Joshua Nassari aiombe radhi CHADEMA

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Niliona tetesi Jana, za habari ya Magufuli akimsifia Joshua Nassari, Kuwa Ni Kijana safi, ambaye Usoni ni Chadema lakini Ndani ni CCM. Haya yalikuwa Ni matusi ya Magufuli kwa Chadema kumtumia Nassari. Ni aibu sana na ni Unafiki Kusema ati mtu safi anayefanya Mema na anayetenda haki Ndani Ni CCM. Ni CCM ipi? Iliyoiba Ushindi wa Urais Bara? Iliyofuta Ushindi wa Zanzibar? Inayohaha Kila Mahali Kuiba Nafasi za Umeya? Iliyowarudisha wezi wote wa Escrow kwenye madaraka? Iliyokalia Uchafu wa Muhimbili, badari, TRA etc? CCM ipi ambayo huyu anazungumzia?

Najua Siku za Nyuma, Mwenyekiti Mbowe alishahudhuria na Kumsifia Kikwete na Magufuli katika Ufuunguzi wa Barabara. Lakini hakufanya hivyo wakati Wabunge na Madiwani wa Chadema wakiwa wamekamatwa na Kufuunguliwa Kesi za Kishenzi. Alichokosea Nassari ni Timing, Kuwepo kwake Ziara za Magufuli kama Kimalaya fulani, Kumemfanya Magufuli amtumie sawia kujihalalisha na Kutukana Vyama.

Joshua Nassari bwana mdogo, Nikuambie Kuwa alichokupa Magufuli sio Sifa Ni Matusi, Nimekuona Kwenye Gazeti Ukichekelea kama juha, kwa sababu hutumii akili. Wakati akina Halima Mdee, Wabunge na Madiwani wa Chadema wakiwa Rumande wewe unapeleka maninii kwenye Ziara za anayetuma unyama huu.

Na Kama Ulilazamika Kwenda, Ulitakiwa Palepale baada ya Kikao Ukanushe, "Sifa" Zile na Useme wewe Upo pale Kama mbunge wa UKAWA na Huoni sawa Kufananishwa na CCM.

Mwisho Nikuambie Nassari Mwanangu, Ulichofanya Ni sawa na Kuwapiga Mateke ya Puani na Masikio, watu mmoja mmoja wa Chadema waliopigwa na Polisi, waliowekwe jela, waliokesha waliotoa fedha, waliokupigania kuwa Mbunge. Ukitaka Kujua CCM hawana Maslahi Na wewe Mwangalie Ole Sendeka! And you are very light weight compered to many! Hata Nikikusikiliza Bungeni Joshua Wewe bado Kabisa Kukua, angalia Usijinyonge Kisiasa.

Na Kwa Ukawa Kama Josua Hatatubu, Mvumilieni amalize Muda wake, lakini akimaliza aende atakako. Msimpe tena Tiketi ya Kugombea Ubunge Arumeru. Ni bora jimbo lipotee Kuliko kuwa na Mbunge anayesaliti Wenzake waliompigania
 
Sasa mtu akijitokeza akikusifia mbele ya umati wa watu unaomba tatizo ni lake au lako? Wewe hujafanya chochote na hutakiwi kuomba radhi
 
Sasa mtu akijitokeza akikusifia mbele ya umati wa watu unaomba tatizo ni lake au lako? Wewe hujafanya chochote na hutakiwi kuomba radhi

Umesoma tu Kichwa cha habari cha uzi, Usingejibu hivi!
 
Noted mimi natokea Meru ni muda tu haujafika he has to quit! No compromise na anayemzika mazima ni mkuu wa Wilaya huyu ametokea kuwa karibu sana na wana Meru kuliko hata mbunge na mkuu huyu wa wilaya ana tengeneza njia nyeupe kwa mgombea wa ccm atakayekuja. Nasari haonekani ibadani wala kwingineko. .....anyway mambo yake ni complicated sana. CDM bado tunaipenda SANA
 
Ok. Sasa naona baadhi yenu Chadema mnataka kufanya siasa za ufanatics.

Hiyo siasa ya "you are either with us or you are against us" ni siasa ya kizamani, ya kutumia nguvu bila akili.

Nassari simjui kabisa japo nimeishi kwa miaka mitatu jimboni kwake.

Ila kitu kimoja nakijua. Nassari amewekwa jimboni na wana arumemeru awe chachu ya maendeleo yao kama mwakilishi wao bungeni.

Hawajamweka pale kuonyeshana ubabe na Magufuli.

Siyo interest yao, siyo interest yake, na kiuhalisia -- na sisi wananchi tunaona-- kama Chadema itajikita kuonyeshana ubabe na Magufuli, huo ndo mwanzo wa mwisho wa Chadema.
 
Sijui tatizo la Joshua ni lipi ,Raisi anapokua mkoa wowote ni kina nani wanaruhusiwa kumpokea ?? Barabara inayofunguliwa inapita pia na jimboni kwa Nasari ,shida iko wapi ?? Ni Magufuli huyu huyu alimwombea Mrema Augustino kura japo hakua mwana ccm ,kama lema na Nasari wana matatizo yao ufanywe utaratibu wa kuwapatanisha ndani ya chama ,vinginevyo watazua mgogoro usiokua na maana
 
Kuna ukweli kauli ya jana JPM kuhusu vyama ni ya kidictator mbele ya madictator wenzie, isiyo na busara wala hekima.

As for Nasari natumaini anajua anachokifanya na athari zake. Kuna wengi tunaosononeshwa na mwenendo wake wa sasa.
 
Na umeya dar na kilombero na jipu la Zanzibar halafu unammchekea magufuli wa nini!
 
Someni Kabla Hamjajibu, Mimi Joshua simjui Kiundani wala Sina Chuki naye, Nimetathmini yaliyotokea na Haivumiliki. Kama anajitambua alitakiwa amsahihishe Magufuli, Huwezi Kukubali Kutumiwa Kuwatukana wenzako waliokufikisha ulipo. Na Pia kwa yaliyokuwa yakiendelea Huko Dar es salaam na Kilombero, Joshua Nassari hakupaswa kukutana na Magufuli. Ingekuwa Halima Mdee Ni dada yake Nassari angeenda Kukutana na aliyemweka Rumande kwa sababu za Kishenzi? Sasa hilo ndio naona lilikuwa Kosa Kubwa na Ujinga wa Nassari.
 
Noted mimi natokea Meru ni muda tu haujafika he has to quit! No compromise na anayemzika mazima ni mkuu wa Wilaya huyu ametokea kuwa karibu sana na wana Meru kuliko hata mbunge na mkuu huyu wa wilaya ana tengeneza njia nyeupe kwa mgombea wa ccm atakayekuja. Nasari haonekani ibadani wala kwingineko. .....anyway mambo yake ni complicated sana. CDM bado tunaipenda SANA
Kosa la Nassary ni lipi? Mbowe ndio awe wa kwanza kuwaomba radhi kwa kuwaletea fisadi Lowasa!

Mzalendo Nassari usichoke ...
 
Someni Kabla Hamjajibu, Mimi Joshua simjui Kiundani wala Sina Chuki naye, Nimetathmini yaliyotokea na Haivumiliki. Kama anajitambua alitakiwa Amponde Magufuli, Huwezi Kukubali Kutumiwa kama, "Condom" Kuwatukana wenzako waliokufikisha ulipo. Na Pia kwa yaliyokuwa yakiendelea Huko Dar es salaam na Kilombero, Joshua Nassari hakupaswa kukutana na Magufuli. Ingekuwa Halima Mdee Ni dada yake Nassari angeenda Kukutana na aliyemweka Rumande kwa sababu za Kishenzi? Sasa hilo ndio naona lilikuwa Kosa Kubwa na Ujinga wa Nassari.
Kama huna uwezo wa kuvumilia uhame nchi lasivyo ukileta fyoko fyoko utatandikwa wewe na kikundi chako.....
 
photo.php
photo.php

Siasa sio uadui wala vita. tunataka maendeleo bila kujali yameletwa na CCM au CHADEMA
 
Kwanza Marandu inabidi uombe radhi kwa kuongezea maneno ya uwongo.Magufuli hakusema ndani ni ccm,alisema ndani mpenda maendeleo. Lakini tuulizane hapa,Nassari alikuwa pekee mtu wa chadema pale kwenye mapokezi? Kwa nini asakamwe yeye tu.
Kulikuwa na Mh Meya wa jiji la Arusha,kulikuwa watu wengi tu wa chadema. Pili Mh Msigwa alimpokea waziri mkuu Mjaliwa lakini hayajasemwa. Tatu Mbunge Mh prof Jay juzi alikuwa na waziri wa mifugo jimboni kwake kutatua mgigoro wa wakulima wa miwa,mbona haulizwi chochote?
 
Magufuli ana wakubali wabunge wote wa ukawa, na haoni sababu ya kuogopa kulisema hilo, akiwa waziri wa ujenzi alisha msifia Mh. Mbowe jimboni kwake mbele ya wananchi wake, lakini Magufuli hajawahi kumsifia mbunge yoyote wa ccm, zaidi ya kuwashurutisha wafanye kazi maana anajua ni mizigo tu. Nasari heshima kwako na kwa wana meru, ile kauli ya kusema moyo uko ccm mH. aliogopa wana ccm watamsaliti asipo tamka lichama lao.
 
Back
Top Bottom