JPM aomba wananchi wamsaidie kutumbua majipu

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
7,033
15,616
Rais wa JPM aomba watanzania wamsaidie kukamua majipu madogo na uchungu huku yeye akitumbua yale makubwa.

Asema majipu madogo yapo ktk jamii inayotuzunguka.

Embu tupia hapo jipu ambalo linakukera tusaidiane kulitumbua wewe unamshika me naliminya
 
Kwangu ni kile kikokotozi cha TRA.......waizi tu........
 
MICHANGO YA HARUSI.....HILO JIBU LIMEKAA MGONGONI HATA MIKONO KULIPAPASA UJUWE LIMEIVA AU BADO NI KAZI KWELIKWELI.
 
Mikataba ya kazi ifanywe homogeneous. Huwa sielewi mfano wafanyakazi wa sekta moja unakuta huku mkataba unatoa hiki lakini kule kwingine hicho kitu hakipo ..sasa unajiuliza hawa wanapewa hisani ama huku sie ndo tunaibiwa make zote ni sekta zinazofanana. Hata maeneo mengine mkataba mtu anapewa nyumba lakini kwingine wala hicho kifungo hakipo. Naelewa Luna vitu ambavyo ni lazima kuwepo kwenye mikataba haijalishi huyu yuko Mbeya ama Kigoma na hii ndo jipu yangu, serikali iwasaidie watu kuharmonise mikataba katika idara zinazofanana
 
Katiba pendekezwa ndio jipu mama. Tukitumbua hili mengine yote yatapona taratibu.vinginevyo tunatibu Ukimwi kwa pain killers
 
Mali zote zilizoko Tanzania zisajiliwe.
Kuanzi majumba ,mashamba ,viwanja,vituo vya mafuta na wamiliki halisi wa malori na mabasi wajulikani.

Inaonesha kuwa wamiliki wakubwa wa mali nyingi zilizotapakaa kila mkoa ni watumishi wa umma.
Hii itasaidia kujua nani ni Fisada au nani ametumia rasilimali za umma kujilimbikizia mali.

Pia itasaidia kuondoa huu mtindo wa wezi walioka madarakani kuwasingizia watu wengine kuwa ni mafisadi na wala rushwa huku wao wakiwa ni mafisadi papa na nyangumi.

Sasa hivi bila kuwa na usajili wa mali na wamiliki wake watanzania tunaweza tukawa tunawapongeza mafisadi na kuwapa majina mazuri ya uchapakazi na hapa kazi tu.
Utajiri walionao watumishi wa juu wa umma hauendani na mishahara yao.
 
Wenyeviti na watendaji wa mitaa kutoza 10% ili kunumua ardhi hasa zisizopimwa wakati hawana mamlaka hayo.
JPM piga marufuku na ndo huongeza migogoro ya ardhi isiyo ya lazima.
 
Pia JPM au waziri wa ardhi toa tamko la kusitisha maendelezo yoyote ya ardhi ambayo hayana kibali cha manispaa pia iende sambamba na kuunda taasisi ya kusimamia uendelezaji wa miji na upimaji kama ilivyo CDA.
Tunatamani tuone hayo yakitokea lkn yanahitaji msukumo wa viongozi wa juu.
 
MABASI NA MADALADALA KUKATIZA RUTI NAONA HILI LINAPUUZWA SANA / WAZIRI WAKE MUHUSIKA HAKIKA SIMFAHAMU UKATIZAJI RUTI NI UKIUKAJI WA LESENI ZAO/ GARI IMEANDIKWA BUG--DONDWE AU NZASA AU MASAKI KIPUUZI KABISA NA MAKUSUDI KATIKA LENGO LA KUTESA WANANCHA NA KUWAONGEZEA GHARAMA ZINAISHIA CHANIKA.
HILI NI JIPU BAYA KWELIKWELI/ LIMETAPAKAA NCHI NZIMA.hakika ninafahamu lengo la rais wetu ni wananchi wanyonge nao wafaidi matunda ya uongozi wa DK.MAGUFURI
 
Mfanyakazi aliyeajiriwa sekta binafsi anateseka sana kwa kukatwa kodi kubwa bila ridhaa yake ikiwa pamoja na kulipa kodi kwa bidhaa na huduma anazonunua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom