John Heche: CHADEMA haiko tayari kwa Maridhiano

John Heche: CHADEMA haiko tayari kwa Maridhiano

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka na kusisitiza kuwa kamwe CHADEMA haitowasiliti Watanzania.

Akiongea leo January 03,2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche amesema “CHADEMA, Chama chenu hakitakuwa tayari kwa maridhiano yenye kupumbaza, kuhadaa, yenye ulaghai na yenye kuliondoa Taifa kwenye ukweli, haki na kile ambacho Taifa inataka, kamwe hatuwasaliti Watanzania”

“Ni ubatili na dharau kubwa kwa Watanzania kuyaita maridhiano sasa katika mazingira ambapo Serikali iliamua kwa makusudi kuwapuuza Wananchi, Vyama vya siasa na Wadau wa demokrasia juu ya hitaji la nchi kuhusu mabadiliko (reforms) ya mifumo ya uchaguzi nchini, uchaguzi batili hauishii kwenye siasa pekee, huingia moja kwa moja kwenye tumbo la mwananchi na heshima ya maisha yake ya kila siku”

“Leo ninapotoa salamu hizi ni siku ya 269, tangu Mwenyekiti wetu, Tundu Lissu alipokamatwa na kuwekwa mahabusu kwa kesi ya uongo, batili na yenye uonevu wa makusudi wakidhani atapiga magoti kusujudia sanamu”.
Ujumbe muhimu kwa taifa letu
 
Marekani wana waangalia tu wawe makini sana tena sanaa.....
 
Nilishashauri hakuna haja ya maridhiano na hawa wahuni. Serikali isonge mbele kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa sababu miaka 5 ni michache mno. Tusipoteze kuridhiana na wahuni aina ya Heche.
Washauri wakaridhiane na wamiliki wa shell za. oil com maana hizo ndizo zilizowauma zaidi.
 
Knachonishangaza ni matakataka maccm humu chadema wakionyesha kukataa kila namna ya kufunika kombe ili ccm wamalize upumbavu walioufanya mo29 majibwa ya maccm humu yanawaona chadema kama waasi wasiopenda amani hki ni kchekesho cha karne. Serikali n kama haipo, ccm imekufa rasmi haipo kbs..na chadema wanasubiri reforms tu mpira uwekwe kati tuone.
 
Hamna maridhiano na Manyumbu Kwanza na ruzuku 0.
mchangishe hadi sumuni.
Si tunakula ubwabwa na Rungwe huku..
 
Sasa mkikataa maridhiano Lissu ataendelea kukaa mahabusu muda usiojulikana, mpaka aje atoke kama ni wa kutoka si leo
Haki ina gharama zake Mandela alikataa kuridhiana na makaburu akakaa gerezani kwa miaka 27.
 
Back
Top Bottom