JKT wakanusha kutokea vifo katika mafunzo

JKT wakanusha kutokea vifo katika mafunzo

Yaani nchi hii,we dont have vision,we dont have mission,we dont have priorities,all things goes for its own...that if things hits the wall then ndo unakuwa kifo chake...Pesa zimetumika nyingi lakini utashangaa miaka miwili mitatu wanakuja kusema imesitishwa kutokana na kasoro zilizojitokeza...Hivi wanaanzisha vitu bila kujua nini kitatokea???Sina imani kabisa kama hii program itaishi zaidi ya miaka 10.

We are counting down for it and we are approaching a Big 0!!!!
 
umeona jf ni zaidi ya bbc ila
mwizi hata akikamatwa anaiba hakubali ng'odo

Hawa jamaa walivyo majuha walianza kwa kukana eti hakuna kifo lakini baada ya kukomaliwa na wananchi kwa data halisi eti wamekurupuka tena na kudai eti ooo alikua na malaria mara sijui vitu gani khaa! Kwa nini walikana? Tz hakuna jeshi iwe polisi, jkt, jw wote wamejielekeza kuua raia wasio na hatia kwa mitindo tofauti tofauti kama Iringa-polisi wakamuua Mwangosi, Mtwara-polisi na jw wakaua raia, wakambaka mama mjamzito kisha kumpiga risasi, Arusha-jkt wameua mwanafunzi, nk nk. Walaaniwe maaskari wote waliowahi kushiriki mauaji ya raia wasio na hatia.
 
mmhh wanajikosha tu hao jkt...jana nilikuwa na chart na mtu yupo jkt arusha oljoro anasema ni kweli kuna kifo kimetokea ila sababu za kifo zinafichwafichwa..hofu imetanda sana huko kwenye haya makambi ya jeshi..hao watoto huko wameenda kupata mateso tu hasa kwa watoto wa kike sio pazuri yani wapo hatarini kurudi na magonjwa ya zinaa....walioamua kulifuta waliona mbali sasa sijui kwa nin limerudishwa.....wazazi ingieni barabarani kupinga watoto wenu kupelekwa jeshini..hapafai kwa karne hii ambayo mtu anafanya uhalifu anaangaliwa tu au anaambiwa ni suala binafsi...jkt my left foot

Kuna wazazi wengine wanapenda watoto wao waende huko ili kuwakomoa.
Kuna wanafunzi wanalazimishwa enda
Kuna wanaotishiwa kwenda
Wanaopenda kwenda ni wachache sana na ukiangalia lazima wanapenda kuja kuwa wanajeshi siku moja
 
Huu ni moja ya uongo na kuwaweka watu roho juu. Na kama kuna mwanafunzi mgonjwa yupo kambi yyt tofauti na ruvu basi ni uzembe na upuuzi. Mtandao wa JKT umewaelekeza wanafunzi wote wagonjwa kwenda Ruvu JKT, ww unatudanganya. Tupe jina la mtoto wako hapa. Nimemtafuta mkuu wa Oljoro, anaitwa Myalla na hakuna kitu km hicho.

kwa hiyo msemaji wa jeshi ni muongo? kwa sababu amekiri kutokea kwa kifo kambini jkt oljoro
 
Walifute kule ni.kueneza zinaa na mateso toka lini uzalendo ukajengwa kwa mateso juu ya watu badala wainvest kwenye technology wao wanafikiria nguvu Tanzania ya zidumu fikra za mwenyekiti ni tofauti maafande wenyewe

Wakitoka huko watakuwa wakatiri sana na uwezo wa kushika bunduki hivyo tuangalie twaweza kuwa twatengeneza vijana watakao kuwa wanateka watu kwani najua hawatapata kazi wakimaliza vyuo.
Je wale ambao hawatapita kuendelea na chuo wao unadhani watafanya kazi gani?
 
Lkn yule afande alikiri kutokea kwa kifo hicho na kueleza sababu ni upungufu wa damu uliotokana na kuugua malaria kwa muda mrefu...sasa rasta nakuona unabisha tu yaani we unabisha tu...

huyo jamaa anatetea uovu wa jkt kwa nguvu zote
 
Operations za kijeshi zina kila aina ya mazaga zaga.
 
Nimefuatilia kwenye tovuti ya JKT na nimepitia jina moja baada ya jingine kwa wanafunzi walioteuliwa kwenda JKT OLJORO awamu ya kwanza sijaona jina la HONORATUS UISO hivyo labda anajina lingine,

Hivyo basi mtoa mada tuambie hilo jina. Au hizo taarifa umezitoa wapi? Ili uwe mzalendo na nchi yako mafunzo wanayoyapata kule yanajitosheleza,nimategemeo yangu serikali itajipanga kuongeza muda wa mafunzo mpaka miezi tisa ili tuwe na vijana wazalendo na wakakamavu na pia nimategemeo yangu serikali ipitishe sheria vijana ambao hawajapitia JKT waende kwa nguvu wakajifunze uzalendo na sio kupiga kelele.

hao waloenda jkt miaka hiyo weng c ndio viongoz wa leo.WaNaoingza nnch katika mikataba mibovu awakufundishwa uzalendo miaka hiyo?
Mkuu uzalendo unatoka ndan ya mtu
 
Nimeangalia kwny pdf ya jkt 19 May 2014 awamu ya kwanza sijaona jina la honoratus uiso. Majina yote yapo kwny www.jkt.go.tz na hakuna jina hilo. Tujaribu kupost vitu halisi maana wengine tuna watoto huko.

Nimefuatilia kwenye tovuti ya JKT na nimepitia jina moja baada ya jingine kwa wanafunzi walioteuliwa kwenda JKT OLJORO awamu ya kwanza sijaona jina la HONORATUS UISO hivyo labda anajina lingine,

Ndugu wewe mama watetea huo ujinga basi ni wewe ila elewa watu wana akili zao humu. Mimi kuna binti yuko pale na jina lake laanza na Ho sasa ukisema kuwa hakuna mwenye hilo Jina napata mashaka na uelewa wako
Hivyo basi mtoa mada tuambie hilo jina. Au hizo taarifa umezitoa wapi? Ili uwe mzalendo na nchi yako mafunzo wanayoyapata kule yanajitosheleza,nimategemeo yangu serikali itajipanga kuongeza muda wa mafunzo mpaka miezi tisa ili tuwe na vijana wazalendo na wakakamavu na pia nimategemeo yangu serikali ipitishe sheria vijana ambao hawajapitia JKT waende kwa nguvu wakajifunze uzalendo na sio kupiga kelele.

Tumekusikia
 
Nyie acheni tu,
Binti yangu yuko huko, toka aende nikama na mimi nimekuwa kumfuzd.
Akili haipo kabisa;

God be with all of them.
 
kwa hiyo msemaji wa jeshi ni muongo? kwa sababu amekiri kutokea kwa kifo kambini jkt oljoro

Ujue haka kanchi kila taasisi haina mpangilio, yaani kwa mfano hai angalia msemaji wa jeshi kakubali kifo kimetokea japo kapoza habari kwa kutaja malaria ndo sababu, wakati huohuo vijiaskari vilivyoko humu jf vimekazana kusema eti hakuna kifo, sasa sijui hii ina maanisha nini? Heshima ya majeshi imepotea sana siku hizi.
 
Acha kunizushia mkuu, mimi ni mkufunzi wa mtaani kwetu, ila wanaotoa story zisizo na miguu ndo tatizo. Nimeshaupata ukweli. Tatizo la hii jamii inawaona wanajeshi km nchi nyingine, afu wakisikia nafasi ndo hao hao wanapita huku n huku wakitoa hongo ili watoto wao wapate ajira.

Mkuu suala la mwanafunzi kufa hilo ni kweli ila sababu ya kifo chake sidhani kama ni mateso... inawezekana alikuwa na na personal problem na ukizingatia kifo kipo kwa kila mmoja wetu bila kujali sababu na umri wa mtu...
 
Ujue haka kanchi kila taasisi haina mpangilio, yaani kwa mfano hai angalia msemaji wa jeshi kakubali kifo kimetokea japo kapoza habari kwa kutaja malaria ndo sababu, wakati huohuo vijiaskari vilivyoko humu jf vimekazana kusema eti hakuna kifo, sasa sijui hii ina maanisha nini? Heshima ya majeshi imepotea sana siku hizi.

halafu hawa ndio wakufunzi wa jkt, sio ajabu mateso na vifo kuwepo
 
Pota, hakuna mtu yeyote aliyekufa JKT. Ninuzushi na sijui nini nia ya baadhi ya watu. Tumeingiliwa na magubegube wasio wa tz. Kuna wajanja wanataka tuvurugikiwe na amani hapa nchini. Ipo siku tutawasaka mchana kweupe.

Yaani wewe mkuu unatumia nguvu nyingi kukanusha wakati kule kwenye website ya Jeshi la Kujenga Taifa wamekubali kuwa kuna mwanafunzi amefariki katika kambi ya Oljoro.
 
Yaani we acha tu, ni huzuni, majanga, mateso, mauaji, ubakaji na kila aina ya matakataka.

mbaya zaidi hao wanaofanyiwa hivi ni watoto na wamelazimishwa kwenda huko
 
halafu hawa ndio wakufunzi wa jkt, sio ajabu mateso na vifo kuwepo

Mi nafikiri wakufunzi waanzie ngazi za staff sergent na kuendelea siyo hivi vi lance corporal, vi corporal na vi sergent ni shida sana na ujuvi kibao bila kujali utu.
 
Ujue haka kanchi kila taasisi haina mpangilio, yaani kwa mfano hai angalia msemaji wa jeshi kakubali kifo kimetokea japo kapoza habari kwa kutaja malaria ndo sababu, wakati huohuo vijiaskari vilivyoko humu jf vimekazana kusema eti hakuna kifo, sasa sijui hii ina maanisha nini? Heshima ya majeshi imepotea sana siku hizi.

Mkuu hebu nisaidie kushangaa..Wenyewe wamekubali halafu kuna watu humu wanatumia nguvu nyiiingi kukanusha
 
Mi nafikiri wakufunzi waanzie ngazi za staff sergent na kuendelea siyo hivi vi lance corporal, vi corporal na vi sergent ni shida sana na ujuvi kibao bila kujali utu.

hivyo vi corporal na vi sergent ndio vibakaji na vitesaji vya jkt
 
Back
Top Bottom