisha ishia, na upepo umeshaanza kuvuma sana tu na kama mvua zitaanza kunyesha tena zitaharibu mazao yetu.

Inaweza kuwa Mkuu kutokana na tabia nchi ya Tanzania,
Hata hivyo Altitude ya eneo husika pia huchangia mvua kuonyesha au kutokunyesha, pamoja na suala la upepo.

Mvua za Vuli huanza mwezi wa kumi mwisho kukomaza baadhi ya mazao ya miti maembe ambayo huanza kutoa maua mwezi wa Saba au wanane, mpaka mwezi wa kumi na moja baadhi ya miti ya matunda hutoa matunda yaliyoiva. Naomi huu ndio msimu wa wadudu na Ndege kuzaliana tofauti na masika ambayo viumbe vipendavyo majimaji ndio huzaliana Kama vile Mbu, vyura n.k.

Mvua za Vuli sio nyingi kama Mvua za masika licha yakuwa Jua linakuwa linapita katika eneo lilelile.

Hii ni mada nyingine
 
Back
Top Bottom