JKT wakanusha kutokea vifo katika mafunzo

JKT wakanusha kutokea vifo katika mafunzo

godmasai

Senior Member
Joined
Apr 9, 2013
Posts
102
Reaction score
47
JKT wamekanusha vikali kuwepo na vifo kwenye mafunzo ya muda mfupi ya vijana waliomaliza kidato cha sita, habari hizo zilitolewa ktk mtandao huu wa jf na mmoja wa watumiaji. hivyo siri ya jeshi je ilivuja?

====================

Elick-Komba-July4-2014.jpg

Wasemaji wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ), Luteni
Kanali Elick Komba (kushoto) na Meja Emmanuelo Murugi,
wakizungumza na waandishi wa habarijijini Dar es Salaam
jana kutoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya vifo vya baadhi ya

Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekanusha taarifa zinazosambazwa kupitia simu na mitandao ya kijamii kuwa vijana watatu wamefariki baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili katika mafunzo yanayoendelea kwenye kambi ya JKT Oljoro, Arusha.

Msemaji wa JKT, Luteni Kanali Erick Komba, alikanusha taarifa zinazoenezwa juu ya kuhusika kwa jeshi hilo na vifo hivyo kikiwamo kifo cha mwanamke aliyefariki katika kambi hiyo.

Kanali Komba alisema kumezuka taarifa zenye nia ya kulichafua JKT na kupotosha jamii baada ya kifo cha Honorata aliyefariki kwa upungufu wa damu (anaemia).

"Taarifa zilizosambazwa ni uzushi, hakuna vifo vya vijana watatu vilivyotokana na ukatili katika kambi ya JKT Oljoro. Ukweli ni kwamba amefariki kijana mmoja anayeitwa Honorata Oiso," Kanali Komba aliwaambia waandishi wa habari jana.

"Kuna mtu anayetumia kifo hiki kusambaza ujumbe wa uongo kwa jamii. Wazazi wake wamethibitisha ukweli juu ya kifo cha mtoto wao," aliongeza.

Source: Nipashe
 
mmhh wanajikosha tu hao jkt...jana nilikuwa na chart na mtu yupo jkt arusha oljoro anasema ni kweli kuna kifo kimetokea ila sababu za kifo zinafichwafichwa..hofu imetanda sana huko kwenye haya makambi ya jeshi..hao watoto huko wameenda kupata mateso tu hasa kwa watoto wa kike sio pazuri yani wapo hatarini kurudi na magonjwa ya zinaa....walioamua kulifuta waliona mbali sasa sijui kwa nin limerudishwa.....wazazi ingieni barabarani kupinga watoto wenu kupelekwa jeshini..hapafai kwa karne hii ambayo mtu anafanya uhalifu anaangaliwa tu au anaambiwa ni suala binafsi...jkt my left foot
 
Nisingetarajia waseme kuna vifo vmetokea kila mtu alitarajia wakane.
Ni kweli huko JKT hapafai kila mtu anajua hilo ni hatari sana huko. Dawa ni kuifuta tu
 
Nisingetarajia waseme kuna vifo vmetokea kila mtu alitarajia wakane. Ni kweli huko JKT hapafai kila mtu anajua hilo ni hatari sana huko. Dawa ni kuifuta tu
Yaani nchi hii,we dont have vision,we dont have mission,we dont have priorities,all things goes for its own...that if things hits the wall then ndo unakuwa kifo chake...Pesa zimetumika nyingi lakini utashangaa miaka miwili mitatu wanakuja kusema imesitishwa kutokana na kasoro zilizojitokeza...Hivi wanaanzisha vitu bila kujua nini kitatokea???Sina imani kabisa kama hii program itaishi zaidi ya miaka 10.
 
Kumbe jf imekamata mpaka watu wa jeshi wanasoma humu na kwenda kukanusha kwenye media zingine? Pole zao ila uuaji wa raia si uungwana.
 
Walifute kule ni.kueneza zinaa na mateso toka lini uzalendo ukajengwa kwa mateso juu ya watu badala wainvest kwenye technology wao wanafikiria nguvu Tanzania ya zidumu fikra za mwenyekiti ni tofauti maafande wenyewe
 
Mwaka jana taarifa hizi ziliripotiwa hapa,naona na mwaka huu zimekuja tena
 
Hebu tupeni jina la marehemu, shule aliyotoka na eneo alilotoka jamani maana hadi sasa hatujui ni nani. Wote wanasema kuna kifo lakini cha nani haisemwi na JKT wamekana.
 
Hebu tupeni jina la marehemu, shule aliyotoka na eneo alilotoka jamani maana hadi sasa hatujui ni nani. Wote wanasema kuna kifo lakini cha nani haisemwi na JKT wamekana.

ni binti anaitwa honoratus uiso, anatokea moshi
 
kosa nililofanya sikumuuliza kuwa aliyekufa ni mwanafunzi aliemaliza shule ipi na alkuwa akitokea wapi kimakazi ila ntajaribu kupaste mazungumzo yalivokuwa..ninarusha alizonitumia tu ili kuokoa muda na nafasi nisiwachoshe wanajamvi kusoma maelezo marefu .. nimemuliza mbona kawa kimya???:
majibu..Uku kwema. . .me sna phone. . .na2mia 2 simu za watu wengne

nikamuuliza hali ya huko....
majibu: Uku hamna zaid tu ya watu kuumwa sana. .juz kati 2memzka mdada na watu kama wawl wamechanganykiwa.
.
nikamuuliza viongozi wanalionaje hilo au wanajibu nin
majibu...Viongz wanasema uku kufa kawaida na m2 akfa cku yake imefka

nikamuuliza yey binafsi anaish vip mana ana tatizo la kuishiwa damu
majibu...namshkr mungu kwa hlo hawanipi kazi nzito. . .haya kwaher nlikuwa nakusalim nardsha sim kwa mwenywe
mwisho wa maongezi

maongezi haya si ya kutunga ni ya ndugu yangu yupo oljoro arusha na hizi text tumechat jana
 
halafu kesho watakuja kukanusha
 
imeshasemwa anaitwa honoratus .....na ni kweli wenye majina ya herufi H wengi wao wamepelekwa huko arusha oljoro kwa kuwa hata huyu ndugu yangu aliyeko huko kambini jina lake linaanza na herufi H(naomba nisilitaje nisije kumsababishia matatizo huko kambini)
hapo nafkiri unaweza kuunganisha picha na kujua taarifa hii ina ukweli kiasi gani
kimsingi jeshi linadanganya wananchi yapasa liombe radhi watz....huko jkt ruvu watoto wanawekwa uwanjani usiku hadi saa nane za usiku tena wasichana kwa wavulana wakiwa wamechanganywa...naskia ni ufuska tu ndo unaofanyika hapo.....wazaz msiposimama kidete kuikemea serikali ilitazame upya hili suala tarajieni watoto warudi na magonjwa ya zinaa,ulemavu au maiti
 
Usimsahau kwenye sala zako, JKT ni balaa kuna mateso, manyanyaso ya hali ya juu ambayo yanaweza kabisa kusababisha mtu arudishe namba. Halafu badala ya kutafakari namna ya kuboresha hali hii ya kutisha kama inawezekana wanakanusha tu!!!! Hii kitu ni ya kuifuta tu.

mdogo wangu yuko huko
maneno ya joy yameniogopesha
 
Nimeangalia kwny pdf ya jkt 19 May 2014 awamu ya kwanza sijaona jina la honoratus uiso. Majina yote yapo kwny www.jkt.go.tz na hakuna jina hilo. Tujaribu kupost vitu halisi maana wengine tuna watoto huko.
 
ni binti anaitwa honoratus uiso, anatokea moshi
Nimefuatilia kwenye tovuti ya JKT na nimepitia jina moja baada ya jingine kwa wanafunzi walioteuliwa kwenda JKT OLJORO awamu ya kwanza sijaona jina la HONORATUS UISO hivyo labda anajina lingine,

Hivyo basi mtoa mada tuambie hilo jina. Au hizo taarifa umezitoa wapi? Ili uwe mzalendo na nchi yako mafunzo wanayoyapata kule yanajitosheleza,nimategemeo yangu serikali itajipanga kuongeza muda wa mafunzo mpaka miezi tisa ili tuwe na vijana wazalendo na wakakamavu na pia nimategemeo yangu serikali ipitishe sheria vijana ambao hawajapitia JKT waende kwa nguvu wakajifunze uzalendo na sio kupiga kelele.
 
Nimeangalia kwny pdf ya jkt 19 May 2014 awamu ya kwanza sijaona jina la honoratus uiso. Majina yote yapo kwny Jeshi la Kujenga Taifa na hakuna jina hilo. Tujaribu kupost vitu halisi maana wengine tuna watoto huko.
honoratus jina la kiume...angalia kama kuna honorata ndo pacha wa jina hilo, hayo ni majina ya kilatini kama romanus,romana,,,beatus,beata etc
 
Usimsahau kwenye sala zako, JKT ni balaa kuna mateso, manyanyaso ya hali ya juu ambayo yanaweza kabisa kusababisha mtu arudishe namba. Halafu badala ya kutafakari namna ya kuboresha hali hii ya kutisha kama inawezekana wanakanusha tu!!!! Hii kitu ni ya kuifuta tu.

namuombea Sana Mungu amuepushie na hayo majanga....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom