spade4spade
JF-Expert Member
- Jun 5, 2014
- 2,207
- 2,158
Matusi, kejeli na dhararu hadi mnataka kupasua screen zenu za android na kompyuta, mmefura kwa hasira utafikiri mnaonana wkt serikali na watendaji wake wanaendelea kutenda bila hata kujua mnachopigania kwny jf. Tuulizane, tujenge hoja na tuelimishane kwa kuwa wote hatuwezi kuwa wanasheria, waandishi, wanajeshi au hata wasukuma mikokoteni. Tukielimishana tunaweza kujenga uzalendo na u tz. Jf ingetumika vizuri tungesaidiana kufanya biashara, kupata kazi, kuwaumbua maadui wa nje na ndani ya nchi, na kuelimishana mambo yaliyoko nje ya mazingira yetu lkn yapo kwa wenzetu. Mambo yote ya JKT, IPTL, Maji, madini, n.k. yanaweza kutatuliwa kwa sheria za nchi zinazotungwa bungeni. Kumlaumu mtu anayetekeleza hatuwezi kupata suluhisho zaidi ya mlolongo wa matusi tunayoyashuhudia. Tuchangie na tuelimishane km wa tz bila ya kutapishana matusi na dharau. Ni ushauri tu.