Josina Machel: Zitto Kabwe November 2014

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Josina Machel katika S is for SAMORA

Uhuru wa nchi ya Msumbiji hauwezi kuelezwa bila kumtaja Samora Machel na bila kuitaja Tanzania. Hata hivyo Watanzania wengi na pia wana Msumbiji wengi wa kizazi cha sasa wanapoteza kumbukumbu kuhusu nafasi ya Tanzania katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo. Mwandishi Sarah LeFanu ameandika kitabu ‘S is for SAMORA’ na kuweka mtiririko wa historia ya Shujaa huyu wa ukombozi wa kusini mwa Afrika. Katika kitabu hiki unaona namna Tanzania ilivyoshiriki kwa damu katika kuhakikisha ukombozi wa nchi hiyo. Kwa wale wanaopenda historian a kumpenda Samora wanaweza kutumia kitabu hiki kama rejea sahihi kabisa ya Kiongozi huyu mwana mapinduzi.

Ingawa kitabu hiki kinamhusu Samora, wasomaji wangu watanisamehe kwamba rejea yangu itamhusu Mke wa Samora Machel aliyeitwa Josina Machel. Katika mtiririko wa kitabu hiki hasa kati ya mwaka 1965 mpaka mwaka 1971 utamsoma mpiganaji Josina. Lakini utamsoma zaidi kuanzia ukurasa wa 95 mpaka ukurasa wa 104. Kitabu hiki kina kurasa 284 bila nyongeza mbalimbali ikiwemo Taarifa ya ajali ya ndege iliyomwua shujaa Samora.

Josina alikuwa shujaa wa uhuru wa Msumbiji kabla hata Samora hajawa shujaa. Akiwa na umri wa miaka 18 tu aliondoka nchini mwake ili kuja Tanzania kujiunga na waasi wa FRELIMO, chama kipya kilichokuwa kimeanzishwa ili kukomboa Taifa la Msumbiji kutoka kwenye ukoloni mkongwe wa Kireno. Hata hivyo alikamatwa na Wareno na kuswekwa jela kwa miezi kadhaa. Hakukata tamaa na alifanikiwa kutoroka na kuingia Tanzania kasha kupata mafunzo ya kijeshi na kupambana mstari wa mbele katika mapambano. Josina alikuwa mwanamke wa shoka, msichana mrembo na shupavu. “Binti unayeweza kujivunia kwa mzazi, dada mkuu wa shule kwa Mwalimu Mkuu na mrembo ambaye wavulana wote mtaani wangependa kutoka naye” ndivyo mwandishi anamwelezea Josina alivyokuwa.

Akiwa Tanzania kabla hajapata mafunzo ya kijeshi alifanya kazi kama dada wa nyumbani kumsaidia Janet Mondlane kulea watoto wake. Mara nyingi Edward Mondlane na Janet Mondlane walikuwa hawapo nyumbani na hivyo Josina alifanya kazi ya kuwaletea watoto watatu hawa. Mmoja wa watoto waliolelewa na Josina ni Nyeleti Mondlane ambaye hivi sasa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama cha FRELIMO na Mbunge katika Bunge la nchi hiyo. Baadaye Josina alikuwa mchumba wa Kamanda Mkuu wa Jeshi la FRELIMO Filipe Magaia ambaye mwaka 1966 aliuwawa na majasusi wa PIDE, ambacho kilikuwa kikosi cha kijasusi cha Serikali ya Ureno. Josina aliamuriwa kutolia kufuatia kifo hicho cha mpenzi wake kwani yeye kama kamanda hakupaswa kuonyesha udhaifu wowote ule. Baadaye Josina alijikuta akimbembeleza rafikiye Janet Mondlane ambaye naye mwaka 1969 alifikwa na majonzi ya kuondokewa na mumewe Rais wa chama cha ukombozi cha FRELIMO.

Wakati Mondlane anakufa Josina alikuwa na mimba ya Samora Machel ambayo baadaye ilimleta duniani mtoto wao aliyeitwa Samito. Josina na Samora walifunga ndoa huko wilayani Tunduru katika kambi ya Jeshi ya FRELIMO. Katika harusi ile makamanda wote walihudhuria akiwemo Rais wa sasa wa Msumbiji Armando Guebuza na Rais aliyetangulia Joachim Chisano na Makamu wa Rais Marcelino Dos Santos. Aliyefungisha ndoa ile ni Uria Simango ambaye baadaye alikosana na wenzake na kunyongwa huko Niassa. Hivi sasa watoto wa Simango ambaye alikuwa Rais mwenza wa FRELIMO ni viongozi wakuu wa chama cha upinzani cha MDM na kabla ya hapo walikuwa katika chama cha RENAMO. Davis Simango ni Rais wa MDM na Mhandisi Uteri Simango ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni. MDM ni chama kilichojimega kutoka chama kikuu cha upinzani nchini humo cha RENAMO. Chama cha RENAMO kina mahusiano ya kisiasa na kimwelekeo na chama cha CHADEMA hapa nchini Tanzania. RENAMO ni chama chenye rekodi mbaya sana ya kutesa na kuua wananchi wakati wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Msumbiji. Mwezi Julai mwaka 1987 katika kijiji cha Homoine jimbo la Gaza, RENAMO ilichinja wagonjwa wote 424 waliokuwa wamelazwa hospitalini. Vile vile RENAMO walikuwa wanachukua watoto wachanga na kuamuru wazazi wao kuwaweka kwenye kinu na kuwatwanga mpaka wanakufa.

Baada ya kujifungua Josina alimwacha mtoto wake Dar es Salaam na kwenda kwenye maeneo yaliyokombolewa (liberated zones) ambapo alikuwa anasimamia elimu ya ustawi wa Jamii. Jimbo la Niassa na Cabo Delgado ndio maeneo yaliyokombolewa mapema. Nakumbuka kusoma kwenye kitabu cha Yoweri Museveni ‘Sowing the mustered seed’ kwamba yeye Yoweri Museveni na Jenerali Ulimwengu wakiwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliambatana na Ferdinand Ruhinda kutembelea maeneo yaliyokombolewa. Museveni katika vita yake nchini Uganda alitumia njia hii ya ‘liberated zones’ katika kushika maeneo na kuweka utawala unaofaa.

Josina Machel alifariki dunia mwezi Aprili, 1971 inasemekana kwa ugonjwa wa kansa ya ini. Hata hivyo kuna maneno yaliyozagaa jijini Dar es Salaam kwamba inawezekana Josina alikufa kwa sumu. Samora Machel alilia sana kwenye moja ya vikao vya FRELIMO na baadaye aliandika shairi ‘haujafa Josina’. Kana kwamba Josina alijua atakufa, pale alipokuwa dhaifu sana aliondoka Cabo Delgado na kukabidhi silaha yake kwa makamanda wenzake. Maneno ya mwisho ya Josina yalikuwa “Makamaradi, siwezi kuendelea tena. Mpeni silaha yangu hii Kamanda mkuu wa Jimbo kwani itasaidia katika ukombozi wa watu wa Msumbiji”. Nchini Msumbiji tarehe 7 Aprili ni siku ya Wanawake kama kumbukumbu ya Josina Muthemba Machel.

Ni nani ambaye asingependa kuwa na Mke kama Josina? Basi angalau binti yako kama unamsoma Josina baada ya kuwa umeoa.
 
Nafikiri ujumbe wako upa hapa Bwana Zitto.......

.......MDM ni chama kilichojimega kutoka chama kikuu cha upinzani nchini humo cha RENAMO. Chama cha RENAMO kina mahusiano ya kisiasa na kimwelekeo na chama cha CHADEMA hapa nchini Tanzania. RENAMO ni chama chenye rekodi mbaya sana ya kutesa na kuua wananchi wakati wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Msumbiji. Mwezi Julai mwaka 1987 katika kijiji cha Homoine jimbo la Gaza, RENAMO ilichinja wagonjwa wote 424 waliokuwa wamelazwa hospitalini. Vile vile RENAMO walikuwa wanachukua watoto wachanga na kuamuru wazazi wao kuwaweka kwenye kinu na kuwatwanga mpaka wanakufa......
 
Hata ndege ,sgr ,bwawa la umeme, uchumi wa kati ,haviwezi kukamilika bila kumtaja Magufuli
 
Zitto asante kwa historia ya mwanamapinduzi huyu, siku zote nimekuwa nikitamani kusoma habari zake kwa lugha ya Kiswahili...
 
Chama cha RENAMO kina mahusiano ya kisiasa na kimwelekeo na chama cha CHADEMA hapa nchini Tanzania. RENAMO ni chama chenye rekodi mbaya sana ya kutesa na kuua wananchi wakati wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Msumbiji
Aisee...
 
Ahsante Sana zitto
 
Uhusiano wa Chadema na RENAMO uko kwenye nini ?
 
Nafikiri ujumbe wako upa hapa Bwana Zitto.......

.......MDM ni chama kilichojimega kutoka chama kikuu cha upinzani nchini humo cha RENAMO. Chama cha RENAMO kina mahusiano ya kisiasa na kimwelekeo na chama cha CHADEMA hapa nchini Tanzania. RENAMO ni chama chenye rekodi mbaya sana ya kutesa na kuua wananchi wakati wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Msumbiji. Mwezi Julai mwaka 1987 katika kijiji cha Homoine jimbo la Gaza, RENAMO ilichinja wagonjwa wote 424 waliokuwa wamelazwa hospitalini. Vile vile RENAMO walikuwa wanachukua watoto wachanga na kuamuru wazazi wao kuwaweka kwenye kinu na kuwatwanga mpaka wanakufa......
Kama hicho chama kilikuwa na tabia hizo alafu leo kina mahusiano na chadema, basi chadema ni chama cha hovyo
 
.....Chama cha RENAMO kina mahusiano ya kisiasa na kimwelekeo na chama cha CHADEMA hapa nchini Tanzania. RENAMO ni chama chenye rekodi mbaya sana ya kutesa na kuua wananchi wakati wa vita vya wenywe kwa wenyewe nchini Msumbiji....

Zitto unafiki wako dhidi ya wapenda mabadiliko ya kweli na wapigania demokrasia ya kweli ni raisi sana kuutambua!!!

Chuki yako ni kubwa sana dhidi ya CHADEMA, nafikiri huna tofauti na mtoto ambae yuko tayari kumuua mama yake mzazi aliembeba tumboni na kumtunza utotoni hadi balehe!!

Umeiingiza CHADEMA kwenye paragraph ya mauaji,CHADEMA hiyo imeandikwa kwenye hicho kitabu?!! Kulikua kuna ulazima wa kuiandika CHADEMA?!!

Lengo lako kuendelea kuhadaa kua Mbowe ni gaidi aombe msamaha?!!

Zitto nakumbuka miaka ile ulipokua na Mwigulu Nchemba huku ukiwa kiongozi wa CHADEMA na ukashiriki kumpa platform Mwigulu amchafue Lwakatare kua ni gaidi,huku ukifurahia na maneno hayo yakaletwa bungeni na Lwakatare mkamtesa ila hatimae haki ikashinda!!

Historia ya wanasiasa wa Kigoma siku zote wamekua ni malaya wa kisiasa huku wakiwa vibaraka wakuu wa CCM,nawe unatoka Kigoma!!

Wasiofuatilia nitawakumbusha. Moses Machali,Mkosamali,Kafulila na pia Marehemu Dr Wade Kabouro ambae aliwahi kuhudumu kama Katibu Mkuu wa CHADEMA (huyu aliwahi kusema siku akirudi CCM amlale mama yake mzazi,well,kafa akiwa CCM pale Lumumba)

Taifa lenye watu wanafiki ni ngumu sana kustawi kwenye haki na utu wa dhati!!
 
Key point
"RENAMO kina uhusiano wa kisiasa na Chadema"....

Renamo kiliua sana watu miaka ya 1980"

Mimi sio mfurukutwa wa vyama vya siasa, hivyo hiyo sehemu haina mashiko kwangu...

Nina sababu ya kuvutiwa na harakati za mwanamama/mwanamapinduzi Josina
 
Back
Top Bottom