cha kwanza ni kuondoa mchezo wa kuwapa watu kazi ya kuzisambaza nguzo za umeme,kwanini Tanesco wenyewe wasifanye kazi hiyo? inakuwaje unampa mtu kazi ya kuiuzia Tanesco nguzo tena nguzo hizo zinatoka njombe,zinapelekwa SA na kurudishwa Tanzania na kuuzwa kwa bei kubwa.lakini pia niwakati sasa wa Tanesco kuachana na utumiaji wa nguzo za miti,ni vyema wakatumia nguzo zinazotenezwa na cement,hii inafanyika china na majirani zake,ukitumia nguzo za aina hii,huitaji kubadilisha kila wakati,huitaji kuogopa moto na zinadumu kwa muda mrefu.tatizo la vishoka Tanesco limekuwa kubwa sana,ni wakati sasa wa eng huyu mramba kupambana nalo,ni vyema tanesco wakawaeleza wananchi ufikapo tanesco nani anahusika na nini na mafundi wao wapewe vitamburisho vitakavyo weza kufanya watu kuwatambua wafanyakazi wa TANESCO bila shida