JK awa Vasco da Gama ... Makala ya Raia Mwema

Hi wote Wanablog,
Hauwezi kulinganisha Iran na Marekani.Marekani wanainfluence katika dunia na ndio maana wazee wanakwenda wenyewe.Ni mara ngapi Rais Mkapa aliwah kumtuma mwakilishi kwenda Marekani?Hivi ni vitu vya kuangalia.Usiangalie Tanzania tu angalia na nchi nyingine kama Pakistan aliyekuwa swahiba mkubwa wa Taliban lakin Marekani alipoomba support ya kuwapiga Watalibu Musharaff aliitikia haraka sana.Wazee wanataka acceptance kutoka kwa bwana Misitu.
Si kweli kuwa anaweza akaenda wenyeji wakamwambia tuko BUSY au kisingizio kingine. Ziara za viongozi wakubwa zinaandaliwa na mabalozi baada ya kuafikiana na serikali husika na ndipo viongozi wanakwenda hivyo usitegemee ata siku moja kiongozi akaambiwa mambo kama hayo.Inawezekana Marekani nao wanainterest na ndio maana wanamwalika mara kwa mara.
Ahsanteni

Hata yeye mwenyewe alipoulizwa (kwenye mahojiano na BBC nadhani) kuhusu mfululizo wa safari zake si alijibu "ukiitwa na wakubwa kama hawa utakataa?"
 
Awe tayari kuuandika uvumbuzi wake kwani Vasco Da Gama aliandika kile alichokutana nacho na alichoweza kuvumbua , na huyu wa kwetu aje na ripoti ya uvumbuzi wake.

Naona marekani wanataka kuweka base kwani jana balozi wa marekani alikuwa anakagua gwaride la JWTZ na kusema kuwa amekwenda kuangalia kikosi kitakachokuwa kinaenda Lebanon mwezi february mwakani.

Kama balozi wao anapewa heshima ya kukagua vikosi vyetu huu ni mpango kamaili kuwa tayari wako njia kuleta kambi hapa kwetu ngoja tunusenuse kwanza wakuu.
 
Yes. we once had Vasco dagama. Ila utashangaa waliochangia huu uzi....wako wanauliza kwa nini Magufuli hataki kusafiri! We live in interesting time indeed.
 
Back
Top Bottom