sometimes watu nasi tuwe reasonable......sidhani kama chuki na dharau zitatusaida kwa sasa!
Kila mtu anahaki ya kuchagua mtu wa kumkubali. JK amelazimisha kuwa raisi kwa kura ambazo ni yeye tu na wapambe wake wanaojua walizipataje. 2 plus 2 huwa ni nne. JK amelazimisha 2 plus 2 iwe saba na bahati mbaya Dactaroli JK amekataa kusema kagundua kanuni mpya ya hesabu. "Bwana mtake msitake lazima 2 plus 2 iwe saba.
Sasa na wewe unachokileta hapa ni ubabe huo huo unataka tutake tusitake lazima tumpende na kumheshimu jk. For your informationto be loved and to get respect depends much on how one brands him/her self. As for now, hutalazimisha watu wapige makofi ya kushangilia pumba za jk. Ni watu wasiokuwa na uwezo wa ku fikiri na ku reason peke yao watalazimishwa kufagilia kitabu cha wasifu wa mtu aliyejaa kashfa na unafiki.
JK ni mtu mbinafsi anayefanya mambo yote kwa maslahi yake binafsi. Na anapenda kusifiwa kama mtoto.
Zaidi ya yote pamoja na kuwaumiza watu hataki kuona watu waseme ubovu wake. Ubadhilifu wa mali za uma, utendaji kazi mbovu, ubinafsi na udictator wake sasa anajikosha kwa kuandika kitabu.
Personally sina munda wa kusoma habari zake kwani hana maana. Hakuna kitu nitapata kwa sababu sina cha kujifunza toka kwake. Wala hana la kuniburudisha. Kama anataka watu wasome aandike kitabu cha ufafanuzi juu ya "Anguko la CCM". Aeleze jinsi ufisadi ulivyoanza kuingia na kusharimiri ktk Serikali ya CCM na kudumaza maendeleo ya Watz. Brainwashing strategies zilizotumika kuwafanya wa Tz kama wewe hapa waendelee kupiga makofi ya kushangilia watawala huku ndugu zao wakifa kwa kukosa huduma za afya. Watz wakipiga makofi kushangilia elimu imekuwa kwa kuwa kuna shule nyingi za kata bila kuona kwamba hizo ni kambi zilizolenga kupunguza vijana wazururaji na vibaka mitaani na si sehemu ya kupata elimu. Azungumzie jinsi jopo lake na mafisadi wenzake walivyojipanga kuibia nchi kwa makampuni na mikataba ya wizi. Aseme namna anavyotumia muda wake wa kukaa ikulu kuwalinda mafisadi na kuwashamirisha ili waendeleeze utawala vizazi vyao vyote. Namna wanavyolinda mtaji wao wa kuendelea kuteketeza nchi ambao ni "ujinga endelevu wa wa Tz."
Kinyume cha hapo mpenzi, sioni anaujasiri gani wa kuandika kitabu cha kujifagilia kama si kukosa aibu na kuzidi kuonyesha dharau zake kwa wa Tz. Kwamba wote ni wajinga wasioweza kufikiri wala kuelewa mambo anayofanya yeye na serikali yake.
"Dharau na chuki hazisaidii kwa sasa" una maana gani? Unafiki na kujikomba kwa mafisadi ni dalili ya kukosa ufahamu na kujitoa muhanga ufe kijinga.
It is too late. Kitabu hicho wagawieni mafisadi wenzenu mliopanga nao namna ya kuunda mazingira mabovu yakuwatengenezea mlango wa wazi wa kuibia taifa kwa mlango wa Dowans. sisi hatuna interest na unafiki wenu. If possible wagawieni hao waliopewa madaraka kama u DC, Ubunge nk kwa ajili ya kulipwa fadhila.
Sis watz hatuna hisa kweny hayo mambo yenu. Huko huko, usitulamishe kumpenda na kumheshimu mtu aliyeshindwa kujiheshimu mwenyewe.
Tena hii thread iishe. Hatuna muda wa kumjadili jk na mamluki wake.
.