Jua kesho tarehe 21 Machi litaingia Ikweta, Masika kuanza

Ninachojua mimi sio kwamba jua halina movement yoyote la!
Jua lina mzunguko wake ambao hujumuisha sayari zote zilizo kwenye umiliki wa jua pamoja na dunia.

Huo mzunguko wa jua au mjongeo wa jua hatuwezi kuuhisi kama vile sisi viumbe waliopo dunia hatuwezi kuuhisi mzunguko wa dunia ila matokeo ya mzunguko huo ndio tunaoyapata kama hivyo Masika joto baridi nk.

Huo mzunguko wa jua ni wa muda mrefu mno kiasi sisi kupata matokeo ya mzunguko huo inachukua vizazi na vizazi.

So dunia inalizungika jua, lakini jua nalo lina mzunguko wake kwenye point yake huko angani.
HAPANA Jua halina mzunguko (km una link hapo tuwekee)
nachojua kuna Black hole na kuna vitu kibao vinaelekea lkn kinachotoa energy /Moto ni Sun
Earth ina mzunguko wake kulizunguka Jua tunapata siku 364 days & 6hrs ndio mleta Mada kauelezea
 
Ndiyo , linapohamia Ikweta

1647846576138.png
 
Ahsante sana mkuu, ubarikiwe🙏

1647847696711.png

Siku 90 zijazo jua litakuwa kizio cha kaskazini(Northern Hemisphere) ambayo ni Tropical ya kansa, kumaanisha jua na miale yake litakuwa mbali na kizio cha kusini, hivyo upande wetu(chini ya ikweta itakuwa ni msimu wa baridi(winter) huku nchi za ulaya ukiwa ni msimu wa kiangazi(summer)
 
Dah Leo ndio nimeelewa maana ya equinox ,tangu nimalize kidato Cha tatu cjui nilikuwa na jibia mtihan , shukran sana mtoa mada...
 
Dah Leo ndio nimeelewa maana ya equinox ,tangu nimalize kidato Cha tatu cjui nilikuwa na jibia mtihan , shukran sana mtoa mada...

Karibu Sana.
Wala sio kosa lako,
Mara nyingi elimu tuliyofundishwa wengi wetu tuliikariri ndio maana tunasema haina maana yoyote lakini kimsingi inamaana Kama utaielewa
 
Kwema!

Joto la leo likanifanya niikumbuke Jiographia ya Kidato cha Kwanza.

Leo na kesho Tarehe 20 na 21 March Jua litakuwa Ikweta baada ya kuingia katika kizio cha Kusini (Southern Hemisphere) Tropical of Capricorn tangu mwaka jana Septemba lilipokuwa pia Ikweta.

Hivyo ni kusema jua limetokea Kusini na hivi leo na kesho litakuwa Ikweta likiigawanya Dunia katika mapande mawili yaliyolingana.

Kumaanisha usiku na mchana kutakuwa sawa na hii wanajiografia wanaiita EQUINOX yaani usiku na mchana kulingana.

Kumaanisha kuanzia tarehe 22 masika umeanza, mvua katika baadhi ya maeneo zitaanza kunyesha hasa kwenye wiki ya mwandamo wa mwezi katika siku 10 mpaka 15 zijazo.

Jua huwa Ikweta mara mbili kwa mwaka 20, 21 March ambayo hutambulika Vernal Equinox ambapo Msimu wa Masika huanza, na usiku na mchana hulingana.

pPa 22, 23Septemba ambayo hutambulika kama Autumnal Equinox ambapo msimu wa Vuli huanza, pia urefu wa usiku na mchana hulinganana.

Jua kwa sehemu kubwa ndio huongoza hali ya hewa na tabia ya nchi.

Masuala kama ya jotoridi, kiwango cha unyevunyevu angani, upepo, mawingo, mvua huratibiwa kwa kiasi kikubwa na jua.

Miale ya jua huchangia pakubwa.

Hata hivyo upo uhusiano wa mwezi kuandama na mabadiliko ya halo ya hewa Kwa baadhi ya maeneo.

Endapo jua litakuwa Ikweta basi mambo yafuatayo yanatarajiwa,
1. Ongezeko la joto Kali
2. Mlingano wa usiku na mchana
3. Mvua kuanza kunyesha hasa siku chache kabla ya mwezi kuandama n.k.

Athari za kiafya zinazoweza kujitokeza:

1. Watu kuumwa kifua na mafua kutokana na wengi kulala usiku wakiwa wamepunguza vyakujifunika, ilhali nyakati za usiku wa manane hali ya hewa hubadilika na kuwa ya baridi.

Hivyo mapafu huingia unyevuunyevu kutokana na baridi.

Tutarajie mvua Maeneo ya Dar es Salaam kwani na maeneo mengi ya Pwani kuanzia wiki hii kutokana na kutakuwa na ongezeko kubwa la unyevu unyevu angani kutokana na joto na uwepo wa bahari hivyo mvua itanyesha.

Naomba niishie hapa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es Salaam
Good, very good! Lakini Hariel, haya yalikuwa kweli kabla ya mtu anayeitwa "Mabadiliko ya Tabia Nchi" kuingia. Am I right?
 
Good, very good! Lakini Hariel, haya yalikuwa kweli kabla ya mtu anayeitwa "Mabadiliko ya Tabia Nchi" kuingia. Am I right?

Haya ni kweli mpaka sasa, ingawaje yapo mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana uharibifu katika anga la mbali ilipo tabaka la Ozone layer (O3)kuharibiwa hivyo miale ya jua inatoka pasipo uwiano mzuri Hali iñayopelekea mabadiliko katika tabia ya nchi na Hali ya hewa.

Zingatia miale ya jua(insolation) inaathiri Kwa shemu kubwa Tabia ya nchi na Hali ya hewa katika Dunia yetu.
 
Ninachojua mimi sio kwamba jua halina movement yoyote la!
Jua lina mzunguko wake ambao hujumuisha sayari zote zilizo kwenye umiliki wa jua pamoja na dunia.

Huo mzunguko wa jua au mjongeo wa jua hatuwezi kuuhisi kama vile sisi viumbe waliopo dunia hatuwezi kuuhisi mzunguko wa dunia ila matokeo ya mzunguko huo ndio tunaoyapata kama hivyo Masika joto baridi nk.

Huo mzunguko wa jua ni wa muda mrefu mno kiasi sisi kupata matokeo ya mzunguko huo inachukua vizazi na vizazi.

So dunia inalizungika jua, lakini jua nalo lina mzunguko wake kwenye point yake huko angani.
Kuna mtaalam mmoja sijui alipotelea wapi @mgalanjuka aka @monstgla alitupatiaga hii elimu kuwa kumbe hata jua linazunguka. Si jua tu, hata nyota za kwenye galaxy hii, pia zina mzunguko wake kuizunga black hole.

Maswali hapana.
 
Dunia kila jambo lawezekana
 
Haya ni kweli mpaka sasa, ingawaje yapo mabadiliko ya tabia ya nchi kutokana uharibifu katika anga la mbali ilipo tabaka la Ozone layer (O3)kuharibiwa hivyo miale ya jua inatoka pasipo uwiano mzuri Hali iñayopelekea mabadiliko katika tabia ya nchi na Hali ya hewa.

Zingatia miale ya jua(insolation) inaathiri Kwa shemu kubwa Tabia ya nchi na Hali ya hewa katika Dunia yetu.
Ngoja nisubiri maana huku kwetu Kila kitu kimekauka kwa jua kali
 
Ninachojua mimi sio kwamba jua halina movement yoyote la!
Jua lina mzunguko wake ambao hujumuisha sayari zote zilizo kwenye umiliki wa jua pamoja na dunia.

Huo mzunguko wa jua au mjongeo wa jua hatuwezi kuuhisi kama vile sisi viumbe waliopo dunia hatuwezi kuuhisi mzunguko wa dunia ila matokeo ya mzunguko huo ndio tunaoyapata kama hivyo Masika joto baridi nk.

Huo mzunguko wa jua ni wa muda mrefu mno kiasi sisi kupata matokeo ya mzunguko huo inachukua vizazi na vizazi.

So dunia inalizungika jua, lakini jua nalo lina mzunguko wake kwenye point yake huko angani.
Nielimishe, hivi jua linaelea elea huko juu? Eti na duniabyetu inaelea elea ?
 
Huku ngurumo za htr sana,
Muda wwte naona inaweza kushuka,
Big up sn mkuu,
 
Back
Top Bottom