Kunataarifa zisizokuwa Rasimi Naibu Waziri Ujenzi Harrison Mwakyembe Amepigwa risasi yeye pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mbeya!Kadri habari zitakavyokuja tutawajulisha.
Kwa nini kila jambo lihusishwe na siasa!! Tusubiri uchunguzi kwanza ndipo tuzungumze. Poleni ndugu wote mlioondokewa na mpendwa wenu.
Poleni saana wana Rungwe wape pole saana familia ya marehemu. Mungu awape nguvu ya kuhimili machungu ya msiba huo mzito!!!!!!!! Lakini jamani Watanzania tuache mambo ya ubwenyenye, huyu mtu alirundikiwa madaraka mengi tena makubwa, Mkt wa CCM Wilaya, Mkt wa Halimashuri Wilaya, Diwani wa kata,bila shaka mjumbe wakamati sijui ipi na tume kibao. Vyote hivyo ni mzigo mzito kila anapokanyaga. Poleni wandugu wafiwa!!!!!!!!!Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mh. Mwankenja ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa leo majira ya Nne na dk 10 nyumbani kwake Kiwira. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa marehemu Mwankenja alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kuwasili nyumbani kwake.
Wauaji walitoweka mara baada ya kukamilisha mauaji yao na kabla ya watu kukusanyika. Hadi sasa sababu za mauaji hayo hazijafahamika. Hata hivyo baadhi ya viongozi waliofika nyumbani kwa marehemu usiku huu wanahofu mauaji hayo kuhusiana na masuala ya kisiasa.
Poleni wafiwa. Tumeondokewa na nguvu kazi muhimu wakati tukiitegemea. MUngu ampe ppumziko la milele.
Ila kauli chafu kama za Kagasheki zisipewe nafasi kuwa chama fulani kinausika na mauaji.