FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 93,165
- 109,703
Mkuu.
Naamini hapo kwenye "UWA" umemaanisha "Huwa" kwa hili tu unapaswa kujitafakari maana umeshindwa kuandika kiswahili fasaha. Ni madhara ya kuharibiwa kwa mfumo wa elimu na chama unacho shabikia.
Mapokezi ya Chifu au Mfalme au kiongozi yoyote aliyepewa heshima na jamii aliyoikuta hutegemeana na utamaduni wa eneo husika. Itilima wanamfunga furushi la khanga kiongozi kama ishara ya kumthamini, kama wanavyofanya kwa machiefu wao, kama walivyo mpokea Heche kama mfalme.
Kama "mfalme" sishangazwi na neno hilo haswa baada ya Ufipa kuchakachuwa katiba iliyoachwa na kina Bob Makani.
Ufalme nje-nje. Imefikia mpaka kurithishana baba mkwe na mkwe. Tumesoma humu pia kuwa Mfalme mstaafu Mtei hamtaki tena Slaa, hayuko kwenye ukoo. Vipi wewe? bado unahitajika au unajipendekeza-pendekeza tu?
Kama hivi kumpamba mtu eti "kama mfalme". Khaa, mwanamme mzima kupamba wanaume wenzio kwa maslahi hata haya huoni?