Joshua Nassari MB.

Fredrick Sanga.
Dogo Nassari anaropoka sana muwekeni chini mfahamisheni siasa za Tanzania zilivyo.

Wewe ndio inaelekea unatumia makamasi katika kuchambua haya maswala, kwani wewe kwa upeo wako mfupi unafikiri siasa ya Tanzania ipo vipi yaani kwa mfano niki kuliza...?
 
Last edited by a moderator:
Habari zenu wana JF...!

Nimesikitishwa na suala la Joshua Nassari kushambuliwa kama mpira wa kona bila sababu ya msingi..,kisa tu aliimwaga CCM kwenye uchaguzi arumeru na pia kukataa mamilioni ya CCM kuisaliti CHADEMA..!

Hao wanaoshambulia Nasari wapo makundi mawili, kuna CCM, ambao wanajubu mapigo ya kushindwa, huku wakiwatumia wahariri wa Magazeti ya MWANANCHI na NIPASHE, vile vile na baadhi ya watu ambao hawajui nini maana ya Siasa, wanafuata tu mkumbo..,maanak siku hizi imezuka kasumba kila mtu mwanasiasa!

Wanaosema NASSARI msaliti nia yao ni moja tu.,,kuibomoa CHADEMA..! na sasa wanahakikisha wanamgombinisha NASSARI na baadhi ya wabunge na Viongozi CHADEMA, mfano wa habari ya leo iliyoandikwa kwenye gazeti la MTANZANIA chini ya BASHE..,"ETI KWAMBA MBOWE AMEZIMA UASI CHADEMA" hii kauli ni ya uchochezi dhidi ya CHADEMA..,

Wanaosema NASSARI ni msaliti, hawataishia tu hapo watasema vincet msaliti,Godbless lema msaliti, na mwisho hata Dk.Slaa msaliti..,

Kama Nassari angekuwa pandikizi..,Lazima angewezesha CCM ishinde uchaguzi wa Arumeru, kwani LOWASSA NA BEN MKAPA wasingekubali kudhalilika, na hata kukubali mamilioni waliotumia kuteketea bila kushinda..kwakuwa CCM wanajulikana kwa kulaziimisha matokeo na kuchakachua kura
 

Sikia usiwe na hofu wala usi mm underestimate Dogo Janja kumbuka mweshimiwa mwenyewe mku wa anga alisema hiyo ilikuwa ni hamasa tuuu....... usijali hakitengwi kitu hapa...!
 
"Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"

Nini tatizo la kauli hii, mbona kuna kauli mbaya kuliko hii zimewahi kutolewa tena na viongozi wakuu wa nchi? Zanzibar ni nchi, Kimbau (Mafia iwe nchi), Kigoma ijiunge na Burundi, Kanda ya kusini ijitenge nk nk. Binafsi nilisikitishwa sana na kauli zake za mwanzo alipomtisha rais asifike Arusha, zilinisikitisha lakini zinafundisha. Funzo ni kwamba wananchi wanataka maendeleo ni sawa na mtoto anaposema leo baba usiponiletea kitabu nakufungia mlango, kimatendo ni mbaya lakini kiuhalisia yuko sahihi.

Nassari ni Nassari kamwe hatuwezi kumbadilisha. Kwa akili yake alipoona kauli zake za mwanzo zimechukuliwa tofauti akadhani kujutia aliyoyasema ni kusema 'kwani mimi ni nani mbona ni mdogo sana?' Sisi tunaweza kumshangaa lakini bado na yeye atazidi kutushangaa, na tukiendelea kumshangaa tusione ajabu akaja na kauli itakayotushangaza zaidi.

Hakuna kauli inayokuja kwa bahati mbaya, kauli za bwana 'mdogo' si za bahati mbaya is a wakeup note kwa utawala wetu ujue kumbe kuna watu wanamawazo ya kujitenga. Kinachotakiwa kwa serikali ni kujiuliza tatizo ni nini, ni 'kitabu' watu wanataka maendeleo. Kama serikali ina mwona Nassari ni mwehu na inakimbizana naye inaweza kuaibika zaidi. Kumbuka amesema yeye 'mdogo' hana hata platoon wao wana kikosi cha jeshi, ni aibu iliyoje kwa mkuu wa nchi mwenye maximum security kuogopa kwenda Arusha eti ametishwa na matamko ya Nassari.

Zanzibar kuna kikundi kiitwacho 'UAMSHO' hiki si kikundi cha siasa, wao si tu wanatoa matamko kama alivyofanya Nassari bali wanafanya kwa vitendo. Hivi sasa kuna watu wanakusanya sahihi za kuuvunja muungano na rais anajua, nafikiri hilo ndilo serious zaidi. Tutakuwa wanafiki kumzuia mtu mmoja anayetoa kauli huku tukiacha kundi cha watu mia likiendelea. Narudia tena sikufurahishwa na kauli za Nassari hasa zile za kwanza lakini nafarijika zimetoa somo fulani kwa jamii na watawala.
 
Wewe ndio inaelekea unatumia makamasi katika kuchambua haya maswala, kwani wewe kwa upeo wako mfupi unafikiri siasa ya Tanzania ipo vipi yaani kwa mfano niki kuliza...?

Pro-Chadema JF wengi ni wachanga kwenye siasa hivi hunaweza kumpiga marufuku Rais wa Tanzania kwenda Arusha? Akili za kitoto kabisa hizi
 
Kweli huyu dogo anahitaji semina elekezi. Wewe tayari ni mbunge, maana yake wanachi wote katika jimbo lako wanawakilishwa na wewe. Ukisema wanaona Jimbo lako limesema. Sasa ukija na sababu za udogo wakati wewe ni mbunge naona kama hujui unachoongea. Nafikiri jifunze kujifunza kwanza, na kukaa kimya ni busara.
 
Leo baada ya mahojiano na polisi Arusha mjini zaidi ya masaa sita,Nassari akiongea na waandishi wa habari alisema "Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"

Source;ITV News 2000hrs*
Mdogo ki umri au ki akili,kama ni yote mawili,nawahurumia wananchi wa Arumeru.
 
Mwanakijiji kidogo huwa tunakuheshimu lakini naona una mwelekeo wa kukuza hili jambo tena kwa tafsiri ya hatari kuliko hao mapolisi.Wewe mtu anayesema eti Rais ajaye hatatoka kaskazini ya Tanzania na kwamba jina lake analo JK, na kwa siku zote hizi Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu haijakanusha(ikiwa imejitahidi kukataa habari za JK kupewa hongo ya suti,kupikwa kwa hukumu ya kesi ya Lema na matukio mengine) unaelewa uzito wa maneno yake kwa sisi watanzania wa kaskazini au hata mtanzania asiye wa kaskazini mwenye akili kidogo?
Kwa kweli kama POLISI wameshapoteza RELEVANCE ushahidi upo Arusha.Mbeya jamaa walimrushia mawe JK kweupee mkasema ni walevi wale?Wale ni watu walioonesha kutokuridhishwa na mfumo na wanajua hata risasi za moto zingeliweza kuwapitia lakini wakajitolea.
Naomba usiwe mwoga kiasi hiki ndugu mwanakijiji tena muunge mkono NASSARI na wewe usimame uwe tayari kuhesabiwa,kwa risasi,virungu,tindikali,ama powder za Russia/Ukraine!
 
Inavyoonesha bado Nasari anasumbuliwa na bangi alizovuta sekondari.
 
Pro-Chadema JF wengi ni wachanga kwenye siasa hivi hunaweza kumpiga marufuku Rais wa Tanzania kwenda Arusha? Akili za kitoto kabisa hizi
Wewe unayeshangaa hayo ndiye mchanga kwenye siasa kuwa uyaone, kuna nchi zimewahi kujitenga kwa sababu ya serikali kutojali matatizo ya sehemu moja. Halafu mkuu uko addicted sana na 'H'.
 
I doubt the mental ability politically of Nassari on issues...
he talks cheaply & lightly ..... kuanzia sasa kumbe JJ Mnyika ni very matured, huyu kwa CDM wamchunge naona atachafua CDM kwa maneno....

You might be out of your senses 4sure kwani wewe una vipimo vya I.Q ya mtuu kwa kutumia your own selfishness point of view n thinking capacity ama ni vipi yaani? Dont ever under estimate a person kwa mtazamo wako duni wa siku moja2, keep in mind whenever your right no one remembers while when you wrong no one forgets.... dont act like a layman if u dont happen to be one....!
 

Kwa taarifa yako mimi mrdash1 nimezaliwa na kukulia kanda ya ziwa, kata yangu ya kiriba, musoma (V) imezungukwa na ziwa Victoria lakini hakuna hata kijiji kimoja chenye maji ya bomba, bado mama na dada zetu wanabeba ndoo za maji vichwani kutoka ziwani hadi majumani mwao, wanatembea km 0 - 5 kulingana na mahala makazi yao yalipo kutoka ufukwe wa ziwahalafu wewe lofa wa fikara ndo unataka kutuambia nini hapa?? Kwamba ccm ni ya kitaifa na inaliendeleza taifa???? kwa taarifa yako ccm ni kampuni ya mafisadi na wahujumu uchumi inayomiliki nguvu za dola
 
Wewe unayeshangaa hayo ndiye mchanga kwenye siasa kuwa uyaone, kuna nchi zimewahi kujitenga kwa sababu ya serikali kutojali matatizo ya sehemu moja. Halafu mkuu uko addicted sana na 'H'.

Kumbe ni kweli Chadema mnataka kujitenga...
 
Kumbe ni kweli Chadema mnataka kujitenga...

Tumia akili wewe, usiwe kama pimbi wa madoadoa wacha kuropoka kama umekalia *****. Wewe una uwakika gani na unayo yasema....?
 
Pro-Chadema JF wengi ni wachanga kwenye siasa hivi hunaweza kumpiga marufuku Rais wa Tanzania kwenda Arusha? Akili za kitoto kabisa hizi

Listen bwana being pro haijalishi unadhania utajifunzaje bila kukosea, isitoshe kuwa pro ama senior jf haitoshi kupima uchanga na uelewa wa mtuu. Mbona wazee wazima wa CCM hawana jipya mfano mtu kama Wasira na Chenge wao unavyo hisi hadi leo hii wamekomaaa kisiasa kweli.? Haimanishi unaweza kumpiga marufuku raisi kwenda arusha, besides mwenyekiti Mbowe alishawaeleza yakuwa ile ilikuwa ni hamasa ilio jaa shahuku2 ya kuonyesha kuchoshwa na ushenzi wa chama tawala CCM kinachongozwa na huyo aitwaye raisi wa Tanzania. Na jibu la swali lako nadhani nimekujibu....!
 


Mkuu Mungii, wewe ni mojawapo ya watu ninao waheshimu sana katika jukaa hili ila unaanza kunipa wasiwasi.
1. Kwamba hukubaliana na kauli ya 'Dogo Janja' na pia "pumba" za MMK nikujikanganya maana hoja ya msingi ya Mzee Mwanakijiji inapinga kauli ambayo unasema hukubaliana nayo.

2. Hizi tabia za kutenganisha chama na viongozi wake ni tabia za CCM, " chama ni kizuri ila viongozi ndo wabovu" na si Chadema. NASARI NI KIONGOZI NA KIONGOZI NI TASWIRA. Anabeba sura ya taasisi/watu anaowaogoza na Nasari anapaswa kuwa hivyo. Kujaribu kumtenganisha Nasari na Chadema unakosea

3. Kinachobishaniwa hapa si sababu zilizomplekea Nasari kusema aliyo yasema. Kinacho jadiliwa/bishaniwa nikwamba Nasari alikosa hekima kueleza alichokikusudia. Moja ya Sifa kuu za kiongozi ni kuwa na hekima/busara. Kwa lugha nyepesi uwezo wa kutambua kitu gani unapaswa kufanya/kusemea na kwa wakati gani. Wakati huo uwe wa furaha au huzuni, sherehe au majonzi. Maranyingi uwezo wa kiongozi unajidhihilisha katika kutatua matatizo kwenye complex situations.

4. Ni utamaduni humu janvini kwa wanajanvi hukubaliana na kupongeza ama kupinga hoja za wenzao. Katika kuonyesha kuikubali hoja wengine hutumia "LIKE" na wengine hueleza hisia zao kwa kuandika na umekuwa ukifanya ama kufanyiwa hivyo karibia kila siko. Nadhani hauko sahihi kumbwambia mwenzio anajikomba kwa Mwanakijiji.

5. Hii tabia ya kulinganisha uovu kwa uovu sio nzuri na bora tukaizika.

6. Ninaanza kupata hisia kuwa baadhi ya vijana wa kasikazini wamenasa kwenye mtego wa CCM. Mtego wa kutumia ukanda/ukabila kuigawa CDM. Kuweni makini makini tena makini. Siku mkianza kujiona zaidi wanaarusha kuliko wanachadema, huo ndo utakuwa mwanzo wa kudidimia kwa harakati hizi ambazo sote ni wadau.


MKUU MUNGI MIMI NA WEWE TU WAPENZI WA CHADEMA LAKINI USIPENDE KUWA MPENZI KIPOFU
 
Suala la udogo na kugawa nchi haviingiliani kabisa!!! Hapa kikubwa ni nguvu ya ushawishi, kwani wakina Martin Luther walivokuwa wanafanya movement walikuwa watu wazima????

Nafikiri CDM ni kuwa makini na zaidi ni kumrudisha dogo Nasari jikoni apikwe upya kabla yakupewa mic na kuingia Majukwaani. Maana kunawatu wapo tayari na makini kunote makosa ili watokee humo. Nasari uwe makini na Kauli zako, wewe ni Mbunge ni Public figure maneno unayoyasema sisi tunayapa uzito!! Usijifanye hamnazo...
 

umeniwahi mzee mwanakijiji! .... nilitaka kuliongea hili ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…