JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

avunje wizara ya aya ampe nape nnauye ataiweza yeye ni mtetezi wetu ss wanyonge!

Huyu ilitakiwa hata bungeni aingie kupitia zile nafasi kumi alizokuwa nazo Rais za kuteua wabunge, sijui kwanini Rais anachelewa katika hili. Nape anatakuwa awepo bungeni (hata bila ya uwaziri), mbali ya kuwa na nafasi yake katika Chama.
 
Rais anazidi kuchelewa kufanya maamuzi makubwa, mwelekeo wa wasaidizi wake umepotea kiasi kwamba siku si nyingi kila mmoia atashika njia yake. Misuguano ni mikubwa mno. Inaonyesha sasa kila mmoja anasema bora liende tutakakoangukia hukohuko.Mfano ni wale wanaotoka ofisi moja na kuwa na kauli tofauti ni ajabu na kweli, hakika wanatakiwa kusalimu amri kuwa sasa ni maji ya shingo. Hakuna hata sekta moja iliyo sawa, kila mahali wanalia kivyao. Tulishaambiwa vita nyingi huletwa na tofauti kubwa ya walionacho na wasionacho kwa Tanzania hilo ni tatizo kubwa mno kwa sasa. Hayupo aliyeko madarakani anayekumbuka shida za watanzania kwa sasa, wote wanaangalia maslahi binafsi tu kuanzia mkuu wa kaya!!!!
 
kwa nini hii thread bado haijapotezwa na mods?
 
Mwenyekiti ana fadhaiko wa akili.....damu za watu wasio na hatia zinamuadama. na hao tiss waende to hell
 
Huyu ilitakiwa hata bungeni aingie kupitia zile nafasi kumi alizokuwa nazo Rais za kuteua wabunge, sijui kwanini Rais anachelewa katika hili. Nape anatakuwa awepo bungeni (hata bila ya uwaziri), mbali ya kuwa na nafasi yake katika Chama.

Mchambuzi,

Rudia posti zako zilizopita. Katiba ya sasa ni ya 1977 wakati wa chama kimoja. Hivyo check and balance haipo. Kumteua Nape inaweza kuwa jambo zuri. Lakini akienda bungeni na yeye akanogewa na masimbi ya bunge anaweza kujisahau.

Sasa hivi ni kushinikiza tu masuala ya katiba hili katiba ipatikane ambayo watu watakuwa hawaogopi chama bali waliomchagua.

Wabunge wakijua kuwa kuna wagombea huru, wagombea wa vyama vya upinzani wataweka akili nzuri. Vilevile viti maalumu viondoke. Kama kuna nia ya kuwashirikisha kina mama, basi kwenye majimbo wakubaliane kuwaachia kina mama.
 
Suala la katiba upo sahihi - kuhusu ukosefu wa check and balance mechanism. Hoja yangu juu ya Nape na ubunge ililenga kuunga mkono hoja ya mdau mwingine, nikiwa na mtazamo kwamba - katika hali ya sasa CCM inahitaji wabunge wenye ujasiri na walio tayari hata kupingana na hoja za kijinga za serikali na chama tawala mle ndani ya bunge. Ndio maana nikamtaja mtu kama Nape ambae kwa kiasi kikubwa ameonyesha uwezo katika hilo, ingawa kweli inawezekana akayeyuka na yeye mle ndani kama wengine. Inasikitisha kuona wabunge kama Kilango wakiwa kigeu geu, Ole Sendeka nae sijui nini kimemsibu, na wengine kadhaa ambao waliwapa matumaini wananchi.
 
........ ajiuzulu kikwete, ndio kikwazo cha maendeleo ya nchi hiiii........
 
Wana jamvi
Hapa Dodoma kimenuka. JK kafika kutoka MWZ ili kuonana na wabunge. Wabunge wa CCM wakaitwa na kuingizwa ukumbini ili kumsubiri. Awali Katibu wao Jenester Mhagama alitoa tangazo kupitia Naibu Spika kuwa wabunge wote waache simu zao wazi ili kuitwa wakihitajika.
JK aliendelea kupata briefings na kuambiwa hali ni mbaya. Akashauriwa afanye reshuffle upesi ili kupoza moto. Kama kawaida akawa mbishi, lakini pia akasita kuingia ukumbini kuonana na wabunge. Mwishowe wabunge wameambiwa waende kulala kwa sababu JK bado ana kikao na watendaji.
Kuna hatari kesho ya reshufle. Mawaziri wote matumbo moto hususan Afya, Nishati, Fedha na Ujenzi. Vijana wa TISS wamemweleza kuwa baraza zima ni kama haliko kazini isipokuwa wizara moja tu- Ya Pombe Magufuli.
Vijana wa TISS wameingia kazini kwa kasi sana usiku huu kujaribu kubadili upepo miongoni mwa wabunge.

Chanzo: Mimi mwenyewe nikiwa Dodoma mjengoni.
Ampe Magusifuli uwaziri mkuu ili tuwe na kasi ya kupiga mbizi,pia ataifanya Chato makao makuu ya mkoa.Magusiufuri si mkyeso bana
 
=======
Waliokuwa wanamshauri ni viongozi wa CCM ndani ya bunge (kamati ya CCM) - Mhagama, Ndugai, PM na wajumbe wa Kamati Kuu walio katika serikali. Walikuwapo pia viongozi waandamizi wa TISS. Yeye kang'ang'ania eti Beatrice Shelukindo na wenzake wampigie kura ya kukosa imani naye. Mbishi kweli.
Amwambie EL na RA kuwa wampigie kura ya kukosa imani kama kweli hawajampigia,Beatrice ni dagaa tu
 
Akitoka Dom break ya kwanza atawahutubia wazee wa Lalasalama,watampigia makofi wee hadi ''stresi''iishe
 
Je hali itakuwa vipi ndani ya CCM baada ya wimbi hili la kisiasa kupita?
 
Suala la katiba upo sahihi - kuhusu ukosefu wa check and balance mechanism. Hoja yangu juu ya Nape na ubunge ililenga kuunga mkono hoja ya mdau mwingine, nikiwa na mtazamo kwamba - katika hali ya sasa CCM inahitaji wabunge wenye ujasiri na walio tayari hata kupingana na hoja za kijinga za serikali na chama tawala mle ndani ya bunge. Ndio maana nikamtaja mtu kama Nape ambae kwa kiasi kikubwa ameonyesha uwezo katika hilo, ingawa kweli inawezekana akayeyuka na yeye mle ndani kama wengine. Inasikitisha kuona wabunge kama Kilango wakiwa kigeu geu, Ole Sendeka nae sijui nini kimemsibu, na wengine kadhaa ambao waliwapa matumaini wananchi.

Nimekupata. Lakini mwache Nape akae nje kwanza. CCM wakiwa na safu za watu wazuri, katiba haitabadilika. Wacha kwanza katiba ibadilike na wakina Nape waje wakiwa na uhuru wa kisiasa.
 
Mimi nadhani hii ni nafasi pengine ya mwisho kwa JK kurudisha hadhi yake na ya CCM mbele ya umma. Anahitaji kufanya mabadiliko makubwa na kuondoa mawaziri legelege wote; pia mwanasheria mkuu wa sasa hatoshi, huyu hafai katika mchakato wa kupata katiba mpya. Pia ni muhimu kwa rais kubadili mfumo wa serikali, hasa sekta ya elimu na afya. Pia apunguze ukubwa wa baraza la mawaziri kwa kufuta wizara nyingine au kuziunganisha ili iwe ishara kwa umma ya kuanza kubana matumizi tunapoelekea bajeti mpya mwezi juni. Na katika hotuba yake kuunda baraza jipya, awe mkali na awe tofauti kabisa, na ashike uzi huo huo kwa kipindi chake kilichobakia. Akiachia nafasi hii imponyoke, atakuwa na shughuli nzito sana ya kukipa CCM uhalali mbele ya umma, na pia mawaziri wengi wataendelea kumchukulia kama mshijaki. Hili litakuwa janga kubwa kwake hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa CCM, Novemba mwaka huu.

Huwezi kuondoa tatizo la nyumba yenye msingi unaodidimia kwa kuipaka rangi. Kuvunja baraza la mawaziri ni danganya toto kubwa kuliko ile ya Mwinyi kusema "wahalifu dawa yao inachemka" na kuja kutupa Mrema.

Tatizo letu hatuna utamaduni wa kuwajibishana, hatuna utamaduni wa kutoridhika na kutokubali kudanganywa, hatuna utamaduni wa kutolindana. Ndiyo maana unaona mtu ambaye kajiuzulu kwa kashfa kama Lowassa leo anaongelewa favorably kwamba anaweza kuwa rais.

JK akivunja baraza la mawaziri atakuwa anataka kutibu TB kwa Cofta, hizi cosmetic covers hazisaidii.

Kama rais anataka kuwawajibisha mawaziri wake hashindwi, na kama rais hawezi kuwawajibisha mawaziri wake hawa, kipi kinawafanya mfikiri kwamba ataweza kuwawajibisha mawaziri wapya?
 
Binafsi sijaona waziri aliyefanya jambo baya la kufukuzwa uwaziri. Labda mnijulishe.
 
JK directionless government is doomed to fail, no wonder he remained carefree and unconcerned with people's dissatisfaction over his cabinet's performance even after repeated calls to substitude his underperforming ministers with competent ones. He, at this point of time, seems to respond to the public sentiment but its too late to rescue this stumbling country from falling. The reshuffle he is contempleting to carry out will not help change deteriorating things but only could diffuse the damage that was otherwise to be spawned by the collapse.
Mkalimani plz am kata secondary product nimetoka kapa
 
-Spika Makinda: Wabunge wana hali ngumu kwa kuwa WAMEKOPA sana! Bila shaka Spika ana maanisha wamekopa kwa ajili yetu, wapiga kura wao. Mikopo yao hiyo ni kwa ajili ya maendeleo ya majimbo yao!
-WM Pinda: Posho hizi tunazigawa kwa wananchi. Tukitoka humu mjengoni wapiga wetu wapo hapo nje wanatusubiri tuwasaidie nauli, karo, hela ya matibabu,...Mfuko wa Jimbo unafanya kazi zipi?
-NS Ndugai: Hamjui tu wenzetu huko kwenye mihimili mingine wanalipanaje. Mnatuandama sisi tu. Mtu kama Sumaye aliyejiandalia mafao mazito kabla ya kustaafu uwaziri mkuu eti naye anahoji posho hizi. Sumaye analipwa 80% ya mshahara wa sasa wa WM Pinda kila mwezi pamoja na huduma zingine.
Yoote haya tunagharamia SIASA na WATEULE wachache wa wanasiasa hawa. Tufanyeje?
 
Back
Top Bottom