Kitia
JF-Expert Member
- Dec 2, 2006
- 418
- 73
Wana JF.
Leo tumepata habari kuwa JK atakutana na baadhi ya Watanzania waishio Finland tarehe 12 Februari 2008. Katika mkutano huo ataongea na kupokea maswali. Mimi binafsi naona kuwa kuna haja ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kufanyiwa marekebisho kutokana na hali ya sasa ya vyama vingi. Vilevile marekebisho hayo yalenge kuondoa loopholes ambazo zinapelekea kushamiri kwa ufisadi na kukomaza 'granddady' politics. Upeo wangu wa siasa za Tanzania sio mkubwa sana, kwa hiyo naomba kwenu Wakuu, mawazo zaidi kuhusu mada hii, na vipengele vipi vilivyopo katika katiba inayotumika sasa vinatakiwa kufanyiwa marekebisho.
Natanguliza shukrani.