JK ateua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO

JK ateua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO

Jembe lililokuwa limebaki TANESCO, nadhani sasa wenye majenereta wayapeleke Sudan Kusini, Tz hakutakuwa na mgao tena wa kushinikizwa kuzima umeme ili majenereta yauzwe!

that iz hope against hopes,,,,,,,
 
Jamaa yuko vzr lkn siasa ndani ya tanesco ndio tatizo kubwa.......
 
Wakiteuliwaga huwa tunasifia weee baada ya miezi michache tunaanza kulalamika kwamba ukoo wa panya unaendelea..

Kuongoza Tanesco, TRA, TPA na BOT ni kazi kubwa sana kuliko taasisi yoyote nchi hii..

Naomba mods hii thread muiweke strictly ili tuwakumbushe watu miezi sita ijayo waliokuwa wanamsifia jamaa jembe wanasemaje..

Hata JK alipopewa urais watu tulishangilia zaidi ya hivi lakini tumeona balaa lake..

Tanesco alieimudu alikuwa IDRISA RASHID sababu hakutaka Siasa Tanesco na serikali ilimgwaya sana,,japokuwa nae alikuwa kafisadi lakini kazi ya u CEO anaiweza vibaya mno,, toka enzi yupo BOT gavana wa Bank BOT haikutetereka na hata Tanesco aliijenga sana, lakini baada ya huyo UKOO wa panya unabadilishana tu ulaji
 
Shirika la ovyo sana, JK ni moja ya watu walioliangamiza kwa kuingia mkataba wa kifisadi na IPTL, akiwa ni waziri wa nishat na madini,

Mkuu, unaweza kutuwekea tuhuma za ufisadi za JK, kama ambavyo ilitajwa na Dr. Slaa pale mwembe yanga temeke?

Mkurugezi aanzie na hapo, kisha ashushe gharama za bei ya umeme.

Mkuu acha kujitoa ufahamu, ni nani asiejua mbinu za Rostam kuwachomoa wanasheria wa voda na kuwachomeka tanesco, kuanzia enzi za Ngeleja, haya kamchomeka mwingine tena huko tanesco. ..Na asiejua uswahiba wa JK na huyu mwarabu ni nani...
 
Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.

Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.

Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.

Mhandisi Felchelsmi mramba unamjua?
 
Mungu ampe nguvu ya kuwakumbuka walalahoi wanaochechemea kwa ukali wa maisha

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Kama huyu jamaa aliyeteuliwa hapendwi na Mstaafu Gen.Mboma basi atakuwa mtu safi kwani huyu mzee askari mstaafu ni fisadi aliyekubuhu sana; mahela yote aliyokwapua akiwa jeshini ameficha Uswisi na wakina Kikwete wanaogopa kuyarudisha!!! Mboma ni zaidi ya yule aliyepelekwa kuwa balozi China kwa ufisadi!!!!

Felichesmi Mramba ameokoka, ni mzee wa Kanisa la TAG Ubungo. Wakati mwingine husimama madhabahuni kuhubiri. Hivyo naamini ni mtu safi, ana msimamo, kwa hivyo kama Gen Mboma ni fisadi, watatofautiana sana kimtazamo.
 
Eng Mramba amekuwa kaimu wa nafasi hiyo kwa mda mrefu tangu alipofukuzwa kazi Eng Mhando,

Ninamfahamu vizuri na ni rafiki yangu wa karibu, uzuri zaidi nikuwa jamaa ni mtu wa kiroho yani ni mlokole halisi asiyependa njia za mkato, Amekumbana na urasimu wa wanabodi wakiongozwa na Gen Mboma hasa wakishinikiza ishu za dowansi lakini wameshindwa na sasa tanesco imeongezw ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 12 kwa siku hadi 50milioni kwa siku, haya ni mafanikio makubwa kwake.

Kwa utendaji na uadilifu sina hofu nae labda abadilike baada ya kukabidhiwa kiti rasmi,
maombi yaanzie hapa
 
Ila wadau,tatozo c Mkurugenz wa Tanesco,tatizo ni hao wanaompendekeza na kumchagu,,,,,,wanakuwa na ajenda zao,ila zinapofanyiwa kazi mzgo humuangukia mkurugenz wa Tanesco,,,,,,,
 
Eng Mramba amekuwa kaimu wa nafasi hiyo kwa mda mrefu tangu alipofukuzwa kazi Eng Mhando,

Ninamfahamu vizuri na ni rafiki yangu wa karibu, uzuri zaidi nikuwa jamaa ni mtu wa kiroho yani ni mlokole halisi asiyependa njia za mkato, Amekumbana na urasimu wa wanabodi wakiongozwa na Gen Mboma hasa wakishinikiza ishu za dowansi lakini wameshindwa na sasa tanesco imeongezw ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 12 kwa siku hadi 50milioni kwa siku, haya ni mafanikio makubwa kwake.

Kwa utendaji na uadilifu sina hofu nae labda abadilike baada ya kukabidhiwa kiti rasmi,

Ni ukoo wa Mramba money two???!!!!
 
Rais Kikwete jioni hii amemtangaza rasmi Mhandisi felchesmi mramba kuwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco uteuzi ambao umeanza rasmi leo hii

Hivi Mramba amekuwa mhandisi lini? Alimaliza BA pale Chuo 1995, uhandisi una misingi yake na sijui kama kufanyia Tanesco muda mrefu mtu anweza kujiendeleza hadi akwa mhandisi kamili?
 
Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.

Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.

Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.

Uliwahi kumuhonga Bw. Njombe akakataa? Kwani kwa kawaida watumishi wa umma husaidia [hupendelea] watu wa makabila yao? Na je hayo ndiyo matarajio ya wananchi wa makabila mbalimbali re. mtu wa kabila lako katika ofisi ya umma atakusaidia/atakupendelea? Na unataka wasomaji wa ujumbe wako tuamini kwamba Bw. Njombe ana sifa za kuwa mtendaji mkuu wa TANESCO kuliko Bw. Mramba? Au ulitegemea tu Bw. Njombe ateuliwe? I think you are making rather a too general statement to be taken seriously. Na kwanini hawa wakuu wa mashirika wanateuliwa? Kwanini wasishindanishwe na mwenye kushinda apewe kazi ya kuongoza shirika. Uteuzi siku zote unazingatia value judgment na hivyo kwa asili ni biased.
 
YerikoNyerere ile capacity charge ya IPTL na DOWANS Tshs 150,000,000/" kwa siku bado ipo???
Shirika linazama kwa ufisadi!!!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom