JK apaa tena

Rais wetu JK yupo busy sana na mambo ya nje kuliko ya nyumbani......hapa nyumbani hatulii kabisa ndo maana mafisadi wanapumua na kujiimarisha zaidi na zaidi......kwa kupaa paa hivi sijui kama hawa mafisadi atawaweza wengine anapaa nao huko huko anako elekea.

Ukiwa makini utagundua au utaelewa kwamba kazi kubwa ni ya waziri mkuu,,, sio ya Rais....

Tulishajadili kwamba Rais wa Tanzania... ana mambo makubwa kwenye wizara hizi.

-Nje na Mahusiano ya Kitaifa
-Fedha
-Utumishi na Utawala Bora
-Ulinzi na Usalama....

Wizara zingine nyingi Waziri Mkuu ndiye mwenye kuziongoza kwa karibu zaidi... so there is no any harm for president to travel... ni part ya majukumu yake.

Ukitumia akili ndogo utajua kwamba Mswati alituletea fedha siku za karibuni kwa kukaa kwenye mbuga zetu... sio ustaarabu kutokwenda kumsalamia.
 
kwa wale msioelewa tafteni taarifa Raisi wa Botswana anasafiri mara ngapi kwa mwaka! Halafu linganisheni maendeleo ya Botswana na ya kwetu! Na mipango yao Baada ya Miaka 10 ijayo wanataka kufanya nini!
Kiufupi ni kuwa hatuna raisi! ivi unataka kuniambia atasoma lini report alizopewa?
 
Mkuu heshima mbele.
Hapo umenena kabisa watu mlio karibu na twakimu tunaomba mfatilie kwa umakini ziara za rais wa Botswana anasafiri mara ngapi kwa mwezi na kwa mwaka....kijuu juu Botswana wapo juu zaidi yetu Tanzania kiuchumi na huduma za jamii.Hii yote inatokana na uchapaji kazi wa Rais wao....sisi rais wetu atavunja record ya kusafiri sana Duniani itabidi baada ya muda wake wa uongozi hili tuliiingize kwenye kitabu cha Gueness...naamini atakuwa amevunja record.
 
Siyo lazma Rais wa nchi aitikie mwaliko wo wote anaweza akatuma viongozi wengine.Ya ndani yanamshinda ndiyo maana anona apoteze mawazo huko nje.
 
.... ivi unataka kuniambia atasoma lini report alizopewa?
Ripoti anazisoma akiwa safarini..kwani huko anapata muda mwingi wa kuzipitia...Safari si Mbaya kama anapata muda wa kujifunza mazuri walionayo wenzetu....Hata vasco Dagama hakuwa akitembea tu for leisure...Kama JK na Timu yake safari zao haziwasaidii kujifunza mazuri....hapo tena utakuwa mushkeli mkubwa!!!
 
Siyo lazma Rais wa nchi aitikie mwaliko wo wote anaweza akatuma viongozi wengine.Ya ndani yanamshinda ndiyo maana anona apoteze mawazo huko nje.

Eee bwana ndugu yangu mi naona hii siyo bure kuna haja ya kumtafuta mtaalamu wa miti shamba ili atuambie ni nani aliyemloga rais wetu lakini mimi nina wasiwasi na hawa mafisadi. KWANINI HATULII NYUMBANI?
 
Ukiwa na issue huna sababu ya kusafiri, wenyewe watakufuata. Angalia wanavyopigana vikumbo hapo Tripoli kwa mzee Muamar, ingawa walimuita gaidi na kumsakizia ushenzi mwingi tu, lakini leo hii hawaishi kwenda kwake.
 
Tripoli kuna mafuta ndio maana wanakwenda, hivi enzi za Mwalimu mbona hatukuwa na mafuta lakini walikuwa wanamfuata mpaka Butiama, hivi huyu mkulu hawezi kutulia Chalinze wakamfuata?

Sasa hivi anaingia NY, damn it!
 
Halafu anarudi tena US, after all this!

Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilipata nafasi ya kuwa mmoja wa watanzania tuliokutanishwa na balozi Ombeni Sefue, balozi wetu hapa Marekani katika kikao cha kuratibu uanzishwaji wa Diaspora Association of Tanzanians Abroad (DATA), kikao kilichofanyika Hilton Americas Hotel, Houston, Texas. Habari zaidi ya nini kitaendelea baada ya pale zitatolewa baadaye. Tulipata input nzuri tu toka kwa Bw. Ole Naiko (TIC), Bw. Dunstan Mrutu (Baraza la Biashara), Bw. Elvis Musiba (chamber of commerce), among others ... kamati maalum iliundwa ili kuratibu mambo ya chama hiki.

Anyways, nilichotaka kusema ni kwamba kitaitishwa kikao cha watanzania wote waishio Marekani siku ya uzinduzi wa hiki "chama", na Rais ndiye anategemewa kukizindua, hivyo atakuja Marekani, sijui itakuwa wapi exactly, ila itakuwa sometime in Novemba.
 
sioni ubaya JK kwenda Swaziland

Nchi inaendelea vizuri tuuu

Kweli Mkuu hakuna ubaya kwani alikwenda kuungana na maraisi wenzake katika sherehe kubwa yaani uhuru wa nchi na kuzaliwa kwa mfalme wao. lakini kumbuka unapokwenda huko huwezi kosa mbwembwe za Mswati au wanafamilia wake. Nilikuwa nikiangalia kwenye mtandao nilibaki midomo wazi.

Jionee mwenyewe huyu mtoto wa King Mswati akiwa anakwenda kuwasalimia marais wa nchi mbalimbali. Fungua hiyo doc ni picha bana, habari ndo hiyo!

"King Mswati III's first daughter, Princess Sikhanyiso, arrives at the Somhlolo Stadium on September 6, 2008 in Lobombo prior to celebrate the 40th anniversary of Swaziland's independence and his father's 40th birthday with dignitaries and Heads of States from Africa."
 
Attachments

  • King Mswati III.doc
    326 KB · Views: 96
Baada ya siku mbili kurejea kutoka kwenye mazishi ya Levy Mwanawasa......Rais wetu JK amepaa tena jana jioni kwa ndege ya serikali kwenda kwa Mfalme Mswati-Swaziland kuhudhulia sherehe za uhuru wa nchi hiyo pamoja na Birthday ya mfalme huyo ambaye anatimiza miaka 40 wao wanaita ni 40-40.Ambazo zitaligharimu taifa hilo $40 milion
Imethibitishwa kuwa akitoka huko anaunga moja kwa moja kwenye mkutano wa nchi za Afrika ...................

Tatizo lipo wapi jamani? Kama mtu ni raisi wa nchi na upande mwingine ni Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Africa sio kama kuna shida hapo unless unahoja mpya na ya msingi ambayo yeye haijui.
 
Halafu anarudi tena US, after all this!

Naona atahuthuria hapa......

The Africa Travel Association (ATA)
Presents
The 3rd Annual
PRESIDENTIAL FORUM ON TOURISM
Hosted by
New York University’s Africa House
Featuring
Visiting Heads of State from across Africa
On the occasion of the 63rd United Nations General Assembly Meeting
Showcasing
Destination Africa:Unleashing the Possibilities
Moderated by
Ali Velshi
CNN Senior Business Correspondent and Host of “Your $$$$$”
Friday, September 26, 2008
10:00 a.m. — 1:00 p.m.
Doors open & Registration begins at 9:15 a.m. Program starts promptly at 10:00 a.m.
New York University, Kimmel Center, Eisner and Lubin Auditorium
60 Washington Sq. South, 4th Fl. (Between La Guardia Pl. & Thompson St.)

Please RSVP online at http://africatravelassociation.org/ata/events/apft.html by Tuesday, Sept. 23

Call: +1.212.447.1357
www.africatravelassociation.org
 
Ijumaa na Jumamosi iliyopita nilipata nafasi ya kuwa mmoja wa watanzania tuliokutanishwa na balozi Ombeni Sefue, balozi wetu hapa Marekani katika kikao cha kuratibu uanzishwaji wa Diaspora Association of Tanzanians Abroad (DATA), kikao kilichofanyika Hilton Americas Hotel, Houston, Texas. Habari zaidi ya nini kitaendelea baada ya pale zitatolewa baadaye. Tulipata input nzuri tu toka kwa Bw. Ole Naiko (TIC), Bw. Dunstan Mrutu (Baraza la Biashara), Bw. Elvis Musiba (chamber of commerce), among others ... kamati maalum iliundwa ili kuratibu mambo ya chama hiki.

Anyways, nilichotaka kusema ni kwamba kitaitishwa kikao cha watanzania wote waishio Marekani siku ya uzinduzi wa hiki "chama", na Rais ndiye anategemewa kukizindua, hivyo atakuja Marekani, sijui itakuwa wapi exactly, ila itakuwa sometime in Novemba.

Mkuu kipunguni Heshima mbele kwa kuhudhuria kwako kikao cha DATA jumamosi ya Tarehe 06/sept'. huko Houston. kutakuwa na kikao kingine kama hicho huko Minneapolis Jumamosi ya tarehe 13/09 na Jumuiya ya Watanzania waishio huko wamekwishafahamishwa na Ubalozi.Balozi Sefue ndio atakuwa msemaji mkuu katika Mkutano huo,Balozi amekwishaonana na Watanzania waishio Washington DC na Washington Seattle (kwa wakati tofauti) kwa ajili ya kuunganisha watanzania waishio Marekani.Kama ulivyozungumza awali kuna juhudi za kukamilisha uundwaji wa DATA ili uzinduliwe na Rais Kikwete mwishoni mwa mwaka huu.

Juhudi hizi za kuunganisha Watanzania zimepamba moto kila pande ya Dunia sasa,baada ya mwanachama mwenzetu humu,kulifikisha wazo hilo Bungeni baada ya kufanya ziara na kuzungumza na watanzania waishio Michigan na Texas.Kuna Utaratibu unaandaliwa na wizara Husika ili kila Balozi iwe na Mtu anayeshughulikia Jumuiya za Watanzania katika Nchi husika.

Kwa Taarifa tu,Mkuu Sokoine aliyeko Ubalozi wetu DC anahamia Toronto Canada kuchukua nafasi ya Mama Msechu,ambaye anarudi/amerudi nyumbani kwa majukumu mengine wizarani.
 
Back
Top Bottom