ubongokid
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 2,030
- 3,908
Ndugu zangu;
Kila nchi inakopa,na kila mkopo lazima utumike kikamilifu.Hata hivyo hii mikopo ambayo tunaaminishwa kwamba imetumika vizuri ni changa la macho.
IKO hivi.Idadi ya watu Tanzania ni Chini ya Milioni 60.Idadi ya shule ni chini ya elfu 20.Trilioni moja ni sawa na Bilioni 1000.Kamata Trilioni 1.3 ya covid imepelekwa kujenga madarasa,na TOZO ya uzalendo nayo imeenda kujenga madarasa basi inamaana yamejengwa madarasa ya thamani ya milioni 100 kwa kila moja ambayo ni sawa na madarasa 10,000.Kama kila darasa linakaa wanafunzi 40 inamaana wanafunzi laki nne na zaidi wamejengewa madarasa mapya.
Katika hali ya kawaida unaweza fikiri kwamba JOB NDUGAI aliteleza ulimi aliposema kwamba TULIPITISHA TOZO ili TUPUNGUZE KUKOPA lakini MBONA bado TUNAKOPA?Ni swali la msingi sana.Kama serikali imeweka TOZO zenye majina tofauti na kila siku wanabuni majina mapya ya TOZO na kodi .JE inaleta PICHA gani iwapo tunaendelea kupewa mikopo yenye majina TOFAUTI?
Je, serikali inafuja PESA zetu? TRA wanasema wamekusanya trilioni 11 kwenye miezi kama 6 iliyopita na wakati huo huo tumechukua mikopo ambayo ni sawa na kiasi hicho cha makusanyo ingawa miradi iliyofanywa bado haijafikia kiwango hicho cha cha makusanyo.JE nani muongo?
Binafsi naamini kabisa NDUGAI alisema ukweli wake na alichagua kuondoka kishujaa pamoja na kwamba alikuwa sehemu ya ufedhuli na unyonyaji.Huyu Ndugai alikaa India kwa Muda mrefu akitumia pesa za walipakodi kula RAHA ukiona mpaka amefikia hatua ya kufunguka UJUE kuna JAMBO
ANYHOW.Nfasi ya kazi ipo WAZI niwakumbushe tu wale vijana ambao wanao mpango wa kuwa SUPIKA kwamba nafasi iko wazi na mtu yeyote anaweza kugombea mradi tu kuwe na chama cha siasa kinachokudhamini..So muanze kazi mapema.