JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

Walio karibu na system wanasema Rais atavunja baraza la Mawaziri baada ya Uchaguzi wa CCM mwishoni mwa mwaka huu ili kupata timu ya kumfikisha 2015.

Kwa mtizamo wangu hata raisi akilivunja baraza la mawaziri hakutakuwa na jipya. Kitakachotokea ni kubadilishana wizara kama kawaida i.e. waziri wa wizara A atapewa B na wa B atapewa C. Akibadilisha sana itakuwa waziri atapewa unaibu waziri then kazi kwisha. Sasa kwa mtindo huu huwezi tegema performance ibadilike. Kiini hasa cha tatizo ni huyo huyo anayevunja baraza la mawaziri (at least this is how I see it).
 
Watu tunahitaji mabadiliko, lakini ukiona timu nzima ya hawa magamba hakuna aliye bora!
 
Sasa wewe Makoye unaleta habari,then unauliza wanajamvi watoe habari zaidi!!!wewe umezipata wapi tetesi zako!!!
 
JK this is your golden chance to prove that you are ' a man of the people'...
listen to your people,the citizens na waache hao wabunge wachumia tumbo wakwamishe muswada wa sheria kisha wapige chini...
Nakuhakikishia kuwa wananchi watakupa credit na kukusamehe maovu yako yote ulowatendea.
na hao wabunge watakula matunda ya matendo yao maana jimboni watazomewa kama mwizi...
maoni uloletewa na upinzani ndio yanawakilisha wananchi...act on it...

we are watching on you JK..
Be brave enough to turn down their selfish demands.. we all know the source of all this is the POSHO ISSUE...
STAND FIRM JK,NO POSHO.....
 
Pinda hana jipya. Jk anaacha kuwapa uwaziri akina mwanli ambao ni majembe anawaweka akina mkuchicha,mwinyi na wasira
 
Mi namuangalia Pinda kwa sura tofauti..

Pinda ni mtendaji makini sana na nadhani kwake nafasi za juu si matakwa yake.. Yaani ni kama wanafalsafa..huwa hawapendi uongozi,ijapokuwa ni viongozi bora sana...

Najaribu kudhani hata Rais alipomteua,alihitaji kubembelezwa ili akubali nafasi ya uPM.. Kwanini? Yeye hakuwa na kundi,na si mpenda kudurufu mali na hivyo kukosa urafiki ama uhusiano wa kibiashara na mafisadi...

Ni mmoja wa viongozi bora lakini wametumika vibaya na serikali yetu.. Inasemekana alipata kuomba ajiuzulu,akakataliwa,kwani ingebidi cabinet iwe reshuffled kwa mujibu wa katiba.. Na hivyo kuiaibisha serikali ya JK.

Kiufupi,yeye ni ndege wa mbawa tofauti na wenzake,lakini wale wa rangi moja wanamng'ang'aniza kuwa asijali,ili mradi anaweza kuruka..

Hapo ndipo lilipo tatizo...
 
Amuoaye mama yako ni baba yako. JK afanye maamuzi magumu na asiogope. mimi niko nyuma yake. Pinda hafai kuwa PM kwa kuwa hajiamini.

hivi bado kuna watu mnaishi kwa matumaini kua kikwete anaweza kutoa mamuzi magumu?
 
Sijui mpaka nini kitokee ndo waondoke madarakani!
 
naona haya mabadiliko yaguse mpaka spika na naibu spika, hili liwe fundisho kwa wabunge wa ccm waache ushabiki katika teuzi za viongozi iwe spika au naibu spika nk nk, matokeo yake ndio hayo hoja za kitaifa zinapigwa chini.
 
Mchambuzi itasaidia kama utaliangalia hili kialisia na kuacha kumtetea kiongozi wako wa kichama na nchi. Bill aitoki mbinguni kwenda bungeni kujadiliwa na mpaka hapa walipo kutaka kuipigia kura hiwe sheria ujue ni kwamba imepitia process ndefu sana. Sasa embu jiulize ni nani aliepeleka hii bill bungeni (ilianza kama a private motion au ilikuwa ni ya serikali). Kwakuwa imetoka upande wa serikali regardless nani kaianzisha na inahusiano na matumizi yetu wizara husika ilitakiwa itambue hili mapema sana.

Embu sasa jiulize hii kitu imepitia process gani mpaka kufikia hapo ilipo na raisi kakosa vipi information ya bill muhimu kama hiyo ambayo imeanzishwa na serikali yake au mwanachama wake mpaka imefikia hatua ya kutaka kupigiwa kura bungeni. We uoni kama Mr.President ni mzembe na hajui mengi sana yanayoendelea chini yake, surely mtu hawenzi jianzia expensive bills without his blessing mpaka hapa hilipo, kama alijua implications za hii bill in the first place ana madaraka ya kuizuia hata isifike bungeni, kumbuka yeye ndio Mr.President na kiongozi wa chama kinacho ongoza taifa ana mikono mirefu pande zote mbili.

My take ni kwamba ni muongo he knew all along isipokuwa ime-back-fire sasa anataka kuikana for the sake of his popularity. Kwanini nasema hivi waziri mkuu sidhani kama angeweza jiropokea kwenye umma na kumtaja raisi kama kweli hakujua, isipokuwa sasa tu ndio anatafuta mlango wa kucholopokea.

Worst off Spika wa Bunge anasema watu wameshaanza kupokea hizo posho since novemeber, kama muswaada ndio unataka kupigiwa kura sasa ni nani alieidhinsha wabunge kulipwa kama bunge lilikuwa bado hata alijapiga kura za kuridhia iwe sheria. Talk about political satire maana raisi pengine muongo (siamini kama alikua alijui hili) au labda aheshimiki na subordinates wake maana huko ni watu kujianzia tu ndio maana ana ukana leo huo muswada, Spika mlopokaji asiejua hata kauli zake zinakingana na simple roles of the house he runs. The PM is a joke kazi kutumiwa na kubadilikiwa mambo yanapoenda mrama. Thats Tanzania for you.

Naelewa hoja yako kuhusu posho za wabunge. Lakini focus yangu kubwa ilikuwa ni muswada wa mchakato wa Katiba mpya, na kulitaja suala la posho just on the sideline. Nilieleza kwamba sio kweli kwamba Rais hakujua udhaifu wa muswada ule kwani katika kikao chake cha kwanza na Chadema aliwaeleza kwamba kwa analijua tatizo hili ila akikubaliana nao, 'Chama Chake Cha CCM hawatamwelewa'. Na tumeona katika mkutano wake wa pili na Chadema ameunga mkono hoja yao kuhusu umuhimu wa kufanya mabadiliko husika ndani ya muswada ule. Sasa suala la posho za wabunge nikalizungumzia tu as a secondary driver to mmomonyoko wa mahusiano baina ya Rais na Bunge, kwamba wabunge wamueudhika na suala la Rais kukubaliana na Chadema, lakini humo humo wana machungu yao kuhusu msimamo wa Rais kuhusu posho, na matokeo yake ni kuamua kuiadhibu serikali na miswada yake, huku wakisema hawana imani na Rais na wanaweza kumpigia kura ya kutokuwa na imani nae. Mimi nikalenga hapo na kusema kwamba kama suala ni posho na muswada wa mchakato wa katiba, Rais yupo sahihi.

Otherwise ni jambo lisilopingika kwamba utendaji wa serikali ya awamu wa nne umekuwa legelege sana, na mtu wa kupinga ukweli huu atakuwa ni aidha mwendawazimu au anafaidika na ulegelege huo in one way or another. Mimi inawezekana ni mwendawazimu kwa mengine, lakini katika hili la ulegelege wa uongozi wa awamu ya nne, mbali ya CCM kukosa Dira, Serikali hali ndio mbaya zaidi kwani imepatwa na upofu, under his watch - Rais Kikwete. Na kitu kikubwa kinachochangia hilo kwa kiasi fulani ni wasaidizi wake kwani Rais hawezi kusimamia kila kitu serikalini, lakini hao wasaidizi wake wanamwangusha kwa sababu ya Rais Kikwete mwenyewe. Rais sio mkali. Ni suala la kawaida kumsikia Waziri akisema kwamba yeye atakuwa waziri kwa miaka yote kumi ya Kikwete, tena hata mawaziri wenye utendaji uchwara. Hili halikuwa guaranteed miaka ya nyuma.

Ni matumaini yangu kwamba ataanza mwaka huu vizuri, na kwa kuanzia, kwa kulipa bunge discipline ili wawe na uhusiano wa kikazi zaidi kuliko kichama. Inabidi tufikie wakati wabunge wasijione kwamba ni wao ndio they are doing the president a favour; badala yake inatakiwa wabunge waheshimu kiti cha urais; Vile vile baraza la mawaziri nalo lazima lianze kuheshimu kiti cha rais; Kwa mtazamo wangu, Pinda doesnt make a good prime minister katika mazingira haya ya sasa, ni mpole mno; anahitajika mtu kama magufuli ambae ana rekodi ya kuchukiwa na baadhi ya mawaziri wenzake kutokana na kuingilia utendaji wao legelege; Lakini tatizo la wanasiasa wetu wengi ni kwamba ukipewa nafasi kama hiyo, ndoto yako inakuwa sio kutumikia nchi bali kupalilia njia ya kuwa Rais uchaguzi mkuu ujao.
 
Kuna tetesi kuwa huenda yale yaliyotokea mwaka 2008 yakajirudia tena. Safari hii mtoto wa Mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu anaachia ngazi ya Uwaziri Mkuu baada ya tuhuma nzito tatu(3)zinazomkabili katika ofisi hiyo nyeti.
  1. Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa kwa kushirikiana na spika wa Bunge Anne Makinda AMELIDANGANYA BUNGE KUHUSU POSHO ZA VIKAO ZA WABUNGE KUWA RAIS KIWETE ALIKUWA AMERIDHIA NYONGEZA HIYO YA POSHO KUTOKA SHS.70,000/= MPAKA SHS.200,000/=kitu ambacho siyo kweli.
  2. Mizengo Pinda akishirikiana na Waziri wa Afya na NAIBU wake anatuhumiwa kushindwa kusimamia ipasavyo ili kuepusha au kuzuia MGOMO WA MADAKTARI MUHIMBILI MGOMO AMBAO HATIMAYE ULIPELEKEA MGOMO WA MADAKTARI NCHI NZIMA.
  3. Mizengo Pinda kama Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni ameonyesha UDHAIFU mkubwa kwa kushindwa kuwasimamia Wabunge wa CCM ambao wametishia kupiga KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS WAO Kiwete na pia kutishia KUPINGA MSWADA WA KATIBA MPYA YA JMT.
Kwa mwenye habari za undani zaidi kuhusu hizi tetesi naomba aendelee kutupasha zaidi.

Nawasilisha
hoja hii ni ya siasa zaidi yaani blabla haina mshiko, kwani imegengwa kwenye fikra binafsi zaidi, haina chanzo cha taarifa.
 
Tunatega masikio kusikia kifuatacho!!! Haieleweki nani anasimamia nini na nani anawajibika wapi, mambo si mambo kabisa? Kwa watanzania wa leo nataraji kuibuka jambo lisilotarajiwa na kubwa na la kihistoria kwa nchi yetu.
 
avunje wizara ya aya ampe nape nnauye ataiweza yeye ni mtetezi wetu ss wanyonge!
 
Wana JF naomba tusaidiane kuchambua ni Mbunge Gani kama kweli Ijumaa Rais atalivunja Bunge unadhani atarudi Bungeni?
Je na kama atavunja Baraza la Mawaziri unadhani ni nani anafaa kuwa waziri na ni Wizara gani?
Nawasilisha...
Kuna wabunge wengi sana ambao ni very competent lakini kwa sababu moaj au nyingine hawajateuliwa katika nafasi hiyo chini ya awamu ya nne. Ukiachilia wabunge wa majimboni, Rais ana nafasi kumi za kuteua mtu yoyote kuwa mbunge. kama tunavyojua, mbunge wa kuteuliwa hana much commitment kama yule wa jimboni, ana muda mwingi sana wa kufanya mambo yake, sasa Rais angeteua mawaziri wa sekta muhimu kama Fedha, Afya, Elimu n.k kutoka miongoni mwa wabunge wa kuteuliwa - ambao atawapa huo ubunge on merit, sio kwa fadhila. Hapo tutaona tofauti kubwa sana katika wizara husika. Lakini pia labda niseme kwamba kuna tabia ya baadhi ya makatibu wakuu kuwakwamisha mawaziri wao kwa sababu mbali bali, lakini hili watu huwa hawalisemi; hili ni tatizo kubwa sana katika utendaji serikalini. Inabidi mfumo wa makatibu wakuu pengine ufutwe ili wabaki wakurugenzi wa idara tu ili nguvu wizarani isambae kulingana na vitengo, sio kuwa chini ya mtu mmoja tu - katibu mkuu, ambae akigongana na waziri wake kuhusu mhudumu wa chai, kazi wizarani zinageuka kutoka zile za kuwahudumia wananchi, na kuwa za kukomoana kwa viongozi husika.
 
Back
Top Bottom