Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Joseph Mbilinyi 'Sugu' amlipua Zitto Kabwe

Zito ana kirusi cha ccm,hakuna tiba tena jamaa ndio kawa mwizi oooooop apumzike kwa amani..

Ni kweli ana kirusi cha ccm kinaitwa gunduism kirusi hiki ndicho kinamwandama hata kinana ,
Dalili;
Kupenda sifa
Kuwa ndumila kutatu,
Kujikweza
Lujipendeza
Ujuaji mwingi
Kudandia hoja
Ubinafsi.
 
Sugu anatumika vibaya sana!

Hii ni hatari kwa Mwanasiasa mchanga kama yeye
 
Sugu subiri na wewe ulipuliwe kashfa ya malaria no more umewadhulumu vinega
 
uzuri ni kuwa zitto akijibu wote wataonekana wapuuuzi tu
cheki alivyowahadaa wasanii na wananchi
PENDEKEZO BINAFSI LA MBUNGE KUHUSU KUZUIA UNYONYAJI DHIDI YA WASANII WA TANZANIA KATIKA BIASHARA YA MIITO (RING BACK TONES)

Kwenda kwa: DR ABDALLAH KIGODA, Waziri wa Viwanda na Biashara

Kuhusu
: BIASHARA YA MIITO YA SIMU (RINGBACK TONES)

Kumekuwa na malalamiko makubwa sana kuhusu biashara ya mauzo ya nyimbo kama miito kwenye simu. Malalamiko haya yalianzia kwa wasanii wenyewe na baadaye mimi binafsi niliwasilisha hoja zao Bungeni mwaka 2012. Hata hivyo, hadi sasa malalamiko haya bado hayajapatiwa ufumbuzi na hivyo wasanii kuendelea kunyonywa. Tatizo kubwa katika biashara hii ni USIRI na UNYONYAJI kwa wasanii wa Tanzania. Suala la USIRI lipo Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia. Suala la Unyonyaji lipo Wizara ya Viwanda na Biashara.

USIRI

Biashara hii ya "Ring Back Tones" (RBT) hufanywa na Kampuni za simu (Network providers) kwa kununua maudhui kutoka wachuuzi (Content Providers) ambao nao huingia mikataba na Wasanii (Content Creators).

Hakuna sheria yoyote au Kanuni hapa nchini inayoongoza biashara hii na hivyo "Network providers" na "Content Providers" kuwa watu pekee wenye taarifa zote za biashara hii. Kampuni za simu hujumuisha mapato ya biashara hii na mapato yake mengine (Not Ringfenced), hawatoi taarifa za manunuzi ya nyimbo (au ‘content' nyingine yeyote) kwa wadau na hasa wasanii. Wachuuzi (Content Providers) nao hawatoi taarifa za mauzo kwa wasanii na wanatumia uelewa mdogo wa wasanii kuwasainisha mikataba inayowanyonya. Matokeo yake ni kwamba msanii hupata kiasi cha asilimia mbili tu (2.5%) ya mapato ghafi ya kazi yake. Hivi sasa biashara hii ina thamani (turnover) ya takribani shilingi 44 bilioni kwa mwaka.

Suluhisho:

Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano iandike kanuni (regulations) zitakazolazimisha makampuni ya simu kuweka wazi mapato yatokanayo na biashara ya RBT (Miito ya simu) kila baada ya miezi 4 (disclosure rules). Kanuni hizi zielekeze makampuni kutoa
taarifa za mauzo kwa kila kazi (nyimbo/vichekesho etc.)

UNYONYAJI

Kutokana na usiri ulioelezwa hapo juu, wasanii wamekuwa wakinyonywa kimapato. Kwa mfano Msanii hulipwa mapato yatokanayo na ununuzi wa awali wa kazi yake (wimbo) katika mwezi (downloads).

Lakini mapato yatokanayo na "subscriptions" ambapo mlaji hukatwa shilingi 30 kila siku msanii hapati chochote. Hivyo katika mapato ya sh. 1,300 kila mwezi kwa kila mteja kwa kila wimbo, msanii hupata mgawo wake kutoka shilingi 400 tu za ‘downloads' na ndio maana wasanii wote nchini hupata 2.5% ya shilingi 44 bilioni zinazokusanywa na Kampuni za Simu.

Nchini Marekani biashara ya miito ya simu (RBT) imetafsiriwa kama maonyesho (Public Performances) na hivyo "copyright Association" ya Marekani imeweka kiwango cha chini cha mrahaba (royalty) ambacho msanii hulipwa. Marekani msanii hulipwa asilimia
10 ya patoghafi linalozalishwa na kazi yake kama muito wa simu.

SULUHISHO

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara iandike kanuni kwamba mauzo ya kazi za wasanii kama miito ya simu inachukuliwa kama ‘performance' na kwamba Kampuni za simu zitalipa sio chini ya asilimia 12 (12%) ya mapato ghafi, ambapo asimilia 10%
itakwenda kwa msanii na asilimia 2% COSOTA kwa ajili ya usimamizi na Ulinzi wa kazi za Wasanii.

HITIMISHO

Kanuni za Uwazi (disclosure rules) katika biashara hii ya ‘Ring Back Tones' na mgawo wa haki wa mapato (fair and just revenue share) ndio suluhisho endelevu na litakaloleta tija kwa wasanii wa Tanzania na hata Serikali kukusanya mapato stahili. Kanuni
(Regulations) zinazopendekezwa zianze kutumika kuanzia tarehe 1/7/2013

Kabwe Z. Zitto, Mb
Kigoma Kaskazini
Dodoma, 13 Mei 2013.




Alafu nyuma ya pazia anafanya aya hapa chini,kwa ni ni wasanii wasimpotezee kwa huu unafiki

User ActionsJipatie wimbo wa Leka Dutigite by Kigoma all stars kwa kutuma herufi DE kwenda namba 15050. cc: @ChegeChigunda @linex_tz #PeraAfrica




11:44 PM - 24 Apr 2013








Tweet textReply to @PeraAfrica @ChegeChigunda @linex_tz

https://twitter.com/PeraAfricahttps://twitter.com/ChegeChigundahttps://twitter.com/linex_tz







NB: ANGALIA HOJA YAKE KAITOA LINI NA NYIMBO INATANGAZWA LINI KUUZWA.....IYO KAMPUNI NI YA RUGE
 
Hivi kweli Sugu anaweza kupambana kwa hoja na zitto.
Kwakweli chadema mna jiaibisha sana.

Nssf ina mdai mbowe hadi sasa hajalipa.

Kunatofauti kati ya hoja na FACTS.
hizo ni facts. Sasa kazi ni kwake kusema fedha hizo nimkopo au malipo ya wasanii kwa kazi za NSSF.

Mwizi mwizi tu.....anaweza kuwa mkristo ai mwislam....ccm au ACT Tanzania.
 
Ni kweli wasanii wote wa bongo fleva hawataki kumskikia na hawana amu nae,toka alipowaingiza town Leka Dutigite..mpka imefikia wanamuimba kwenye nyimbo zao asiwafatefate na sasa kiukweli ujumbe ameupata

chek hapa chini..............

nashukuru kwa maelezo yako unamaanisha doko anapigwa kotekote labda ni wakati sahii wa kwenda kufundisha labda na chu watamtosa
 
Siasa za majitaka,hiki ndo kitakuja kuwa kifo cha chadema kuendelea kumfuata fuata zitto
 
Hivi kweli Sugu anaweza kupambana kwa hoja na zitto.
Kwakweli chadema mna jiaibisha sana.

Nssf ina mdai mbowe hadi sasa hajalipa.

Leta ushahidi kwamba anadaiwa na hajalipa na kwamba mkopo wake ulikuwa kinyume na sheria.

Usiropoke hovyo kama uule mama wa jana anaejiita profesa...Tiba aijajulikana.
 
siasa za bongo mi sipingi wala sikubali. maana sina DATA. ila kama ni kweli. bas tuanze utawala kidikiteta demokrasia imetushinda. KIZAZ HIKI AKILI NYINGI MPAKA KEROOOO!
 
Zitto kama mwenyekiti wa PAC hakustahili kufanyabiashara na mashirika anayoyasimamia full stop hakuna kuonewa hakuna longo longo Zitto ni fisadi mjanja.

Mkuu...long time. Upo??!!
 
Tunataka na maelezo ya malipo ya NSSF yalikuwa ya nini? Ya tanapa tumeelezwa yalikuwa ya kupromote sadani, je ya NSSF yalikuwa ya nini?
 
Hawa ni sehemu ya Dola!
Ukitaka ufahamu vizuri angalaia Mama yake Zitto Kabwe anavyohudumiwa na Dola ndani na nje ya nchi!!
Wakati mama Zitto Kabwe akiwa ICU taarifa hizo zimesitua watawala hadi kwenda haraka kwenda kumuona kuliko hata Vicky Kamata ambaye ni danguro lao!
Zitto Kabwe na Mama Zitto Kabwe ni sehemu ya watawala wa sasa hata Mungu akiamua utaona huko Kigoma
Utanikumbuka!!

Toka ulivyo okolewa kwenye tundu la choo basi akili yote iliruka nakukosa kujitambuwa
Kwako ww inaonekana red ni green
 
Suala kufanyike uchunguzi ili kubaini kma kweli kuna uozo huo kwenye taasisi za umma.
Chadema baada ya miaka miwili itakuwa kma chama cha mjomba Mrema
 
Katika wanasiasa niliokuwa nawakubali basi ni Zitto...Ata wakati wanaanza kumuanika nikajua ni siasa chafu wanamuonea......Nilikuja kuchoka nilipokaa na kina Linex wanamuziki members wa Leka Tugite waliponiambia namna alivyokuwa anawatumia wasanii kupiga pesa.....Yani jamaa walikuwa wanaongea kwa uchungu uwezi kuamini ni Zitto uyu uyu ... rip leka tugigite


huyu jamaa hana huruma kabisa, hata siku moja ajawahi simama kutetea destiney ya watu hapo chini bali alikimbilia mahakamani kwa ajili yake myenyewe na kuacha wengine wakiweweseka pasipo kujua wapi pa kukimbilia

  • juliana shonza
  • habibu machange
  • kitila mkumbo
  • mtela mwamba
  • deogratius
  • madiwani wa arusha
hawa wote kawazima ndoto zao

kumbe na kwenye mziki ni upopolization

baada mtakuja kusikia hata dimind was suported by yeye for person interest
 
Jamani kwani kuna ubaya kwa mbunge kuwa na kazi nyingine ya kitaaluma.

Mbona Tundu Lisu wanatetea watu mahakamani. Au mh Mtemvu ana kampuni nayotuletea wafanyakazi wa ndani na madereva huku Uarabuni. Je kuna Ubaya au akifanya Zitto ndio kosa.

Kama wameona ame corrupt popote basi waifikishe kampuni Mahakamani na sio kumchafua Zito bungeni.

Pole sana Sugu kwani Zitto ana ilmu kubwa sana kuliko wewe na wenzako.
yani wewe barubaru ni msomi wa phd kweli unakuja na hoja nyepesi na dhaifu namna hii?

poor Tanzania ndio nchi pekee duniani huwezi kutofautisha akili za wasomi na walioishia elimu za msingi.

mahaba haya yote kisa ni mwislamu anayedhini hadi uzeeni na kuoa hataki?
 
Ni katika Hotuba yake ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ya Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo aliyoiwasilisha Bungeni leo hii muda mfupi uliopita. Waziri Kivuli Joseph Osmundi Mbilinyi aka Sugu amemtaja Zitto Z. Kabwe kama Mmiliki wa Kampuni ya Leka Dutigite aliyofanya biashara isivyo halali na Mashirika ya Umma ya NSSF na TANAPA.

Sehemu husika ya Hotuba hiyo ni hii:

Mheshimiwa Spika, Tarehe 13 Agosti, 2012, Msajili Msaidizi wa Makampuni katika Wakala wa Usajili wa Makampuni na Leseni (BRELA) alitoa Hati ya Usajili (Certificate iof Incorporation) kwa kampuni inayoitwa Leka Dutigite Limited. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, Leka Dutigite Ltd. ina ofisi zake katika ghorofa ya kwanza ya jengo la City House lililoko katika Mtaa wa Mkwepu, Dar es SalaaM. Mheshimiwa Spika,

Katiba, yaani Memorandum and Articles of Association, ya kampuni ya Leka Dutigite Ltd. iliyosajiliwa BRELA tarehe 13 Agosti, 2012 inaonyesha kwamba mwenye hisa nyingi katika kampuni hiyo ni kampuni nyingine inayoitwa Gombe Advisors Ltd. ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za kibenki ambazo Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imezipata, mnamo tarehe 10 Desemba, 2012, Hifadhi ya Taifa ya Saadani ilihamisha jumla ya shilingi 12,200,000 kwenda kwenye akaunti na. 0150357447800 iliyoko CRDB Bank tawi la Pugu Road, Dar es Salaam, inayomilikiwa na Leka Dutigite Ltd. Hifadhi ya Taifa ya Saadani inamilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), ambayo ni shirika la umma. Siku moja baadae, fedha hizo zilitolewa kwa pesa taslimu kutoka kwenye akaunti hiyo.

Baada ya hapo, kati ya tarehe 14 Januari na 7 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa jumla ya shilingi 28,600,000. Fedha hizi zote ziliingizwa kama fedha taslimu na mtu aitwaye Mchange (shilingi 3,600,000 tarehe 14 Januari, 2013) na Leka Dutigite (shilingi 25,000,000 tarehe 23 Januari na 7 Februari, 2013). Kufikia tarehe 7 Februari, 2013, fedha hizo zote zilikwishatolewa benki.

Mheshimiwa Spika,
Tarehe 28 Februari, 2013, akaunti ya Leka Dutigite Ltd. iliingiziwa shilingi 32,367,000 na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kwa mujibu wa taarifa za kibenki, siku hiyo hiyo, fedha hizo zilitolewa kwenye akaunti hiyo. Siku nne baadae, yaani tarehe 4 Machi, 2013, NSSF ilifanya malipo mengine kwenye akaunti ya Leka Dutigite Ltd., kwa mikupuo miwili, ya jumla ya shilingi 46,663,000. Siku hiyo hiyo, fedha hizo nazo zilitolewa kutoka kwenye akaunti hiyo kwa mikupuo miwili. Kwa hiyo, katika kipindi cha miezi mitatu katika ya tarehe 10 Desemba, 2012 na 4 Machi, 2013, Leka Dutigite Ltd. ililipwa shilingi 119,930,000 kwa utaratibu huo huo wa ingiza na toa fasta. Kati ya fedha hizo, shilingi 12,200,000 zililipwa na TANAPA na shilingi 79,027,000 zililipwa na NSSF.

Mheshimiwa Spika,
Katika mazingira ya kawaida, sio kitu cha ajabu kwa mashirika ya umma kama NSSF na TANAPA kufanya biashara na watu au taasisi mbali mbali kama makampuni binafsi. Ukweli ni kwamba, kwa upande wa malipo yaliyofanywa na TANAPA, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu imeweza kupata nakala ya mkataba unaohusu Maandalizi ya Filamu (Documentary) kwa Ajili ya Kuhamasisha Shughuli za Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani kwa Kutumia Wasanii Kutoka Kigoma. Mkataba huo umesainiwa tarehe 5 Desemba, 2012, kati ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani na Leka Dutigite Ltd. na una thamani ya shilingi 12,200,000, kiasi kile kile kilicholipwa na Hifadhi hiyo.

Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, mazingira ya malipo haya sio ya kawaida. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa kampuni ya Gombe Advisors Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka za BRELA, kampuni hii ilisajiliwa tarehe 24 Novemba, 2011. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, ofisi za Gombe Advisors Ltd. ziko kwenye jengo la City House, Mtaa wa Mkwepu, Dar es Salaam, ziliko ofisi za Leka Dutigite Ltd. Kwa mujibu wa nyaraka hizo, wakurugenzi wa Gombe Advisors Ltd. ni Zitto Zuberi Kabwe ambaye kazi yake inatajwa kuwa ‘mchumi’, na Raphael Ongangi ambaye anatajwa kuwa ‘mchambuzi wa fedha na vitega uchumi’ (Financial and Investment Analyst). Bwana Ongangi aliwahi kutajwa na gazeti la kila wiki la ----- la tarehe 26 Desemba 2013 kuwa ni mmoja wa washauri wa Zitto Zuberi Kabwe na anasemekana kuwa msaidizi wake.

Mheshimiwa Spika,
Zitto Zuberi Kabwe sio ‘mchumi’ anayetajwa katika nyaraka za BRELA zinazoihusu kampuni ya Gombe Advisors Ltd. pekee, bali pia ni Mbunge, tangu mwaka 2005, wa Bunge lako tukufu. Kama Mbunge, Mheshimiwa Zitto Kabwe ni ‘kiongozi wa umma’ kwa mujibu Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, 1995. Sheria hii inawalazimu viongozi wa umma, wanapokuwa madarakani, kuwa “waadilifu, wenye huruma, utulivu, umakini na watakaoendeleza viwango vya juu vya maadili ili kujenga na kuendeleza imani ya umma kwa uadilifu wa Serikali.”

Aidha, viongozi wa umma “... watawajibika kutekeleza wajibu wao kwa umma na kuendesha shughuli zao binafsi kwa namna ambayo itaonekana na kuthibitika kuwa ni wazi kwa umma na haitatosheleza kwao kutekeleza wajibu wao kwa kufuata sheria tu.” Vile vile, kuhusiana na maslahi binafsi, Sheria hii inaelekeza kwamba “... viongozi wa umma hawatakuwa na maslahi binafsi ambayo yanaweza kuathiriwa na maamuzi ya serikali wanayoshiriki katika kuyafanya.”

Mwisho, kuhusiana na maslahi ya umma, viongozi wa umma wanatakiwa, pale wanapochaguliwa au kuteuliwa, kupanga masuala yao “kwa namna itakayozuia migongano ya maslahi ya wazi, iliyojificha au inayoonekana kuwepo na pale ambapo migongano hiyo inatokea kati ya maslahi binafsi na maslahi ya umma basi itatatuliwa kwa kuangalia zaidi maslahi ya umma.” Kwa kadri ya ufahamu wa Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu, Mheshimiwa Zitto Kabwe hajawahi kutangaza maslahi aliyonayo kwenye mikataba ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd. na NSSF na TANAPA.

Mheshimiwa Spika,
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe sio tu ni Mbunge anayebanwa na masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, bali pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Fedha za Serikali (PAC). Kwa mujibu wa kipengele cha 12 cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge lako tukufu, mojawapo ya majukumu ya PAC ni kushughulikia maeneo yenye matatizo sugu ya matumizi mabaya ya fedha za umma katika Wizara na Mashirika ya Umma yaliyoainishwa katika taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. NSSF na TANAPA ni baadhi tu ya Mashirika ya Umma yaliyo chini ya usimamizi wa kibunge wa PAC.

Kwa maana hiyo, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Zitto Kabwe, kwa kutumia makampuni yake ya Leka Dutigite Ltd. na Gombe Advisors Ltd., amefanya biashara na TANAPA, shirika la umma analolisimamia kama Mbunge na Mwenyekiti wa PAC. Mheshimiwa Zitto Kabwe na wanamuziki washirika wake, kwa kutumia makampuni ya Gombe Advisors Ltd. na Leka Dutigite Ltd., wamelipwa fedha za umma za TANAPA na NSSF.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa maelezo juu ya madai ya ukiukwaji wa Sheria uliofanywa na viongozi wa umma na mashirika ya umma katika kashfa hii. Pamoja na maelezo yatayotolewa , Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi maalum juu ya matumizi ya fedha zilizotolewa na TANAPA na NSSF; msukumo uliofanya fedha hizo zitolewe na matumizi ya fedha hizo kwa kuzingatia masharti yanayosimamia fedha za umma na utawala bora katika usimamizi wa fedha za umma. Aidha, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ifanye uchunguzi juu ya malipo na matumizi husika kwa kurejea masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Sheria nyingine zinazohusika. Kwa upande mwingine, kwa kuwa suala hili linahusu mbunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayohusika na usimamizi wa fedha za umma, Kamati ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge nayo ifanye uchunguzi wake juu ya madai ya masharti ya Katiba ya Nchi, Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge na Kanuni za Bunge juu ya maadili ya kiongozi wa umma ikiwemo yahusuyo utangazaji wa maslahi.

Mheshimiwa Spika;
Mwisho, Kambi Rasmi ya Upinzani ya Bunge lako tukufu inatoa rai kwa wanamuziki na wasanii wengine wote nchini kuwa waangalifu na watu wanaotaka kutumia umaarufu wao kama wanamuziki na wasanii kwa lengo la kufanikisha dili za kifisadi. Bila kuchukua tahadhari ya kutosha, wasanii hao wanaweza kujikuta wakipoteza sifa na umaarufu wao ambao wameujenga kwa jitihada zao wenyewe.

************************************************************************************************

Mapambano ya Kambi Rasmi ya Upinzani yanaendelea.Hayachagua mtu,taasisi au kundi la watu au taasisi

Naililia Tanzania nazililia fikra huru kish nawasikitiki wanasiasa kwa kuchagua njia zenye miiba
 
Mustafa Mkulo njoo huku umuone zitto yuko uchi, sugu Kamvua taulo Kama alivyokuvua kipindi kile
 
Back
Top Bottom