Joshua Nassari aiombe radhi CHADEMA

Joshua Nassari aiombe radhi CHADEMA

Siasa za chuki na kubaguana/kutengana kwenye kilajambo ni za ujinga. Kama kunajambo la kheri na la maendeleo hatunabudi sisisote tujuike kulifurahia, likija jambo la hovyo tutapingana na kuonesha hatupo pamoja.
Nassary alikua sawa kuwepo na wananchi wenzake ktk shughuli ile, Magufuli alitania kama kawaida yake sasa Nassary angelia au? Nilikuwepo ple na ilikuwa jambo jema sana PIA ningeshangaa kama mbunge asingekuwepo
 
Mkuu umempa kumbukumbu nzuri sana...Huyu Marandu kaletwa na Lowassa chadema na ameshaanza kuwaadhibu aliowakuta.
Tulisema sana Lowasa na genge lake wataivuruga CDM ona sasa huyu nyumbu wa 4u movement alichokileta hapa kumchonganisha nasari wa wapiga kura wake.
 
Umempa ushauri mzuri, lakini umechanganya na jazba nyingi mno nakufanya kupoteza maana ya ushauli.
Magufuli ni mtu wa kupenda kuchomekea, ndio maana akikuwa akijinadi kuwa yeye ni M4C, Hivyo, ndugu yangu km amefanya mema mengi jimboni kwake, kwa hili baya moja tumsamehe na tumvumilie
Asante
 
Punguza povu, kutukana hakuwezi kukusaidia kueleweka....u can use normal language na ukaeleweka.....

The way i see u just deviate from strong point here.....I'm talking about Nassari involvement to his people and accountability in helping them......wewe unamshtumu bila sababu za msingi.

Wewe CCM Unampenda zaidi Nassari, Kuliko Mliokuwa Mkiwapiga mabomu Kamapeni za Arusha?
 
Umempa ushauri mzuri, lakini umechanganya na jazba nyingi mno nakufanya kupoteza maana ya ushauli.
Magufuli ni mtu wa kupenda kuchomekea, ndio maana akikuwa akijinadi kuwa yeye ni M4C, Hivyo, ndugu yangu km amefanya mema mengi jimboni kwake, kwa hili baya moja tumsamehe na tumvumilie
Asante

Asira yangu Kubwa Ni kwa wanaojifanya wanamtetea lakini Ni Maccm
 
Kosa la Nassary ni lipi? Mbowe ndio awe wa kwanza kuwaomba radhi kwa kuwaletea fisadi Lowasa!

Mzalendo Nassari usichoke ...
Ina maana hujaona kosa la Nassary? Kosa la Nassary ni kujipendekeza kwa majizi ya CCM.
ni hatari sana ukiona wewe ni CHADEMA halafu liCCM linakusifia, tangu lini shetani akamsifia Mungu?
 
Kwa hiyo TL Marandu hoja yako hapa ni kauli ya JPM ya ;

"...Nassari usoni ni CHADEMA lakini moyoni ni CCM....", siyo?

Aaah mzee wangu, hii mbona ni kauli ya kawaida ya kisiasa tu??

Sawa tu na upinzani unavyomrushia makombora yeye mwenyewe Pombe Magufuli kwamba, usoni ni CCM lakini moyoni ni MPINZANI halisi kwa sababu ndiyo maana anatekeleza hata yale yaliyolalamikiwa na upinzani miaka na miaka kwa mtindo wa kutumbua majipu!

Na kwa hakika sioni sababu ya Joshua Nassari kama alikuwa na nafasi hiyo kujumuika ktk ziara ya Rais na especially kama baadhi ya mambo aliyokuwa anashughulikia Rais yalikuwa yanahusu jimbo lake!

Jana nilimwona Waziri wa Ardhi Bwana William Lukuvi kupitia TV akiwa jimboni kwa Halima Mdee (jimbo la Kawe) kutatua mgogoro wa ardhi wa eneo la Chasimba dhidi ya mwekezaji mmoja

Ofcoz Mbunge mwenyewe wa jimbo lilipo eneo la mgogoro hakuwepo, lakini kwa sababu ya ishu yenyewe ilivyo nadhani chama au Halima mwenyewe alimuomba mbunge wa jimbo la Ubungo Bw Saed Kubenea kumwakilisha na mambo yalikwenda vizuri tu na tunaambiwa mgogoro umeisha.

I think hii ishu si kubwa kwa kiwango hiki na after all wote tunajua tatizo la Rais wetu Bw Pombe Magufuli kwamba, kupitia kauli zake anaweza kuzua tafrani wakati wowote mahali popote juu ya jambo lolote na kwa mtu yeyote hata kama kiuhalisia ndivyo sivyo!!

Wewe si unakumbuka kauli yake juu ya Crisis ya Zanzibar alipokuwa anaongea na wazee wa Dsm, kwamba hataongea chochote kuhusu mgogoro huo kwa sbb atakuwa anaingilia maamuzi ya tume - ZEC!? Ulimuamini?

Si kwamba wengi tulimpinga waziwazi humu kwa hoja, kwamba ana wajibu wa kuingilia na kuutatua mgogoro huo kwa sababu yy ndiye kinara wa JMT na Zenj ikiwa sehemu ya JMT?....Leo unamshangaa kweli huyu mheshimiwa Rais!!?

Mwelewe Magufuli na ukishamwelewa hutapata taabu. Zaidi sana naye anatakiwa atafutiwe kijembe cha kisiasa tu, apigwe nacho na mchezo unaishia hapo.

Binafsi, sioni tatizo la mbunge wa Arumeru Mashariki, ndg J. Nassari ktk hili jambo. So let it go, hakuna tatizo lolote!.
 
Wewe CCM Unampenda zaidi Nassari, Kuliko Mliokuwa Mkiwapiga mabomu Kamapeni za Arusha?
I'm swing voter.....I'm no align to any political party in Tanzania......u can brand me any name u like.....i don't care
 
I'm swing voter.....I'm no align to any political party in Tanzania......u can brand me any name u like.....i don't care

If you are, then you should be the very first person to Understand me, Do you think if Obama a Democrat facilitate the arrest of let say Senator Richard Shelby the Republican for fictitious political shenanigans, The Next day Senator John Mc Cain will be palling around with Obama? if he does will it not be an endorsement of his actions. Don't you think this will be interpreted as a misguided effort to embolden or strengthen the oppressor's hand if you will? think about it.
 
Mleta mada, siku zote mawazo yako yanafanana na mtu anayeishi na wivu mwingi pamoja na kinyongo kisicho na mipaka. Unaanza kumtafutia uadui Joshua Nassari, mbunge kijana ambaye alikuwa tayari hata kufunga safari kwenda mashariki ya mbali ili mradi tu atafute vifaa vya hospitali kwa ajili ya wagonjwa wa jimbo lake. Kusifiwa na Rais ambaye ni mwanaccm kuna ubaya gani?. Maendeleo hayana chama wala itikadi, achana na fikra mgando.
 
Kabisa watu hawaoni matusi ya magufuli kwa Nasari na Chadema??!!aisee kweli siasa ni upofu.mtu anakuonyesha kuwa hujazaliwa na baba sahihi na unachekelea kwamba siasa sio uadui.je kudhalilishwa kwa madiwani Ukawa kina Lijualikali sio uadui huo.
 
Mleta mada, siku zote mawazo yako yanafanana na mtu anayeishi na wivu mwingi pamoja na kinyongo kisicho na mipaka. Unaanza kumtafutia uadui Joshua Nassari, mbunge kijana ambaye alikuwa tayari hata kufunga safari kwenda mashariki ya mbali ili mradi tu atafute vifaa vya hospitali kwa ajili ya wagonjwa wa jimbo lake. Kusifiwa na Rais ambaye ni mwanaccm kuna ubaya gani?. Maendeleo hayana chama wala itikadi, achana na fikra mgando.
kulikuwa na tatizo gani kama angepongezwa bila kutukaniwa chama.msitufanye watu wote wasenge.tazama wanaUKAWA wanavyodhalilika namna hii na dola kwa maelekezo ya ccm bila Magufuli kukemea.halafu mpuuzi mmoja anasema siasa sio uadui
 
kulikuwa na tatizo gani kama angepongezwa bila kutukaniwa chama.
Zaidi ya matusi mheshimiwa mkuu wa nchi hakuongea maneno ya kiungwana?. Magufuli alishawahi kwenda jimboni kwa Mbowe akiwa waziri na akatoa ushirikiano mkubwa. Zitto alitafutiwa ubaya mioyoni mwa watu kupitia maneno maneno ya kimajungumajungu kama haya ya mleta mada, lakini Zitto ni mtu muhimu sana kwenye opposition. Nassari ni hazina ya baadae ya siasa za nchi hii, tusianze kujifanya wasafi kwa kuwachafua wengine, wakati hakuna mkamilifu anayetembea chini ya jua.
 
Hizi akili za kuazima zina walakini sana! Yaani mleta uzi unataka AOMBE RADHI KWA KUAMBIWA HIVYO?
 
Zaidi ya matusi mheshimiwa mkuu wa nchi hakuongea maneno ya kiungwana?. Magufuli alishawahi kwenda jimboni kwa Mbowe akiwa waziri na akatoa ushirikiano mkubwa. Zitto alitafutiwa ubaya mioyoni mwa watu kupitia maneno maneno ya kimajungumajungu kama haya ya mleta mada, lakini Zitto ni mtu muhimu sana kwenye opposition. Nassari ni hazina ya baadae ya siasa za nchi hii, tusianze kujifanya wasafi kwa kuwachafua wengine, wakati hakuna mkamilifu anayetembea chini ya jua.
hivi unaelewa mada kweli wewe
 
Noted mimi natokea Meru ni muda tu haujafika he has to quit! No compromise na anayemzika mazima ni mkuu wa Wilaya huyu ametokea kuwa karibu sana na wana Meru kuliko hata mbunge na mkuu huyu wa wilaya ana tengeneza njia nyeupe kwa mgombea wa ccm atakayekuja. Nasari haonekani ibadani wala kwingineko. .....anyway mambo yake ni complicated sana. CDM bado tunaipenda SANA
 
Ni vyema limeandikwa ili ajitafakari. Kwa hali ilivyo sasa hapa nchini kwa UKAWA kudhalilishwa kisa CCM wachukue umeya hakuna jinsi mtu wa CCM atasifia mtu wa UKAWA kwa nia nzuri hata kidogo!

UKAWA unagandamizwa kwa gharama kubwa sana ambayo inaumiza wananchi kimya kimya tu! Gharama za kurudia uchaguzi Zenj, Kuahirisha uchaguzi wa meya wa Jiji la Dar! Inakera mno!
 
hivi unaelewa mada kweli wewe
Vijembe kwenye siasa ni vitu vya kawaida sana, moyoni ni CCM, kwa hiyo?. Mleta mada anakuza vitu vidogo vidogo, lakini wasi wasi ni kwamba wasomaji tunatofautiana kwenye uelewa, wasije wakaibuka wengine wakaanza kumchukia Nassari kwa sababu tu rais kaongea utani. Halima Mdee alishawahi kumsifia huyu huyu rais, ukiyachukulia mambo kwa uchungu utaishia kuwa mlalamikaji aliyekubuhu.
 
Kwanza Marandu inabidi uombe radhi kwa kuongezea maneno ya uwongo.Magufuli hakusema ndani ni ccm,alisema ndani mpenda maendeleo. Lakini tuulizane hapa,Nassari alikuwa pekee mtu wa chadema pale kwenye mapokezi? Kwa nini asakamwe yeye tu.
Kulikuwa na Mh Meya wa jiji la Arusha,kulikuwa watu wengi tu wa chadema. Pili Mh Msigwa alimpokea waziri mkuu Mjaliwa lakini hayajasemwa. Tatu Mbunge Mh prof Jay juzi alikuwa na waziri wa mifugo jimboni kwake kutatua mgigoro wa wakulima wa miwa,mbona haulizwi chochote?
Mkuu kama hukusikiliza wakati Magufuli anamsifia Nassary bora ungepiga kimya tu. Kuliko kuandika maneno ya uongo hapa!
 
Back
Top Bottom