JK na Shahada za heshima

JK na Shahada za heshima

Haya ndo yetu wasomi wa kiafrika! Siku ya sherehe za uhuru kwenye radio moja kuna mzee mmoja alisikika akiuliza kwamba tuna madokta na maprofesa kibao lakini hajawahi kusikia vipi tafiti au gunduzi za hawa wanazuoni wanaongezeka na kutangazwa kila siku zimesaidia nchi yetu kutoka hatua moja kwenda nyingine kimaendeleo zaidi ya tafrija za kupongezana kwa kupata nondoz zisizojaribiwa katika matendo ya kijamii na kiuchumi wa watu! Hii ni changamoto hata kwa hawa wanotunuku na si anayetunukiwa bila kuomba kwani wanjua vigezo wanavyotumia kufanya hivyo japo wanaweeza kuvipindisha ku-fit their agenda!
 
Haisaidi,hata akipewa degree za heshima 100...Jk ni kiraza tu and pure failure!...kamaliza UDSM kati 1974 au 1975 na kwa nafsi zote alizopata kushika serikalini hakuweza kuongeza elimu yake hata kidogo...being in foreign ministry for 10yrs still he doesn't know any foreign language...jamaa ni zero brain
 
Jana Tumeshuhudia tena Raisi wetu akipewa Degree ya Heshima baada ya ile ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Safari hii ameibukia Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili.

Hivi hizi Degree za Heshima zitamsaidia nini kuongoza nchi. Ukifikiri sana hapa inaonekana kuwa ni usanii na uswahili wa Raisi wetu kupenda sifa kuliko kufanya kazi.

Kwa nini asifanye kazi ili Watanzania wamtunukie Degree ya Heshima kwa kazi nzuri alizofanya. Kwa sasa Watanzania wengi wanaishi kwa shida, bila kupata mahitaji yao ya lazima. Gharama za Maisha zimepanda mno.

Tunafikiri Raisi wetu angeshughulikia kero za Watanzania badala ya kila siku kupanda kwenye majukwaa kupewa Degree za Heshima na Ma- Profesa wanaotaka sifa kutoka kwake.

Raisi wetu Degree za Heshima nzuri zipo kwa Watanzania kama utawatumikia vyema. Lakini kama utaendelea na usanii huu, Watanzania hawatakuheshimu kwa kuwa na hizo Degree za Heshima za Wasomi wanaotaka sifa kutoka kwako.


Cha kuchekesha na kushangaza ni kwamba katika vyuo hivi vyote yeye ndio wa kwanza kupewa degree ya heshima. Muhimbili haijawahi kutoa kwa yoyote zaidi yake. Je ni kweli hakukuwa na wala hakuna mwingne aliestahili zaidi yake???

Au ndo ule msemo wa amezi-force?????
 
Huyo anayempa hiyo degree, yeye mwenyewe mbona naskiaga hana degree yoyote?
 
Huyo anayempa hiyo degree, yeye mwenyewe mbona naskiaga hana degree yoyote?


Unadhani mwenye akili timamu atatunuku hivihivi??? Anyway katika mazingira yetu ya "kuperembana" kila kitu kinawezekana

Acha wafu watunuku wafu wenzao
 
Kati ya mambo yanayonichekesha ni hizi shahada za heshima zinazotolewa kwa viongoz. Hivi majuzi JK ametunukiwa shahada za heshima na vyuo vya nje ya nchi na ndani ya Tz. Mshangao wangu unaenda ni jinsi watendaji katika baadhi ya vyuo vikuu hapa Tz wanavyohangaika kumpa shahada za heshima JK. Nilishangaa sana chuo kikuu cha Dodoma ambacho nadhani hakijatoa mhitimu wa kwanza wa PhD, lakini wanajigonga kwa JK kumpa PhD ya heshima wakati chuo chenyewe bado hakijajengea heshima yoyote.

Watanzania hatuamhitaji rais anayekimbilia shahada za heshima bali anayewaletea maendeleo wananchi wake. Rais anashindwa kujua kuwa baada tu ya uchaguzi bei ya bidhaa mbalimbali imepanda kwa asilimia kubwa. Serikali bado haijasema chochote kuhusu hilo zaidi ya kuogopa mgawo wa umeme baada ya Kafulila kumtishia waziri wa nishati na madini na hoja ya kutokuwa na imani naye.

Tunamhitaji rais ambaye yupo makini na anashughulikia masuala yanayogusa maslahi ya Taifa. chonde chonde wakuu wa vyuo vyetu muwe makini na shahada zenu hizo mnazowatunukia hawa wanasiasa.
 
Usishangae ndugu yangu watu wa Pwani wanapenda shughuli na sifa
 
Hivi Nyerere alipata kupokea hizi shahada ngapi vile? Tena alikuwa anapanda pipa kwa fedha zetu kwenda kuzipokea hizo shahada!
 
Chuo cha Uvuvi Mbegani wampatie Tuzo Mkwere wetu jamani! Nikosa Kumlinganisha Mkwere na baba wa Taifa....Kikwete is the worse president in Tanzania History
 
Naona anashindana na rafiki yake Mugabe (anazo hizi shahada hewa 18 na ndiyo anazidi kuwa zuzu zaidi na zaidi..)
 
Hivi Nyerere alipata kupokea hizi shahada ngapi vile? Tena alikuwa anapanda pipa kwa fedha zetu kwenda kuzipokea hizo shahada!
Hii ya Kikwete ya jana nasikia kaiomba mwenyewe. Hajafanya lolote la maana kustahili tuzo ya udaktari katika uganga. Angalau Nyerere alifanya mengi kuhusu ukombozi wa Afrika na aliupa changamoto kubwa ulimwengu wa magharibi kuhusu uhusiano wake na nchi zisizoendelea. Wazungu walipenda mawazo yake na kumtunuku. Mkwere ni bogus.
 
Hakuna la maana hapa. Hivi ndivyo walivyo viongozi wa kiafrika, kuongoza nchi kumewashinda wanabaki kujitafutia sifa za kuchakachua.
Digrii kama hizi zimetolewa kwa viongozi vilaza kabisa duniani na kumbukeni hata Iddi Amini alilazimisha kama alivyofanya huyu wa kwetu na kupewa digrii na Chuo cha Makerere! Tusiwalaumu wakuu wa vyuo vikuu kwani hawana kabisa ubavu wa kuwakatalia viongozi waroho wa sifa, madaraka na wapenda makuu kama hawa wa kiafrika. Nyerere alitunukiwa PhD kibao na vyuo mbaljmbali lakini alikufa akiitwa Mwalimu na kama kuna namna ya kumwita aliipenda ni kuitwa Mwalimu au Ndugu!
 
Watu wa 'mwambao' wana hulka ya kupenda 'mteremko' na 'kusifiwa'. Sishangai kinachoendelea.
 
Wakuu,
Mmesikia nyingine kali hiyo, eti Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Mzee Alli Hassani Mwinyi ametunuku rais Kikwete digrii ya heshima ya udaktari wa afya ya jamii wakati wa mahafali ya nne ya chuo hicho. Mnaionaje hii kasi ya wazee kukabidhiana hizo digrii??? Alianza Mzee Mkapa pale UDOM na sasa Mzee Mwinyi nae amejibu mapigo. Sijui nani atafuata kumtunuku JK digrii nyingine manake wazee wa aina hiyo bado wengi sana!!

Chanzo cha Habari: Tanzania Daima, tarehe 12 Desemba 2010.
 
Wasi wasi wangu ni kwamba Mkwere atakua analazimisha kupewa hizo degree. Kama angekua halazimishi I think pamoja na kupewa hizo za heshima nyingi asingekubali ku-address-siwa kama Dr. Naona yeye yuko comfortable tuu kuitwa Dr. ka vile kasomea. Mbaya zaidi wala sioni mchango wake katika jamii unaopelekea yeye kupewa hata hizo za heshima ...
 
Hivi Nyerere alipata kupokea hizi shahada ngapi vile? Tena alikuwa anapanda pipa kwa fedha zetu kwenda kuzipokea hizo shahada!

Unataka kufananisha utendaji wa Nyerere na Jakaya? Isitoshe Nyerere alikua akiitwa Mwalimu Juliasi Kambarage Nyerere na sio Dr. Nyerere, we vipi?
 
hahahahaha
hivi mwinyi yeye aliwahi kupewa hizi digrii
 
Vyuo viko kibao siku hizi. By 2015 atakuwa kishapewa za OUT, SUA, USDM, SAUT, Tumaini, MZUMBE, Ushirika............!!!!!! Hivyo apange ratiba yake vizuri tu anaweza akaweka record ya kuwa na degree nyingi za heshima!!!
 
Wakuu,
Mmesikia nyingine kali hiyo, eti Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Mzee Alli Hassani Mwinyi ametunuku rais Kikwete digrii ya heshima ya udaktari wa afya ya jamii wakati wa mahafali ya nne ya chuo hicho. Mnaionaje hii kasi ya wazee kukabidhiana hizo digrii??? Alianza Mzee Mkapa pale UDOM na sasa Mzee Mwinyi nae amejibu mapigo. Sijui nani atafuata kumtunuku JK digrii nyingine manake wazee wa aina hiyo bado wengi sana!!

Chanzo cha Habari: Tanzania Daima, tarehe 12 Desemba 2010.

Anastahili hizo digrii kwa yale mema aliyo ifanyia Tanzania. Kwa kweli abarikiwe na Mungu amlinde na husuda na fitina za watu wabaya wasio itakia Tanzania yetu mema 'amin'.
 
Back
Top Bottom