JK ateua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO

JK ateua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO

Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.

Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.

Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.

Atakuwa ni Mbena huyo, wabena ndivyo walivyo hawana undugu.
 
Wachaga hawaepukiki kwani kila uendako utawaona. Jamaa atakuwa ameshapata gari jipya la kwenda kutesa nalo kwenye matambiko mwezi huu. Ataongeza msafala wa magari kwenda Moshi.
 
Rais Kikwete jioni hii amemtangaza rasmi Mhandisi felchesmi mramba kuwa mkurugenzi mtendaji wa Tanesco uteuzi ambao umeanza rasmi leo hii
sasa mh. tulifikili unaondoa ukabila Tanesco kumbe unauwendeleza? huyu mtu hatari sana kwa kuvuta ndugu zake, ok basi ngoja naye tumwangalie ila chonde chonde lazima uweke misingi imala ambayo itakufanya ukumbukwe na Watanzania kama baadhi ya wizara ikiwemo hiyo, waziri safi sana ulicheza ila mramba sijui?
 
Kanunue kibatari ndugu yangu ukileta ubishi mafuta ya taa nayo wanapandisha.
Ungejua nilipo hata usingeandika ulioandika hapa. Nina miaka zaidi ya nane sijui kitu kinaitwa kukatika umeme huku. Poleni kama bado uko kwenye nchi ya kijuha hiyo.
 
Yaani wewe n akili zako timamu unaishi kwa kuamini maneno ya Slaa?
Bora mimi ninayeamini maneno ya Rais wetu. Kigoma itakuwa kama Dubai na Mwanza itakuwa kama California by 2015!!!
 
Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.

Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.

Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.

Mteue wewe basi.
 
Kuhusu nguzo za cement, kweli ni imara sana. Niliwahi kuona nguzo hizo kule mkoani Tanga. Bahati mbaya wezi wamebomoa nguzo hizo na kuiba nondo zote zilizotumika kujenga nguzo husika. Zinafaa sana labda tu gharama za kutengeneza hizo concrete poles inasemekana ni aghali sana.

Nadhani watu bado hawajajiuliza bei ya hizi nguzo za cement...kwanza nguzo moja ya LV ni not less than 1025usd na nguzo moja ya HT ni not less than 1400usd ambapo kiukweli uchumi wetu hauwezi kuhimili....infact life span ya nguzo za mbao ni 25years while ile ya cement ni lifetime warranty ya not less than 99years....ukweli unarudi pale pale,hii cost nani abebe na kwa uchumi upi wa bongo hii ambayo domestic electricity revenue ni hasara tupu,tanesco inafanya purely hasara tupu kwa umeme wa majumbani.....ndio wanataka kununua hivi sasa as tenda ipo out already ila patakua pagumu sana kwani ni uwekezaji very heavy atleast serikali iwekeze kwenye huu muundo mbinu,itawekeza sasa ndio swali,na hela inatoka wapiiii?domestic customer wa kibongo hawezi kabisaaaa.
 
Labda kwa mengine ila kwa ubadhirifu huyu jamaa ninamjua kuwa sio mbadhirifu kabisa maana ni mtumishi wa Mungu aliyetukuka... labda abadilike. Nimewahi kuwa nae kwenye kanisa moja la Assemblies of God(TAG) na kwa kwa kweli si wa kumtilia shaka uaminifu wake ... naamini kwa hapa mafisadi walie tu..

Kwangu mie nikisikia jina Mramba basi kichwani huja picha ya mnuso wa Alex Stewart
 
Jamani ni nini hii?
Nilitegemea amteue Mhandisi Boniface Njombe kuwa Mkurugenzi Mtendaji.

Jamaa huyu anatisha kwa utendaji na ni mtu wa principles maishani mwake.

Hahongeki, hasaundiki, anachojua yeye ni kazi, haki bin haki. Kuna wakati alifanya kazi mkoa fulani, wa kabila lake wakadhani atawasaidia na matatizo yao, aliwaacha hoi na kuwatimulia vumbi akiwabana na taratibu za utumishi wa umma.

Lakini anyway, penye miti hapana wajenzi.

Mkuu kama unatarajia watendaju wazuri ndio watakaopata uteuzi kwa serikali hii ya Kikwete unakosea. Hapa wanateuliwa wapiga dili...
 
Nadhani watu bado hawajajiuliza bei ya hizi nguzo za cement...kwanza nguzo moja ya LV ni not less than 1025usd na nguzo moja ya HT ni not less than 1400usd ambapo kiukweli uchumi wetu hauwezi kuhimili....infact life span ya nguzo za mbao ni 25years while ile ya cement ni lifetime warranty ya not less than 99years....ukweli unarudi pale pale,hii cost nani abebe na kwa uchumi upi wa bongo hii ambayo domestic electricity revenue ni hasara tupu,tanesco inafanya purely hasara tupu kwa umeme wa majumbani.....ndio wanataka kununua hivi sasa as tenda ipo out already ila patakua pagumu sana kwani ni uwekezaji very heavy atleast serikali iwekeze kwenye huu muundo mbinu,itawekeza sasa ndio swali,na hela inatoka wapiiii?domestic customer wa kibongo hawezi kabisaaaa.

Hazijabuniwa za plastic mkuu?... Au plastic alafu ndani ziwe hollow zijazwe zege... I thnk hazitakuwa expensive hivyo...
 
Hazijabuniwa za plastic mkuu?... Au plastic alafu ndani ziwe hollow zijazwe zege... I thnk hazitakuwa expensive hivyo...

Sasa mkuu hiyo plastic hollow halafu uweke zege hiyo nguzo itapata streghth wapi ya kubeba tension ya cable?concrete poles zinakua reinforced na nondo tena zilizosukwa vizuri sana ziwe na pawa ya kubeba mzigo,sasa zege tupu bila nondo nje una cover na plastic ni waste of time nguzo itakua weak sana...hata useme uweke nondo halafu uje tena u add plastic nje tena itakua even more expensive......nguzo haiwi reinforced na plastic nje hata siku moja,itakua sio nguzo,itakua ni bomba la plastic lililojazwa mchanga ndani
 
huyu mramba siyo yule yule mramba jamani? kwani hakuna watu wengine ambao hata majina ya wazazi wao sio makubwa wanaoweza hizi kazi nao wakapewa nafasi jamani?:bored:

Hana undugu wala uhusiano wowote na pesa2, ni majina tu yanafanana..
 
Acha kutumia data za vijiweni. Kama hujui uliza. Mramba kafanya B.Sc. in Electrical Engineering na alimaliza 1996 - UDSM - Faculty of Engineering (FoE) kama ilivyokuwa inaitwa wakati huo. Alirudi kufanya MBA baadaye.

Sawa mkuu, ni za vijiweni, mnatubishie hata sie tuliosoma naye? na kabla ya kuwa Kaimu Mkurugenzi alikuwa anafanya kazi gani?
 
Uliwahi kumuhonga Bw. Njombe akakataa? Kwani kwa kawaida watumishi wa umma husaidia [hupendelea] watu wa makabila yao? Na je hayo ndiyo matarajio ya wananchi wa makabila mbalimbali re. mtu wa kabila lako katika ofisi ya umma atakusaidia/atakupendelea? Na unataka wasomaji wa ujumbe wako tuamini kwamba Bw. Njombe ana sifa za kuwa mtendaji mkuu wa TANESCO kuliko Bw. Mramba? Au ulitegemea tu Bw. Njombe ateuliwe? I think you are making rather a too general statement to be taken seriously. Na kwanini hawa wakuu wa mashirika wanateuliwa? Kwanini wasishindanishwe na mwenye kushinda apewe kazi ya kuongoza shirika. Uteuzi siku zote unazingatia value judgment na hivyo kwa asili ni biased.

Point of correction; hii nafasi ilishindanishwa kwa interview, so I guess mramba aliwa-outdo wengine
 
rais kikwete jioni hii amemtangaza rasmi mhandisi felchesmi mramba kuwa mkurugenzi mtendaji wa tanesco uteuzi ambao umeanza rasmi leo hii

hongera kwa uteuzi wako kuwa mkurugenzi wa tanesco , nakutakia kila la kheri na mungu akuongoze katika kutatua changamoto zilizopo tanesco moja ni kupanda kwa bei ya umeme na upatikanaji wake.
 
Sawa mkuu, ni za vijiweni, mnatubishie hata sie tuliosoma naye? na kabla ya kuwa Kaimu Mkurugenzi alikuwa anafanya kazi gani?

Jamani muwe mnafanya utafiti kidogo kabla yakupost, Eng Mramba ni Electrical Engineer na kabla yakukaimu alikuwa deputy managing director distribution, ambapo mameneja wote wa kanda na mikoa waliripoti kwake ikiwa ni pamoja na makao makuu. Ndipo alopoteuliwa Mwaka jana kukaimu ukurugenzi mkuu..
 
Back
Top Bottom