JK awa Vasco da Gama ... Makala ya Raia Mwema

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
802
Baada ya kusoma makala iliyo kwenye gazeti la Raia Mwema kuna maswali mengi sana ambayo ninashindwa kupata majibu yake, aidha mwandishi wa makala hiyo hakutoa majibu yake ama ametoa mwanga kiasi. Mwenye details naomba atupatie kwa undani majibu ya baadhi ya maswali niliyo nayo:

1. Kwanini Mh. Kikwete safari za US hazi-delegate kwa wasaidizi wake (Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Bwana Membe)?

2. Kwanini safari ya Iran alipewa Mzee Shein? Inawezekana JK alikuwa anakwepa kitu huko Middle East au kuna conflict of interest?

3. Kwa nini Makamu wa Rais hapewi mojawapo ya hizi ziara za kwenda Marekani?

4. Kwa mara nyingine nimeona swala la uswahiba wa Tanzania na Marekani linaelekezwa kwenye sababu za kiusalama, je, kuna ukweli wowote kwamba hawa jamaa zetu (Marekani) wana mpango wa kuja kuweka base hapa Bongo?

Nadhani kuna maswali mengi sana, lakini haya ndiyo ambayo ninatamani kupata ukweli. Kwa wale walio karibu na system naomba watupatie majibu au kama kuna mtu mwenye majibu yake naomba nieleweshwe, yawezekana nina upeo mdogo wa kung'amua mambo.

Makala hiyo iko hapa: http://www.raiamwema.co.tz/07/12/5/3.php
 
VDG bado hajamaliza kuivumbua US, maana ni nchi kubwa ati! pia si ajabu anataka kuvunja rekodi ya 'Rais wa Tanzania aliyekwenda US mara nyingi kuliko Rais mwingine yeyote' Si ajabu katika miaka miwili aliyokaa madarakani anakaribia kuivunja rekodi ya Mwalimu Nyerere (RIP) aliyekaa madarakani miaka 24.

Kikwete awa Vasco Da Gama kwa safari za nje

Lula wa Ndali-Mwananzela Disemba 5, 2007

Atarudi Marekani karibuni
KUNA vitu ambavyo vinalingana na vile ambavyo havilingani. Kuna matukio ambayo yanafanana na yale ambayo hayafanani. Kuna watu wanaofanana na wale ambao hawafanani. Kuna wanaofanana kwa sababu ya undugu wa damu (mapacha n.k) na wale ambao wanafanana kutokana na sababu za kinasibu tu.

Kwa upande wa binadamu, hata hivyo, hata wale wanaofanana utakuta wanatofautiana kwa kiasi kikubwa. Hata hivyo, kuna wakati ambapo kufanana kwa watu fulani kunatusukuma kujenga hoja mbalimbali kuhusu watu hao licha ya kujali tofauti walizonazo.

Mfano mzuri ni kumlinganisha Mahatma Gandhi na Dk. Martin Luther King Jr. Watu hawa wanatofautiana sana katika mazingira ya jiografia waliyoishi, na ingawa ni watu wa nyakati moja walitofautiana kinasaba na kihistoria.

Hata hivyo, utaona kuwa wanalingana katika mambo ya msingi kama vile wote wawili walipigania haki za watu wao kwa kutumia njia zisizo na matumizi ya nguvu, na wote wawili walijenga hoja ya watu wao kupata heshima na hadhi ya kutambuliwa utu wao.Wote walikataa uonevu wa mwanadamu mmoja kwa mwingine na hatima ya wote wawili ni kuwa walikufa kutokana na vitendo vya mahasidi wao.RAIS Jakaya Kikwete

Ni katika kutafakari kulingana kwa watu, matukio na mambo mbalimbali nilijikuta nikimuangalia Rais Jakaya Kikwete na kujaribu kutafuta mtu wa kihistoria ambaye anafanana naye kimsingi. Baada ya kuangalia kwa muda mrefu nimejikuta na mtu mmoja ambaye sisi watu wa Afrika ya Mashariki tunalijua jina lake vizuri kwani mtu huyo amepitia katika maeneo yetu karibu miaka mia tano iliyopita. Huyu si mwingine bali ni msafiri, mwanasiasa na mvumbuzi wa Kireno, Vasco Da Gama.

Ndiye huyo ambaye historia inamrekodi aliyeweza kuonesha njia ya kutoka Ulaya kwenda India kuzunguka kusini mwa Afrika. Rais wetu Jakaya Kikwete anafanana sana na Vasco da Gama na ni kufanana huko ambako leo kunanituma kuangalia safari za Rais Kikwete nje ya nchi, safari ambazo kwa hakika siyo tu zimekuwa za uvumbuzi bali ni za utambuzi, ugunduzi na kwa hakika zimekuwa ni safari za mwanasiasa, mwanadiplomasia na za kiongozi.

Mwanzoni mwa utawala wake na mara alipoanza safari hizi za kwenda nje ya nchi, tuliambiwa kuwa Rais wetu anafanya hivyo ili kujitambulisha kwa viongozi wa nchi za kigeni kuwa yeye ndiye "Rais mpya wa Tanzania". Wengi tulikubali dhana hiyo bila kuihoji kwa undani kwa sababu tuliamini kabisa kuwa mataifa ya kigeni hayakufuatilia uchaguzi wa Tanzania na kwa hakika hawakujua Rais mpya wa Tanzania ni nani.

Na kwa vile Rais Kikwete alitaka atambulike hivyo ilibidi aende yeye "mwenyewe" kuwaonesha sura yake na tabasamu lake la kukata na shoka. Hivyo safari zake za mwanzo kwenye nchi jirani zilikuwa na lengo la kujitambulisha. Hivyo ndivyo tulivyoambiwa. Miaka miwili baadaye safari za Rais Kikwete na wapambe wake zimezidi kupamba moto bila kukoma. Hivi karibuni Rais Kikwete ataondoka tena kwa ziara ya siku kadhaa huko Marekani.

Kati ya vitu ambavyo tunaambiwa kuwa Rais Kikwete anaenda kufanya ni kutangaza rasmi ujio wa Mkutano wa Kimataifa wa Taasisi ya Sullivan ambao utafanyika nchini mwakani. Kinachoshangaza sisi ambao ni wachunguzi wa mambo ya kisiasa nchini ni ulazima wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kutuutangazia ulimwengu ujio wa mkutano huo nchini.

Hivi ni kweli kuna ulazima wa Rais kwenda kufanya jambo hilo na hakuna kiongozi mwingine anayeweza kumuwakilisha kwenye tukio hilo? Imepangwa kuwa katika hafla hiyo Rais Kikwete atatumbuizwa na kundi la muziki lililotamba mwanzoni mwa miaka ya tisini la Boyz II Men.

Endapo tumefikia mahali kuwa Rais wetu ni lazima aende kwenye vihafla hivi na vimkutano hivi, kwa kweli kuna jambo moja tu ambalo ni dhahiri; nalo ni kwamba Rais Kikwete anapenda kusafiri sana, na safari zake hizi za uvumbuzi na utambuzi zimeanza kukaribia zile za yule msafiri wa Kireno, Bw. Da Gama.

Hata hivyo, watetezi wa safari hizi na makada wa chama tawala wanatuambia kuwa safari hizi siyo za utambuzi tu bali pia ni safari zenye "maslahi makubwa kwa Taifa". Wanapotetea safari hizi makada hawa wanajaribu kutushawishi tuamini kuwa pasipo Rais Kikwete kwenda huko anakokwenda (iwe Uarabuni, Marekani au Ulaya), basi, misaada hiyo na uwekezaji huo hautakuja.

Mfano mzuri unaotolewa ni ahadi ya kutoka Shirika la Changamoto ya Milenia ambapo tumeambiwa kuwa Tanzania itapata karibu dola nusu bilioni miaka michache ijayo. Ilipotangazwa habari hii miezi michache iliyopita, Rais Kikwete alikuwa Marekani na waliopiga baragumu la ushindi wakatuambia kuwa (japo si kwa maneno hayo moja kwa moja) kuwa tumepata msaada huo toka Marekani kwa sababu Rais Kikwete alikwenda huko.

Kitu ambacho hawakutuambia ni kuwa Tanzania haikuwa nchi peke yake iliyopewa ahadi kama hiyo baada ya kutimiza vigezo fulani fulani. Lesotho, nchi yenye watu milioni 2.3 (chini ya idadi ya watu wa Jiji la Dar), imepewa msaada kama wa kwetu wa dola milioni 362), Mongolia, yenye watu kama milioni 3 hivi, na wenyewe walipata msaada kama wa kwetu wa dola milioni 285 na El Salvador, yenye watu karibu milioni sita, wao wamepewa msaada huo toka kwenye akaunti ya Changamoto ya Milenia wenye kiasi cha dola milioni 461.

Hivyo, kufikiri kuwa tulipata msaada huo kwa sababu ya Kikwete kwenda huko ni kujidanganya. Ukweli wa mambo ni kuwa kuna misaada tunayoipata ambayo inaweza kuja bila ya Rais Kikwete kwenda huko kuomba au kuonesha sura yake. Endapo tutaweza kutimiza masharti au malengo fulani fulani wahisani wataona na watasaidia kama wanataka.

Binafsi, naamini kabisa kuwa baadhi ya safari hizi na msururu mzima unaoandamana na Rais Kikwete kwenda nje ya nchi siyo za lazima na zinaweza kufanywa na kiongozi mwingine ye yote yule kama Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Mfano mzuri ni ziara iliyopita ya Makamu wa Rais huko Iran na Misri. Kwa nini Makamu wa Rais hapewi mojawapo ya hizi ziara za kwenda Marekani? Kwa nini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano asiende kwenye mojawapo ya misafara hii?

Isitoshe, safari hizi ni gharama kubwa kwa walipa kodi masikini wa Tanzania. Kwa mfano, kwa mwaka jana peke yake, inakadiriwa kuwa ziara za Rais zilitumia karibu shilingi bilioni 20 (safari, posho, na masurufu mbalimbali). Mwaka huu peke yake sina uhakika, lakini kama kuna mtu atakuwa tayari kutuambia ziara za Rais na viongozi wa juu zimegharibu kiasi gani, tunaweza kupatwa na shinikizo la moyo.

Kwa wale wanaokumbuka, wakati wa kusainiwa mkataba wa Buzwagi kule London, Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Edward Lowassa wote walikuwa nje ya nchi. Msiniulize kwa nini?

Wapambe wanaofuatana na Rais kuanzia wasaidizi, maafisa usalama na wengine kadhaa wanalipwa posho za safari. Na niwahakikishie hizo posho hazilipwi kwa hela ya madafu. Baadhi yao ambao tumepata nafasi ya kugongana nao kwenye mitaa ya New York na Washington DC, na wale ambao tuliweza kupiga nao soga pale London, walikuwa na hela utadhani Bill Gates. Baadhi yao walipotualika hotelini kwao walikuwa wanachomoa toka kwenye mifuko yao "tudola" utadhani wameziokota.

Hawana uchungu nazo na hawana wasiwasi wa matumizi yake. Kuna wengine kwa uwezo walionao (na ni maafisa wa chini) ambao hutumia nafasi hizi za safari kufanya "shopping za nguvu". Nakumbuka mmoja wao alichepukia pembeni kidogo kuja kuangalia kama anaweza kujipatia "ka-usafiri" ka-Hammer II au Cadillac ambako "hakakuwa" ka bei ndogo. Huyo ndugu alikuwa anafanyia kazi "kabajeti kake" ka dola elfu chache. Sasa sijui kama alikuwa anatania au alikuwa "very serious".

Wasafari wanaoambatana na Rais kwa hakika ni lazima na wenyewe "waambulie" kidogo. Mojawapo ya safari zake Rais Kikwete aliambatana na watu karibu 30 (sina uhakika msafara wa kawaida huwa na maafisa wa ngapi), lakini kwa Rais wa nchi ya daraja la tatu, na ambayo licha ya kelele za viongozi wake bado haijaanza kupaa, inasikitisha kuwa tunatumia fedha nyingi katika misafara hii. Nina uhakika kabisa endapo safari za viongozi wote kwenda nje ya nchi zikifanyiwa hesabu bila ya shaka jumla yake itatushangaza.

Sitoshangaa kabisa kuwa tukijumlisha fedha zilizotumika katika safari za Rais, Makamu, Waziri Mkuu na Mawaziri wengine kwenda nje ya nchi kwa miaka iliyopita, madarasa mengi tu ya shule za sekondari na zahanati vingejengwa, na wananchi husika wasingelazimika kuchangia!

Leo hii tunahangaika kuchangisha fedha za kujenga madarasa jijini Dar-es-Salaam. Hivi safari moja ya Rais inaweza kujenga madarasa mangapi? Je msafara mmoja wa Makamu wa Rais au Waziri Mkuu unaweza kusaidia kujenga vyoo vingapi vyenye maji katika shule ya Azania? Je ile misafara ya watetezi wa bajeti walioenda mikoani ingeweza kuweka mapaa mazuri na kununua vifaa vingapi vya zahanati?

Binafsi, naamini kabisa tunaweza kupima mafanikio ya ziara hizo kwa kuangalia hesabu nyepesi. Endapo misaada ambayo tumeahidiwa katika ziara za viongozi wetu pamoja na uwekezaji ambao umefuatia ziara hizo unazidi kwa kiasi kikubwa gharama za kuwasafirisha kina Vasco da Gama wa kileo, basi, taifa linakuwa limepata faida.

Hata hivyo endapo misaada hiyo na uwekezaji huo hauzidi gharama zilizotumika kuitafutia, basi, Watanzania hatunufaikinazo. Na hapa sizungumzii misaada na ahadi zote, ila ile tu ambayo "bila ya ziara za viongozi" isingewezekana.

Leo hii kuwaaimbia wimbo wa uwekezaji Wamarekani na Waingereza ni kama kurudia kibwagizo kile kile kwa kwaya yako. Wamarekani wangekuwa wanavutiwa na Tanzania wangeshaanza kuwekeza muda mrefu uliopita. Siyo kwa sababu hawajui; ni kwa sababu Tanzania haina maslahi makubwa kwa Wamarekani.

Urafiki na Marekani kimsingi unatokana na maslahi na hata wanapommwagia sifa rais wetu na kumpamba kwa pambio na maua tujue kuwa wanafanya hivyo kwa sababu moja tu; Rais wetu anakidhi maslahi yao katika eneo la Afrika ya Mashariki na hasa katika maslahi ya Marekani ulimwenguni.

Kitu ambacho mimi, na bila ya shaka wachambuzi wengine, tumeanza kukiona ni kuwa Marekani inaanza kuvutiwa na Tanzania siyo kwa sababu za kiuchumi hasa bali kwa sababu za kiusalama. Ndio maana wapo wale ambao tunaamini kuwa ziara hii ya Rais Kikwete Marekani inahusiana kabisa na maslahi ya kiusalama ya Marekani. Siamini hata kidogo kuwa Rais wetu anafunga safari kwenda Marekani kusimama kwenye kipaza sauti kutangaza mkutano wa Sullivan na kurudi!

Ni matumaini ya Watanzania kuwa mwaka ujao Rais Kikwete atautumia kukaa nyumbani na watu wake na ataanza kuwaamini viongozi wengine kuwa wanaweza kumwakilisha nje ya nchi vizuri kabisa. Watanzania watapata moyo mkubwa endapo Rais Kikwete ataweza kukaa nchini kwa miezi mitatu mfululizo.

Rais Kikwete na timu yake hawana budi kukaa chini na kuamua kwa umakini mkubwa ni safari gani za msingi na za lazima ambazo zinamuhitaji Rais. Vinginevyo, Rais wetu ataonekana ni Rais msafiri hasa ukimlinganisha na marais jirani zetu. Inakuwaje watu kama kina Kibaki, Kagame, Museveni, Kabila na wengine majirani wanakaa nchini mwao na wanaenda mara moja moja huko ng'ambo, isipokuwa wa kwetu?

Nafahamu kuwa serikali imekuwa ikirudia kusema kuwa Rais hafanyi kazi kwa shinikizo la mtu yeyote. Ukweli ni kuwa isingekuwa wahisani kumpa shinikizo au kuweka shinikizo kwa serikali yetu kuna mambo ambayo yasingefanyika. Uchunguzi wa Richmond, BoT, na mikataba haukutokana na shinikizo la wapinzani kama wao wanavyopenda kudhania. Serikali ya CCM haioni tishio lolote la msingi toka vyama vya upinzani, tishio pekee ambalo CCM wanalihofia ni kutoka kwa wahisani.

Wahisani wakitaka Rada ichunguzwe itachunguzwa na wakitaka Richmond ichunguzwe itachunguzwa. Na ni wahisani ambao wakitaka sheria ya rushwa ipitishwe itapitishwa na nina uhakika kama wakitaka Katiba yetu ifanyiwe marekebisho ya msingi itarekebishwa. Sasa tusifike mahali wahisani wakamwambia Rais wetu apunguze safari za nje!
 
LOL!...Wahisani wamtaka Rais wa Tanzania apunguze kuwatembelea, maana wamechoka na ugeni wake kila kukicha....hii itakuwa siyo ya mwaka bali ni ya karne....:) au akifika wenyeji wanamwambia hatupo au tuko busy na mambo mengine hivyo hatuwezi kuonana na wewe...:)
 
Mh.Keil Kuna mambo mengi kuhusu masuala ya Serikali ya Tanzania na US.Kwa wale walio karibu na Rais wanadai mambo yamebadilika sana kwenye Ofisi hiyo,Mambo mengi yanafanywa kwa siri kubwa sasa,baada ya kuonekana kila kitu kinakuwa Nje mapema,kuna Utaratibu unaoandaliwa wa kupewa utaratibu (Ratiba) wa/ya Rais na Msemaji wa Ikulu.Utaratibu huo Utaanza mapema Mwakani.

Masuala ya Tanzania na US yanawezekana kabisa yanagusa mambo hayo ya Usalama na kuna habari kuwa Rais Bush atatembelea Tanzania mapema Mwakani (Habari hazijathibitishwa).Ziara za mara kwa mara za Kiongozi wetu huko US na Ujio wa mara kwa mara wa delegations kutoka US kuna uwezekano kuna kubwa linalojadiliwa.
 
Hii makala ni nzuri na inatoa changamoto, nina wasiwasi na huyu raia mwema kama ataweza kusurvive na hizi articke za namna hii.
 
Mh.Keil Kuna mambo mengi kuhusu masuala ya Serikali ya Tanzania na US.Kwa wale walio karibu na Rais wanadai mambo yamebadilika sana kwenye Ofisi hiyo,Mambo mengi yanafanywa kwa siri kubwa sasa,baada ya kuonekana kila kitu kinakuwa Nje mapema,kuna Utaratibu unaoandaliwa wa kupewa utaratibu (Ratiba) wa/ya Rais na Msemaji wa Ikulu.Utaratibu huo Utaanza mapema Mwakani.

Masuala ya Tanzania na US yanawezekana kabisa yanagusa mambo hayo ya Usalama na kuna habari kuwa Rais Bush atatembelea Tanzania mapema Mwakani (Habari hazijathibitishwa).Ziara za mara kwa mara za Kiongozi wetu huko US na Ujio wa mara kwa mara wa delegations kutoka US kuna uwezekano kuna kubwa linalojadiliwa.

Ni kweli Mwawado, hata mimi habari za ziara ya Bush Tanzania nimezipata na kuna uwezekano mkubwa wa kuja huko au nchi isiyotajwa ya Afrika mashariki na Kati.

Hili swala la kambi waliweke tu wazi kwani muda si mrefu kila mtu atajua na ni vizuri wakakubali na wakaanza spinning positive spinning sasa hivi.
 
Hii makala ni nzuri na inatoa changamoto, nina wasiwasi na huyu raia mwema kama ataweza kusurvive na hizi articke za namna hii.

Kasana,
Pia nimesoma Raia Mwema ya wiki hii- ni moto kweli! Sijui kama serikali itaweza kuwavumilia.
 
MzalendoHalisi na Kasana:
Ni kwa vipi serikali isiweze kuwavumilia, ali mradi hawavunji sheria yoyote?

Kumbuka wanashinikizwa kufuata "Utawala Bora", hawana hiari yao itakayowafanya wafanye vinginevyo. Wakifungia RaiaMwema - wafadhiri na wengineo wanaotuendeshea serikali yetu unadhani watayakubali hayo?

Halafu mnasahau watawala wanavyopenda kusifiwa, ni nani atakubali kuchafuliwa sifa hizo, eti kwa kufungia kigazeti. Sana sana watajitahidi kuwanunua hao waandishi wanaoonyesha kidomodomo, lakini sio kuwafungia au kuwatia misukosuko.
 
Makala nzuri, ila economy of words is crucial.Sometimes I get the feeling that the article is overly long winded and some analogies are shallow.
 
Ndio sababu katika makala zilizopita tulikokotoa cost benefit analysis za ziara hizi. Tuambiwe kinagaubaga mafanikio, sio kwenda kuomba misaada.
Tushachoka kufundisha!
 
Lula wa Ndali-Mwananzela mpe vidonge vyake fisadi huyo.
 
Ni kweli Mwawado, hata mimi habari za ziara ya Bush Tanzania nimezipata na kuna uwezekano mkubwa wa kuja huko au nchi isiyotajwa ya Afrika mashariki na Kati.

Hili swala la kambi waliweke tu wazi kwani muda si mrefu kila mtu atajua na ni vizuri wakakubali na wakaanza spinning positive spinning sasa hivi.

Je, Watanzania watampokea kichaka kwa mikono miwili? au itakuwa tafrani mtindo mmoja kufuatia sera zake mbali mbali zinazopingwa kila kona ya dunia ikiwemo Tanzania? Je, itabidi FFU kumwagwa kila kona ili kupunguza tafrani hizo?
 
kwani hata kama kuna jambo linalozungumzwa hawawezi kulijadili kupitia njia nyingine za kitechnolojia kama simu au email? ni lazima jamaa apande ndege kila wanapotaka kuongelea hilo suala nyeti?
 
kwani hata kama kuna jambo linalozungumzwa hawawezi kulijadili kupitia njia nyingine za kitechnolojia kama simu au email? ni lazima jamaa apande ndege kila wanapotaka kuongelea hilo suala nyeti?

Hapo ndipo ninapo shangaa na kushangauka,

Hata kama kweli wanataka weka kambi yao bongo, kwani sisi ndio wenye shida mpaka raisi wetu akimbie kimbie kama vile yeye ndo mwenye uhitaji? kama wao ndo wanaomba nafasi kwanini basi wasije wao? ama ndo yale yale tumegeuka kahaba twakimbia kujiuza wenyewe??
 
KUna siku nilisema raia mwema inaelekea wanatoa habari JF, kuna mtu akasema inaweza kuwa ni kinyume chake. Lakini hii ni wazi kuna habari wanatoa JF.

Itabidi waanze kutoa reference ya JF pia. Hili la Vasco Dagama limeanza JF miezi na miezi kabla ya Raia Mwema.

Any way kwa JF ni jambo jema kama mawazo ya hapa yanaanza kusambazwa kwingineko.
 
Very true.. nadhani tuna network kubwa kuliko tunavyofikiria. Nakumbuka hata Majira wamedokoa baadhi ya ripoti humu..
 
Kutokana na kauli iliyotolewa na SADC sidhani kama Tanzania ina mpango wa siri wa kuweka USA base kwani itakuwa balaa kubwa sana.
 
Kutokana na kauli iliyotolewa na SADC sidhani kama Tanzania ina mpango wa siri wa kuweka USA base kwani itakuwa balaa kubwa sana.

Tusubiri tuone ... maana lisemwalo lipo na kama halipo linakuja. Mwisho wa siku haya yote yatajulikana. Sina imani sana na viongozi wa Afrika maana wengi huwa nina hisi wana unafiki fulani. Usije ukashangaa hao viongozi wa SADC ukakuta wameufyata pindi polisi wa dunia atakaoweka kambi hapo kwetu!!!
 
Hivi safari za masafa ni nani zaidi?

1. Vasco da Gama 2. Christopher Columbus 3. Marko Polo

Ingawaje wote walienda sehemu mbali mbali- masafa makali zaidi naona ni yale ya ardhini ya Marko Polo aliyepasua nchi hadi India na China! Hawa da Gama na Columbus wao walipita majini! JK alingalishwe na nani hati ya hao watatu?
 
Hi wote Wanablog,
Hauwezi kulinganisha Iran na Marekani.Marekani wanainfluence katika dunia na ndio maana wazee wanakwenda wenyewe.Ni mara ngapi Rais Mkapa aliwah kumtuma mwakilishi kwenda Marekani?Hivi ni vitu vya kuangalia.Usiangalie Tanzania tu angalia na nchi nyingine kama Pakistan aliyekuwa swahiba mkubwa wa Taliban lakin Marekani alipoomba support ya kuwapiga Watalibu Musharaff aliitikia haraka sana.Wazee wanataka acceptance kutoka kwa bwana Misitu.
Si kweli kuwa anaweza akaenda wenyeji wakamwambia tuko BUSY au kisingizio kingine. Ziara za viongozi wakubwa zinaandaliwa na mabalozi baada ya kuafikiana na serikali husika na ndipo viongozi wanakwenda hivyo usitegemee ata siku moja kiongozi akaambiwa mambo kama hayo.Inawezekana Marekani nao wanainterest na ndio maana wanamwalika mara kwa mara.
Ahsanteni
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom