Kama Kuna cha Kumwomba Nassari radhi ni Kimoja Tu, Kwamba Niliongea Kwa Hisia Kali sana. Na sio from nowhere, Ni Kwa Unyanyasaji Unaoendelea. Kwa Hilo naweza Kuomba radhi kwake na Kwa wale waliodhani Nina chuki naye au Ninataka au Nimetumwa kumundermine, Ukweli Ni Kuwa Message yangu Kwake sijabadilisha.
Kuna Mapunguani ambao ati wanadai Mimi sijui siasa, Wala sio Kujisifu kwa Kufuatilia Porojo za Watu hao, Mimi Uwezo wangu wa Siasa Ni Mara 1000 Zaidi yao. samahanini sana I think they should know this!
Nachoweza Kusema Ni Kuwampa Nassari Mwanangu mfano halisi, Kuna Senator mmoja wa Marekani ambaye mwaka 2000 Aligombea Kama Mgombea Mwenza wa Albert Gore kwa Tiketi ya Democrats, Jina lake ni Joe Lieberman, Well Kukawa na Mizengwe, Al Gore akashidwa na GW. Bush, mtoto wa GH Bush, Huyu Lieberman akaendelea Kuwa Senator baada ya hapo, Lakini Tabia Mbaya ya Lieberman ilikuwa siku zote anakaa Upande wa Wapinzani wa chama chake. Mwaka 2004 Wakamtema, Akagombea kama Mgombea Binafsi Akshinda kwa Shida sana. Mwaka 2010 Upepo Ukabadilika na hakutia mguu.
Josia Mwangi Kariuki, alikuwa Katika chama chake, lakini hadithi yake ni tofauti, Unafiki wake yeye alikuwa ni Fisadi wa Kupita Kiasi lakini akawa anaenda kwa wananchi akatumia Uwezo wake wa Kuongea akaweka picha kwa wananchi kuwa Viongozi wengine, hata Rais Jomo Kenyatta mwenyewe walikuwa mafisadi na Wachafu. Walimuua Vibaya na Maiti yake ilikutwa ikionyesha Kuwa Waliomuua walikuwa na Chuki ya ajabu dhidi yake.
Wananchi walimlilia sana, kwani wakati ule waliamini kuwa JM Kariuki ndiye Kiongozi aliyekuwa msafi na tumaini lao. Lakini Miaka kama 40 baadaye wakati wa Kugawana Mirathi na Mashamba yake Ndio Wakenya wanashangaa Jinsi JM alivyokuwa Fisadi.
Mifano Iko Mingi sana, Huo Mfano haufai sana kwani Unaonyesha Mafisadi walichafuana. Lakini Nachotaka Kusema Siasa ina a lot of moving parts, Jitahidi sana Usiharibu uhusiano au Usifanye jambo la kueleweka Vibaya na Waliokupigania (Chama Chako) Na Usiwape tafsiri Kuwa Unafanya mambo ambayo hata kama sio kwa Makusudi yanahalalisha matendo au maneno mabaya Juu yao.
Ningekuwa na Chuki Nisingesema yote haya, Mfitini hasemi wazi, Nina Nia Njema na Demokrasia Tanzania.
KILICHOWEZESHA MISIBA YA MWAFRIKA NI HULKA YA USALITI