JK ziarani Finland.

Kitia

JF-Expert Member
Dec 2, 2006
418
74

Wana JF.

Leo tumepata habari kuwa JK atakutana na baadhi ya Watanzania waishio Finland tarehe 12 Februari 2008. Katika mkutano huo ataongea na kupokea maswali. Mimi binafsi naona kuwa kuna haja ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano kufanyiwa marekebisho kutokana na hali ya sasa ya vyama vingi. Vilevile marekebisho hayo yalenge kuondoa loopholes ambazo zinapelekea kushamiri kwa ufisadi na kukomaza 'granddady' politics. Upeo wangu wa siasa za Tanzania sio mkubwa sana, kwa hiyo naomba kwenu Wakuu, mawazo zaidi kuhusu mada hii, na vipengele vipi vilivyopo katika katiba inayotumika sasa vinatakiwa kufanyiwa marekebisho.
Natanguliza shukrani.
 
Yeah.. anaenda kutia sahihi mkataba wa kununua ndege ya Airbus 320 mpya wakati mbovu tuliyokwisha ilipia na ambayo tuna madeni tayari bado hata haijaingizwa nchini.
 
Mwanakijiji naomba data za ndege mbovu ambayo tumenunua haijafika inatokea wapi .Duh!!! maana hili limenipita kabisa .

Kitia

1.Katina ni muhimu sana ukiuliza hilo swali

2.Mgombea binafsi kwa nini Serikali inataka rufaa je ina wasi wasi na kufa kwa CCM ?
 
Feb 14 atakuwa hapa na atalala hapa

Hotel Hilton Berlin, Mohren Str. 30, Plz. 10117 Berlin-Mitte
 
Mwanakijiji naomba data za ndege mbovu ambayo tumenunua haijafika inatokea wapi .Duh!!! maana hili limenipita kabisa .

Kitia

1.Katina ni muhimu sana ukiuliza hilo swali

2.Mgombea binafsi kwa nini Serikali inataka rufaa je ina wasi wasi na kufa kwa CCM ?

Naomba ufafanuzi kuhusu (2)mgombea binafsi.
 
Mtikila alienda Mahakamani kudai haki ya mgombea binafsi bila kupitia Chama .Mahakama ikasema sawa . Serikali imekata rufaa yaani mwanasheria wa serikali nadhani kakata rufaa kupinga uamuzi huo na kama bado wana intent kukata rufaa kupinga mgombea binafsi .
Muulize nini msimo wa seeikali juu ya mgombea binafsi ?
 
Raisi wetu sii tulisema ni Vasko Da Gama?

Hii trip ya kutia sahihi ATCL kununua ndege hawaezi kumwachia hata Mramba?

Angalia ametoka Adis- akafika Dar- akaunganisha Pemba- anakaa siku chache Ujerumani- then Finland! Then...!

Ni mtu wa Masafa- kama Marko Polo!
 
Anatumia nafasi hiyo kuwatangazia wazungu hao kwamba yeye ni Rais wa Tanzania na AU ili wajue wasije wakadhani bado ni John Kufa Oops Kufor
 
Mwanakijiji naomba data za ndege mbovu ambayo tumenunua haijafika inatokea wapi .Duh!!! maana hili limenipita kabisa .

Kitia

1.Katina ni muhimu sana ukiuliza hilo swali

2.Mgombea binafsi kwa nini Serikali inataka rufaa je ina wasi wasi na kufa kwa CCM ?

Lunyungu naomba uende kwenye akaivu ya KLH utakuta hii story pamoja na picha ya ndege mbovu iliyonunuliwa. Mashushu wa JF wakiongozwa na makepteni wa KLH walienda mpaka "huko hiyo ndege mbovu ilikofichwa" wakapata picha yake na Mzee wa kijiji akaiweka kule kijijini!
 
Anatumia nafasi hiyo kuwatangazia wazungu hao kwamba yeye ni Rais wa Tanzania na AU ili wajue wasije wakadhani bado ni John Kufa Oops Kufor

Kuna mtu alisema kama utani hapa kuwa JK ataanza tena safari za kujitangaza kuwa ndio Kiongozi mpya wa AU watu wakapinga.... hayawi hayawi sasa yamekuwa!

Mimi hapa na mbavu zangu tu, sina cha kusema
 
Naam ninamkaribisha hapa Finland kwa mikono miwili, asisahau kubeba koti la nguvu la baridi, kwani sasa huku joto ni chini ya 0
 
Hapana katika ziara hiyo hiyo atakuwa Jijini Hamburg tarehe 15 mara baada ya kusherehekea Valentine na my wife wake (au wife wa ziada).

Hata hivyo bado kuna utata kwani inategemea kama ATC wameshapata udhamini wa serikali na kulipa madeni kwa Airbus.
 
Yeah.. anaenda kutia sahihi mkataba wa kununua ndege ya Airbus 320 mpya wakati mbovu tuliyokwisha ilipia na ambayo tuna madeni tayari bado hata haijaingizwa nchini.

East African airways ilipokufa na Kenya kudhulumu ndege zote aliyekwenda kununua zile fokker Friendship na Boeing Kilimanjaro na Serengeti alikuwa ni waziri tu wakati wa mchonga. Tulikwisha sema tangu alifu huyu kijana ni limbukeni.

Wahenga walisema Limbukeni hana .......... ..........

Kuna mtu alisema kama utani hapa kuwa JK ataanza tena safari za kujitangaza kuwa ndio Kiongozi mpya wa AU watu wakapinga.... hayawi hayawi sasa yamekuwa!

Mimi hapa na mbavu zangu tu, sina cha kusema

Hivi bado hajapata nchi ya kukimbilia?
 
Back
Top Bottom