Eng Mramba anachukia rushwa ndiyo sababu Gen Mboma anamgwaya. Hii ni moja ya teuzi chache makini msanii Kikwete alizowahi fanya. Hongera FelchismHuyu Eng. Mramba ni mtu makini na asiyehongeka kirahisi (kwa kumbukumbu zangu za nyuma.). Nina furahi kusikia kwamba hata Eng. boniface njombe ni mtu wa kaliba hiyo hiyo. Labda jambo la kujiuliza hapa ni , Je hawa watu wataruhusiwa kufanyakazi kwa kuzingatia weledi wao? Je hawa watu watawezeshwa kufikia malengo ya shirika? Ningeomba yeyote mwenye taarifa za zaidi kuhusu huyu Eng. Mramba aziweke hapa.
Ukisoma Mwanahalisi....oh sorry.. Mawio la last week linaeleza kuwa huyu jamaa yupo katika mgogoro na mwenyekiti wa bodi ya Tanesco Jenerali mst Robert mboma ambapo mboma anasema jamaa anatakiwa kuachia ngazi lakini anatetewa na katibu mkuu wa nishati bw maswi. Tafuta Mawio la last week lina habari ya kina ya huyu mtu
Labda kwa mengine ila kwa ubadhirifu huyu jamaa ninamjua kuwa sio mbadhirifu kabisa maana ni mtumishi wa Mungu aliyetukuka... labda abadilike. Nimewahi kuwa nae kwenye kanisa moja la Assemblies of God(TAG) na kwa kwa kweli si wa kumtilia shaka uaminifu wake ... naamini kwa hapa mafisadi walie tu..Rais Kikwete jioni hii amemtangaza rasmi Mhandisi felchesmi mramba kuwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco uteuzi ambao umeanza rasmi leo hii
For sure, I admire this guy. Humble,servant of God,kwa kweli taifa linahitaji watu safi kama huyu... bahati mbaya tu ni huu mfumo wa serikali badhirifu ya ccm,nakuombea Ndugu Mramba uyashinde mabaya yote....Hongera Mate Wa Kibaha Secondary Eng Felchism Mramba uadilifu wako ni Tunu kwa TANESCO na Taifa. Umefata nyayo za Dr Kazaura Kamugisha Dir General TTCL. I'm proud of you guys.
Mkuu umenena vema sana,the guy is a man of God.Eng Mramba amekuwa kaimu wa nafasi hiyo kwa mda mrefu tangu alipofukuzwa kazi Eng Mhando,
Ninamfahamu vizuri na ni rafiki yangu wa karibu, uzuri zaidi nikuwa jamaa ni mtu wa kiroho yani ni mlokole halisi asiyependa njia za mkato, Amekumbana na urasimu wa wanabodi wakiongozwa na Gen Mboma hasa wakishinikiza ishu za dowansi lakini wameshindwa na sasa tanesco imeongezw ukusanyaji wa mapato kutoka milioni 12 kwa siku hadi 50milioni kwa siku, haya ni mafanikio makubwa kwake.
Kwa utendaji na uadilifu sina hofu nae labda abadilike baada ya kukabidhiwa kiti rasmi,
Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.
Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.
Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.
Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.
Tutatumia vibatari
Ni ndg na yule mwizi P. Mranba mwenye kesi mahakamani?
Kwaheri Tanesco, tukutane Karimjee kwenye kukuaga. Bado nina kumbukumbu mbaya ya jina hili na yule aliyetuahidi kula nyasi