John Mnyika: Bawacha haijaundwa kwa ajili ya kupeleka wabunge wa viti maalumu bali kuchochea mageuzi ya Demokrasia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,937
141,908
Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika amesema Bawacha haijaundwa kwa ajili ya kuchagua wanawake wa kuwapeleka bungeni kwa viti maalumu bali ni kichocheo cha demokrasia nchini.

Mnyika amesema wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanao wajibu wa kupigania katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.

Pia Bawacha wanapaswa kuwa walinzi wakuu wa rasilimali za nchi na fedha za walipakodi.

Chanzo: ITV habari

====

Mwanza. Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amelitaka Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kwa ustawi wa chama hicho na Taifa.

Mnyika ameeleza hayo leo Jumanne Mei 18, 2021 katika kikao maalum cha kuchagua viongozi wa baraza hilo baada ya waliokuwepo kuvuliwa nyadhifa zao na kufukuzwa uanachama.

Mnyika amesema viongozi watakaochaguliwa wasifikirie kuwa baraza hilo lina kazi ya kuchagua viti maalum vya udiwani na ubunge, wanapaswa kutambua kuwa ni baraza la kutetea wanawake, kupigania tume huru na katiba mpya.

“Nyinyi wanawake wa Chadema kupitia baraza lenu mna nafasi ya pekee kuandika historia kama wamama wa mabadiliko, kama walezi wa haki. Kazi ya kuandika historia hiyo inaanza leo,” amesema.

Huku akiwagusia wanawake 19 waliovuliwa uanachama wa Chadema baada ya kula kiapo cha kuwa wabunge wa viti maalum bila ridhaa ya chama hicho, Mnyika amesema lazima katikati ya usaliti, uhasi na ubinafsi waibuke wanawake wengine wasonge mbele mpaka waifikie Tanzania wanayoitaka.

Amewataka kuweka pembeni ubinafsi na makundi na kuchagua kwa haki viongozi wa baraza hilo huku akiwataka waendeleze mapambano ya kuvunjwa kwa katiba ya nchi kwa wanawake hao 19 kuendelea kuwa wabunge licha ya kufukuzwa Chadema.

Chanzo: Mwananchi
 
Na mapendekezo ya mabaraza ndani ya chadema ,mpendekeza ni mnyika mwenyewe tena akiwa form 6 ,upele umemkuta mkunaji
 
Chama makini kabisa kimebeba na kuwakilisha agenda muhimu ya mabadiliko ya msingi hapa nchini licha ya magumu, ufedhuli, udhalimu na uharamia kilichopitia ktk utawala wa giza wa kidimokrasia toka 2015 - 2020. Hongera Katibu Mkuu John Mnyika Hongera CDM.
Ni jambo jema.

Wewe ni mbenge au mbege?

Samahani lakini!
 
CHADEMA chama changu, nakupenda kwa moyo wangu wote, na Mungu awabariki viongizi wangu wa CHADEMA✌🏽✌🏽✌🏽✌🏽✌🏽
 
Chama makini kabisa kimebeba na kuwakilisha agenda muhimu ya mabadiliko ya msingi hapa nchini licha ya magumu, ufedhuli, udhalimu na uharamia kilichopitia ktk utawala wa giza wa kidimokrasia toka 2015 - 2020. Hongera Katibu Mkuu John Mnyika Hongera CDM.
CDM wanajituma sn
 
Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika amesema Bawacha haijaundwa kwa ajili ya kuchagua wanawake wa kuwapeleka bungeni kwa viti maalumu bali ni kichocheo cha demokrasia nchini.

Mnyika amesema wanawake ni jeshi kubwa hivyo wanao wajibu wa kupigania katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
Pia Bawacha wanapaswa kuwa walinzi wakuu wa rasilimali za nchi na fedha za walipakodi.

Source: ITV habari
Kuweni makini sasa msidanganyike kiwepesi kama 2015, mlipigwa chenga ya mwili mkalamba galasa mwisho wa siku kundi likaenda kuunga mkono juhudi
 
Chama makini kabisa kimebeba na kuwakilisha agenda muhimu ya mabadiliko ya msingi hapa nchini licha ya magumu, ufedhuli, udhalimu na uharamia kilichopitia ktk utawala wa giza wa kidimokrasia toka 2015 - 2020. Hongera Katibu Mkuu John MnyikaTHongera CDM.
Tangu hiki chama kianze kusapoti mashoga na kulilia chanjo,sikipendi kabisa
 
Back
Top Bottom