PostGE2025 John Heche: Tupo tayari kumpokea Halima Mdee CHADEMA

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,122
Reaction score
17,406
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, John Heche amezungumzia kurejea kwa Halima Mdee ndani ya chama hicho wakati wa mahojiano kupitia Wasafi FM;

"Kwanza niseme Halima ni rafiki yangu, na mimi nampenda na anajua. Tumekuwa naye kwenye chama... ni mtu nampenda, anajua na chama chetu kinampenda."

"Halima ni mtu mwerevu, ni mtu ambaye kwa kweli ana mchango mkubwa kwa chama chetu, huwezi kupuuza hilo, huwezi kulikataa."

Kuhusu utaratibu wa kurejea kwenye chama amesema; "Anajua taratibu za chama chetu. Kama alivyofuata Anatropia [Theonest], Anatropia aliandika barua, akafuata 'process' zote, ikaja kwenye kikao..."

"Hivyo hivyo Anthony Komu... alikuwa Mbunge, akafukuzwa na yeye alifuata 'procedure', wote wamerudi ndani ya chama."

"Mirango iko wazi, hiki ni chama cha siasa... Kama anataka kurudi kwenye chama, 'procedure' zipo, 'process' zipo, arudi kwa kupitia utaratibu, atapokelewa kwenye chama."

Kuhusu Wanachama wengine wa CHADEMA walioondoka, Heche amesema; "Na hata wale wengine waliokimbia kule kwenda kwenye kile chama kile kingine... wengi umewasikia wanarudi wenyewe wanasema 'kumbe tulikengeuka'."

Aseme tu covid wote maana mzee ndio alikuwa dalali wao

USSR
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa John Heche amesema wao kama CHADEMA wapo tayari kupokea Halima Mdee

Heche ameyasema hayo kwenye kipindi cha Jana Na Leo kupitia Wasafi Fm Aprili 15, 2026
 
"Kwanza niseme Halima ni rafiki yangu, na mimi nampenda na anajua. Tumekuwa naye kwenye chama... ni mtu nampenda, anajua na chama chetu kinampenda."

"Halima ni mtu mwerevu, ni mtu ambaye kwa kweli ana mchango mkubwa kwa chama chetu, huwezi kupuuza hilo, huwezi kulikataa."

Kuhusu utaratibu wa kurejea kwenye chama amesema; "Anajua taratibu za chama chetu. Kama alivyofuata Anatropia [Theonest], Anatropia aliandika barua, akafuata 'process' zote, ikaja kwenye kikao..."

"Hivyo hivyo Anthony Komu... alikuwa Mbunge, akafukuzwa na yeye alifuata 'procedure', wote wamerudi ndani ya chama."

"Mirango iko wazi, hiki ni chama cha siasa... Kama anataka kurudi kwenye chama, 'procedure' zipo, 'process' zipo, arudi kwa kupitia utaratibu, atapokelewa kwenye chama."

Kuhusu Wanachama wengine wa CHADEMA walioondoka, Heche amesema; "Na hata wale wengine waliokimbia kule kwenda kwenye kile chama kile kingine... wengi umewasikia wanarudi wenyewe wanasema 'kumbe tulikengeuka'."

Mnyika nakuamini sanaa.....naomba siku uje useme ukweli kuhusu covid19 saga mwanzo mwisho tujue tunachezewaje akili
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, John Heche amezungumzia kurejea kwa Halima Mdee ndani ya chama hicho wakati wa mahojiano kupitia Wasafi FM;

"Kwanza niseme Halima ni rafiki yangu, na mimi nampenda na anajua. Tumekuwa naye kwenye chama... ni mtu nampenda, anajua na chama chetu kinampenda."

"Halima ni mtu mwerevu, ni mtu ambaye kwa kweli ana mchango mkubwa kwa chama chetu, huwezi kupuuza hilo, huwezi kulikataa."

Kuhusu utaratibu wa kurejea kwenye chama amesema; "Anajua taratibu za chama chetu. Kama alivyofuata Anatropia [Theonest], Anatropia aliandika barua, akafuata 'process' zote, ikaja kwenye kikao..."

"Hivyo hivyo Anthony Komu... alikuwa Mbunge, akafukuzwa na yeye alifuata 'procedure', wote wamerudi ndani ya chama."

"Mirango iko wazi, hiki ni chama cha siasa... Kama anataka kurudi kwenye chama, 'procedure' zipo, 'process' zipo, arudi kwa kupitia utaratibu, atapokelewa kwenye chama."

Kuhusu Wanachama wengine wa CHADEMA walioondoka, Heche amesema; "Na hata wale wengine waliokimbia kule kwenda kwenye kile chama kile kingine... wengi umewasikia wanarudi wenyewe wanasema 'kumbe tulikengeuka'."

kwani alienda wapi, tangu lini?
 
Mfano, hivi kina Esta ambao kwa sasa ni wabunge wa CCM, siku bunge hili likifikia ukomo wake na kuandaliwa uchaguzi mwingine, hao nao wakiamua kurudi CHADEMA kugombea ubunge watakubaliwa? Hizo zitakuwa ni siasa za ajabu watu kuhamahama vyama, wanakosa misimamo ya kueleweka
 
Iko hivi, kama Lissu ataachiwa kurejea siasani na hali ya kisiasa ikatengemaa nchini mambo yakawa shwari kuna uwezokana makada wa CHADEMA waliokihama chama wakarudi na wanachama wapya wakajiunga nacho na cha ajabu chama hicho kikapata wanachama wapya maarufu kutoka CCM, hili liko wazi kutokana na nyakati za mivumo ya siasa kuelekea uchaguzi mkuu unaokuja kama hali ya kisiasa itaachwa ifuate mkondo wake
 
Ni jambo jema, lakini chama kiwe makini sana.

Mimi nitawashangaa sana chadema nikija kusikia ester matiko au bulaya nao wamekubaliwa kujiunga kwakuwa tu wamefuata taratibu zote.

CCM ipo mwisho wa uhai wake, chadema itawavuta wengi sana wema na wabaya si kwakuwa wanaipenda chadema, bali kufuata fursa. Msipokuwa makini mtajikuta katika mgogoro mkubwa sana siku zijazo.

Nashauri kwa kila atakayetaka kuja, tumieni ile kanuni ya Dr Slaa kuangalia kama mtu huyo kwenu ni asset au liability.

Kwa upande wa Mdee hata mimi nitafurahi sana nikisikia karejea. Mchango wake kwa chadema hauwezi kutiliwa shaka.
 
Naunga mkono hoja. Pamoja na usaliti alioshiriki 2020, bado anahitaji kupewa nafasi nyingine. Anaonekana ni mpinzani wa kweli.
 
Kina Wenje na Kiwia nao wakitaka kurudi sijui itakuje kwa jinsi walivyokisema vibaya chama chao na kuhamia kule
 
Kwa vile CHADEMA kwa sasa imeondolewa vizuizi vya kufanya siasa zake, huu ni wakati wa kufua na kupata wanachama wapya, isitegemee sana makanda wake waliokihama kurudi. Ifufue na kuanzisha matawi mapya mpaka vijijini isisubiri mpaka uchaguzi mkuu ndio iinuke kufanya siasa. Kwenye siasa za ushindani CHADEMA iko hai na inaungwa mkono na wananchi wengi, kura inazo za kutosha kushinda uchaguzi
 
Mkuu Hilo la kuvuna wanachama wapya lingewezekana vizuri kama mzani wa siasa ungekua uko sawa tofauti na sasa ambapo wanachama wanakamatwa ovyo na kubambikiwa kesi za uhaini,uchochezi na kutekwa,hivyo vyote vina changia kuwatisha vijana kujihusisha na chadema na vyama pinzani kwa ujumla.Hivyo ni wajinu wa vyama kudai mzani sawa wa kufanya siasa.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, John Heche amezungumzia kurejea kwa Halima Mdee ndani ya chama hicho wakati wa mahojiano kupitia Wasafi FM;

"Kwanza niseme Halima ni rafiki yangu, na mimi nampenda na anajua. Tumekuwa naye kwenye chama... ni mtu nampenda, anajua na chama chetu kinampenda."

"Halima ni mtu mwerevu, ni mtu ambaye kwa kweli ana mchango mkubwa kwa chama chetu, huwezi kupuuza hilo, huwezi kulikataa."

Kuhusu utaratibu wa kurejea kwenye chama amesema; "Anajua taratibu za chama chetu. Kama alivyofuata Anatropia [Theonest], Anatropia aliandika barua, akafuata 'process' zote, ikaja kwenye kikao..."

"Hivyo hivyo Anthony Komu... alikuwa Mbunge, akafukuzwa na yeye alifuata 'procedure', wote wamerudi ndani ya chama."

"Mirango iko wazi, hiki ni chama cha siasa... Kama anataka kurudi kwenye chama, 'procedure' zipo, 'process' zipo, arudi kwa kupitia utaratibu, atapokelewa kwenye chama."

Kuhusu Wanachama wengine wa CHADEMA walioondoka, Heche amesema; "Na hata wale wengine waliokimbia kule kwenda kwenye kile chama kile kingine... wengi umewasikia wanarudi wenyewe wanasema 'kumbe tulikengeuka'."

Ni jambo jema. Muhimu ni kuwapokea kwa heshima kama anavyosema yuko tayari kufanya kwa Halima. Aheshimu tu haki ya wanachama kutofautiana kimawazo ama sivyo hawatakuwa tofauti na CCM.

Amandla...
 
Back
Top Bottom