geraldincredible
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 2,036
- 7,220
RAIS MAGUFULI NA JIPU LA MSHIPA WA MOYO
Aprili mwaka jana nilifanya mahojiano na Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, aliyeihudumia nchi hii kwa miaka 10 mfululizo wakati wa utawala wa Rais wa Tatu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
Katika mahojiano hayo, kipo kipindi nilimtaka Sumaye atoe pongezi kwa Rais Magufuli, angalau aoneshe kuthamini kazi nzuri anayoifanya ya kutumbua majipu. Yaani kuwaondoa watu wasio waadilifu na wenye kasoro serikalini.
Sumaye akasema kuwa Rais Magufuli anajitahidi kwa sababu anaonesha uthubutu lakini yapo majipu mengine yatamshinda kwa sababu yamekaa sehemu mbaya. Sumaye akaniuliza: “Unaweza vipi kutumbua jipu la kwenye mshipa wa moyo?”
Nami nikatafakari, “jipu la mshipa wa moyo!” Baada ya hapo nikacheka, Sumaye naye alicheka kisha akaendelea: “Hata mimi ningekuwa Rais kupitia CCM kuna majipu yamekaa vibaya, kwa hiyo yangenishinda.” Sumaye akacheka tena!
Kuanzia hapo Sumaye akaniachia msemo: “Jipu la mshipa wa moyo!” Hili liwe kubwa au lile dogo lenye kuitwa jipu uchungu, ukilitumbua linaweza kusababisha mawasiliano kati ya ubongo na moyo yakatike. Kumbe jipu la mshipa wa moyo linaweza kusababisha kifo.
Mwanzoni nikawa na fikra kwamba jipu la mshipa wa moyo ni aina fulani ya vigogo ambao kuwagusa ni hatari. Hata Sumaye mwenyewe aliyenipa msemo huu, alimaanisha watu wazito.
Kwamba unakuta jipu ni Rais mstaafu au kigogo kwenye chama ambacho kimekupa ridhaa ya kuongoza, unaanzaje kumtumbua? Jipu ni mfanyabiashara mzito ambaye huwezi kumtikisa bila kutikisa uchumi wa nchi. Hiyo ndiyo ilikuwa tafsiri.
TAFSIRI YANGU
Hapa naomba nije na tafsiri yangu kuhusu jipu la mshipa wa moyo! Ni kwmba anaweza asiwe kigogo lakini inategemea jinsi ambavyo umemshiba kiasi kwamba unaona kuwa huwezi kumtumbua pasipo wewe mwenyewe kuumia.
Wala hapa haimaanishi urafiki, maana Rais Magufuli alimtumbua kwa aibu, sahibu wake wa miaka na miaka, Charles Kitwanga na maisha yameendelea.
Rais wa Nne, Dk Jakaya Kikwete, aliridhia rafiki yake kipenzi, Edward Lowassa ajiuzulu Uwaziri Mkuu, wakati alikuwa na nguvu pamoja na mamlaka ya kumkingia kifua. Na maisha yaliendelea.
Hivyo, hapa tunatakiwa kuzidi kuelewana kuwa jipu la mshipa wa moyo siyo kigogo tu au urafiki kati ya mwenye mamlaka na anayestahili kutumbuliwa, isipokuwa inategemea na kiwango cha kushibana.
Jipu la mshipa wa moyo lipo hata kwenye mapenzi, yupo mtu ambaye anaweza kufanya uamuzi wa kumwacha mpenzi wake au hata kumtaliki mwenzi wake wa ndoa kwa kosa ambalo ukilichunguza ni dogo tu!
Hata hivyo, huyohuyo mtoa uamuzi wa kuacha mtu kwa kosa dogo, anaweza kukutana na mpenzi mwingine, wakawa kwenye ndoa au bila ndoa, halafu huyo mpenzi mpya akamfanyia tukio kubwa zaidi lakini akashindwa kumwacha.
Tena huyo wa kosa kubwa anaweza kufanya makosa mengi na kurudia mara nyingi lakini mwenye mpenzi wake asichukue uamuzi wa kuvunja mapenzi au ndoa, akawa anavumilia tu, wakati mwingine anashuhudia lakini anacheka kama zuzu!
Uswahilini kwetu watasema mtu huyo kapewa limbwata, yaani kafanyiwa mambo ya mazingara, kwa hiyo hajitambui. Ni kwa sababu anafahamika kwa uamuzi wa haraka, kosa moja talaka, lakini mpenzi mpya makosa mengi makubwa lakini anamkumbatia.
Wenye kukimbilia kuisingizia limbwata na dawa nyingine za ushirikina hawajui kuhusu jipu la mshipa wa moyo. Ndiyo imetokea jipu limeota kwenye mshipa wa moyo, unalitumbuaje? Unadhani mtumbuaji mwenyewe haogopi kifo?
JIPU LA MSHIPA WA MOYO
Siyo kigogo wala rafiki mkubwa anayetambulika lakini ndiye mshipa wa moyo. Huyo akiwa jipu kumtumbua ni vigumu sana.
Dk Kikwete aliruhusu Lowassa ang’oke pamoja na viongozi wengine wengi katika wizara zake. Hata hivyo, yupo mmoja alimlinda mpaka mwisho, licha ya kashfa nyingi kuelekezwa dhidi yake.
Shukuru Kawambwa alikuwa mshipa wa moyo wa JK. Tangu alipotangaza baraza lake la mawaziri mapema mwaka 2006, Kawambwa alikuwemo. JK alimbadilisha Kawambwa wizara mbalimbali.
Januari 2006, JK alimteua Kawambwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Oktoba 2006, akamteua kuwa Waziri wa Maji, Februari 2008, alimteua kuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Maendeleo ya Tehama, Mei 2008, alimteua kuwa Waziri wa Miundombinu, Novemba 2010, alimteua kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Wizara ya Elimu ndiyo hasa Kawambwa alidumu. Maeneo mengine alilalamikiwa lakini kwenye Elimu malalamiko yalikuwa makubwa mno. Yakafuata matokeo ya kutisha mwaka 2012 baada ya watahiniwa wa kidato cha nne, kwa zaidi ya asilimia 60 kupata daraja sifuri.
Shinikizo likawa Kawambwa ang’oke lakini JK hakuelewa kitu alipoambiwa habari hizo. Kawambwa alidumu licha ya kufanya kazi kwa presha, kila upande alipigiwa kelele ang’oke.
Kipindi chote Kawambwa akipigiwa kelele za kutakiwa kujiuzulu mwenyewe au JK akitakiwa kuwamjibisha waziri wake, yapo mabadiliko kadhaa ya Baraza la Mawaziri ambayo yalifanyika lakini mara zote JK alimwacha Kawambwa salama.
Kituko kikubwa zaidi kilijiri Januari 2015, baada ya ripoti ya uchotwaji wa fedha Benki Kuu katika akaunti ya Escrow, iliyohusu mgogoro wa malipo ya tozo za gharama za uwekezaji (capacity charge) kati ya Tanesco na kampuni ya IPTL.
Baada ya ripoti hiyo kusomwa na madudu yake kubainishwa, wapo vigogo walikwenda na maji. Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema aling’oka.
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospter Muhongo, aling’oka. Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof Anna Tibaijuka, alikwenda na maji, vilevile aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
Baada ya hapo, JK alitakiwa kufanya mabadiliko kidogo katika Baraza la Mawaziri. Alifanya hivyo Januari 2015 lakini akawaacha watu hoi, alipoamua kushughulikia matatizo ya Wizara ya Elimu.
JK alimwondoa kazini, aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo na kumbakiza Kawambwa. JK alisema kuwa wakati mwingine matatizo ya wizara yanaweza kusababishwa na watu wa chini na siyo wa waziri. Alimkingia kifua.
Nafasi ya Mulugo ikachukuliwa na Anne Kilango Malecela. Hivyo naibu waziri mpya, aliingia ofisini kufanya kazi na waziri aliyekuwepo muda wote na aliyehusishwa na anguko kubwa la elimu nchini.
Jiulize Kawambwa ni nani? Ni mkazi wa Bagamoyo, Dar es Salaam, wilaya ambayo ndiyo anaishi pia JK. Kawambwa ni mbunge wa Bagamoyo, jimbo ambalo JK alikuwa mbunge wake kabla ya kugawanywa mara mbili kupata majimbo ya Bagamoyo na Chalinze, ndipo JK akahamia Chalinze.
Mazingira hayo ya JK kuvaa miwani ya mbao asione yanayoandikwa na yenye kuoneshwa kuhusu Kawambwa, kuweka pamba masikioni asisikie yaliyonenwa kuhusu Kawambwa, jumlisha mazingira yao ya ukazi, ikawa sababu ya watu kusema: “JK anamlinda ndugu yake.” Ikapitishwa kuwa JK na Kawambwa ni ndugu.
MSHIPA WA MOYO WA MAGUFULI
Nilishampongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kuchokoza suala la Makanikia ili kutetea mapato ya nchi lakini niliahidi kuwa siwezi kushangilia goli la kuongoza, maana suala ambalo ameligusa lipo katika mikataba, bila kuwa makini na kwenda kwa uangalifu wa kutosha, linaweza kugharimu taifa.
Kama ilivyotokea kwenye Samaki wa Magufuli na Dowans, kwa taifa kulipa mabilioni kutokana na kutetea haki ya Watanzania lakini bila uangalifu, inaweza kutokea pia kwenye suala la Makinikia. Akili itumike kuliko hisia.
Tuweke hilo kando, tuje kwenye uamuzi wa Rais Magufuli baada ya kupokea Ripoti ya Kamati Maalum ya Rais ya kuchunguza mchanga kutoka migodini nchini na kujua aina na kiwango cha madini (Makanikia).
Rais Magufuli alisema kuwa Wizara ya Nishati na Madini imeshindwa kusimamia kazi za madini inavyotakiwa, hivyo aliamua kumfukuza kazi Prof Muhongo ambaye ni yeye alimrudisha ofisini baada ya kuondolewa wakati wa JK.
Rais Magufuli pia aliivunja Bodi ya Wakala wa Madini nchini (TMAA), kwa kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa. Rais Magufuli alisema hawezi kumfukuza kazi Kamishna wa Mdini kwa sababu amemteua hivi karibuni lakini mtangulizi wake afuatiliwe na afikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Ikumbukwe kuwa Machi 26, mwaka huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Prof Justin Ntalikwa, sababu ikiwa hiyohiyo ya Makanikia, kwamba Ntalikwa alitaja kiasi kidogo cha madini kilichomo ndani ya mchanga mbele ya Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Turudi kwenye kauli ya Rais Magufuli kuwa Wizara ya Nishati na Madini imeshindwa kusimamia sekta ya madini. Ndani ya wizara, ukimwondoa mtendaji mkuu ambaye ni Katibu Mkuu, Rais anao wasaidizi wake wawili wanaopaswa kumfanyia kazi vile anavyotaka.
Wasaidizi hao kuna namba moja na namba mbili, yaani yupo waziri na naibu waziri. Tayari waziri ameshamfukuza kazi. Je, naibu waziri anapona vipi, wakati yeye mwenyewe ameeleza kuwa wizara imeshindwa kazi?
Naibu waziri ni Dk Medard Kalemani. Mkazi wa Chato, Geita, nyumbani kwa Rais Magufuli. Kalemani ni mbunge wa Chato, jimbo ambalo Rais Magufuli alikuwa mbunge wake kuanzia mwaka 1995 mpaka 2015 alipogombea Urais na kushinda.
Je, Kalemani amepona fyekeo kwa sababu ni mshipa wa moyo wa Rais Magufuli? Je, Kalemani ni jipu la mshipa wa moyo wa Rais Magufuli?
Mwaka jana, kuna gazeti lilivaa ujasiri wa kuanika kile ambacho walikiita ufisadi wa Dk Kalemani. Gazeti hilo lilikiona cha mtema kuni baada ya kujibiwa na Serikali, wakati aliyepaswa kujibu tuhuma ni Dk Kalemani mwenyewe.
Mawaziri mbalimbali hutuhumiwa kwa kashfa za ufisadi lakini mhusika mmojammoja huamua kujibu, maana ufisadi wa mtu ni jambo binafsi. Nauliza tena; Dk Kalemani wa Chato ni mshipa wa moyo wa Rais Magufuli?
MISHIPA YA MOYO
Hivi sasa inafahamika kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni mshipa wa moyo wa Rais Magufuli, vile alivyogeuka jipu, basi likawa jipu la mshipa wa moyo.
Pamoja na kila kilichoelezwa, Rais Magufuli alitokeza na kuwanyamazisha wote wanaojaribu kumsakama Makonda, akasema kuwa hapangiwi mtu wa kufanya naye kazi.
Haitoshi, Rais Magufuli alimfukuza kazi aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, sababu ikiwa kujaribu kutengeneza mzani wa haki, kutokana na tukio la Makonda kuvamia kituo cha Clouds TV akiwa na askari wenye bunduki, kulazimisha kipindi alichokitaka yeye kiruke hewani.
Ukiwa jipu la mshipa moyo kweli hutumbuliwi, maana Adam Malima alisemwa sana akiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini pamoja na waziri wake, William Ngeleja, kwa kushindwa kuiongoza vizuri wizara yao.
Kelele zilitoka nyingi kutaka Ngeleja na Malima wang’oke lakini Ngeleja aliondolewa halafu Malima akahamishiwa Wizara ya Fedha, akawa naibu waziri, akadumu huko mpaka JK alipoondoka madarakani.
Kama Dk Kalemani ni jipu la mshipa wa moyo, basi ataendelea kuwepo wizarani kama ambavyo Makonda anavyokuwepo Dar es Salaam.
Si ajabu pia tukasikia kuwa Dk Kalemani kapandishwa cheo kuwa Waziri kamili wa Nishati na Madini, wakati ni yeye na Muhongo walioshindwa kuongoza wizara vizuri na kusababisha madudu aliyoyaona Rais Magufuli kisha kumtimua Muhongo.
Ukifuatilia, utagundua kuwa hakuna mahali ambapo nimetumia Kiingereza na kuiita hii ni double standard.
Ndimi Luqman MALOTO