TANZIA John Mwankenja auawa kwa risasi

Nsesi

JF-Expert Member
Nov 20, 2008
380
53
1713087783059.png

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mh. Mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa leo majira ya Nne na dk 10 nyumbani kwake Kiwira. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa marehemu Mwankenja alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.

Wauaji walitoweka mara baada ya kukamilisha mauaji yao na kabla ya watu kukusanyika. Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijafahamika. Hata hivyo baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu usiku huu wanahofu mauaji hayo kuhusiana na masuala ya kisiasa.

Marehemu John Mwankenja

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kupigwa risasi
- Utata kifo cha hayati Abeid Karume

- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

- Kifo chenye utata cha Waziri Nicas Mahinda

- Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

- TANZIA - Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

- Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

- Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki
 
This is really bad!. I pray chanzo kifahamike mapema to rule out conspiracy theory ya kusingizia chama fulani!. RIP Mwankenja!.
 
Chanzo na maelezo zaidi mkubwa maana sielewi unaposema sababu za kisiasa.je ni wao kwa wao kama arusha au kama tarime?
 
Pole sana wafiwa wote na mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu. Nafikiri ni mapema sana kuhusisha mauaji hayo na masuala ya kisiasa. Tusubiri uchunguzi wa polisi kwanza.

Mbeya haijafika hapo na Rungwe ni katika wilaya zenye utulivu mkubwa kisiasa hata kama mapambano ya hoja yapo kama kawaida mitaani.

Kiwira ni kwa profesa Mwakyusa ila mwenyekiti alikuwa wa majimbo yote mawili yaani la prof. Mwakyusa pamoja na prof. Mwandosya.
 
poleni wafiwa na wanarungwe kwa ujumla. mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina.
 
MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe John Mwankenja ambaye ni diwani wa kata ya Kiwira ameuawawa kwa risasi usiku huu majira ya saa 5.00 wakati akishuka kwenye gari lake kuelekea nyumbani kwake.

Habari zilizoufikia mtandao huu zinaeleza kuwa alimiminiwa risasi kadhaa wakati akishusha mguu wake kutoka kwenye gari ili kuingia nyumbani kwake eneo la Kiwira.

Maiti yake inapelekwa hivi sasa hospitali ya Makandana kwa kuhifadhiwa, na hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambalo kwa ujumla linaaacha maswali mengi kwa wananchi wa wilaya ya Rungwe na mkoa kwa ujumla.

Taarifa zaidi mtaletewa kadiri zitakapopatikana kutoka Rungwe
 
huyu marehemu kiwira coal mine iko kwenye himaya yake,sio?am just saying,pole sana.na investigation zetu uchwara tena,ngoja tusubiri.
 
Du jamani poleni sana na RIP kwake MWANKENJA
da siamini ni Siasa zetu hizi na mtu wa kwao hukohuko Mbeya (Mnyakyusa) sina cha kuongea km ni mapenzi ya MUNGU sasa tunaenda sivyo
 
huyu marehemu kiwira coal mine iko kwenye himaya yake,sio?am just saying,pole sana.na investigation zetu uchwara tena,ngoja tusubiri.

Kiwira Coal Mine iko wilaya ya Kyela wakati huyu ni wilaya ya Rungwe. Ni majina tu, hizo sehemu mbili ziko umbali wa kama km 50.
 
Kwa nini kila jambo lihusishwe na siasa!! Tusubiri uchunguzi kwanza ndipo tuzungumze. Poleni ndugu wote mlioondokewa na mpendwa wenu.
 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya amekufa baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana usiku huko Tukuyu.

Hamna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.

8589601.jpg

Marehemu John Mwankenja
 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mbeya Ndugu John Mwankenja ameuwawa kikatili na watu wasiojulikana jana usiku.
Ndg John Mwankenja aliuwawa nyumbani kwake kwa kupigwa risasi wakati anaegesha gari lake, alikuwa amerejea tu kutoka Mbeya Mjini alikokuwa ameenda kumwona mke wake aliyelazwa hospitali ya Rufaa Mbeya.
Wauwaji hawajachukua kitu.
Ndugu J Mwankenja alikuwa vile vile Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya.
Mungu amuweke pema roho ya marehemu . AMEN
 
Back
Top Bottom