JK apaa tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK apaa tena

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Fidel80, Sep 6, 2008.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Baada ya siku mbili kurejea kutoka kwenye mazishi ya Levy Mwanawasa......Rais wetu JK amepaa tena jana jioni kwa ndege ya serikali kwenda kwa Mfalme Mswati-Swaziland kuhudhulia sherehe za uhuru wa nchi hiyo pamoja na Birthday ya mfalme huyo ambaye anatimiza miaka 40 wao wanaita ni 40-40.Ambazo zitaligharimu taifa hilo $40 milion
  Imethibitishwa kuwa akitoka huko anaunga moja kwa moja kwenye mkutano wa nchi za Afrika ...................
   
 2. M

  Masatu JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Whats new here? hizi ni routine za kawaida za rais mna sensationalize mambo tu...
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Rais wetu JK yupo busy sana na mambo ya nje kuliko ya nyumbani......hapa nyumbani hatulii kabisa ndo maana mafisadi wanapumua na kujiimarisha zaidi na zaidi......kwa kupaa paa hivi sijui kama hawa mafisadi atawaweza wengine anapaa nao huko huko anako elekea.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu angalia gharama zinazo tumika watu wanalipwa kwa night wanapo kuwa na mkuu bado gharama za hotel na mambo mengine na mlolongo mrefu wa wapambe wanao ambatana na rais pamoja na wake zao.....
   
 5. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #5
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  .... Safari ya kwenda huko kwenye bethidei wala si ya kumlaumu, ni moja ya matukio katika maisha na anaungana na maRais wenzake kusherehekea. Hiyo ya Zambia nayo ilikuwa muhimu aende kwenye msiba.

  ..... Hata hiyo nyingine ya kwenda kwenye vikao vya AU ni muhimu awepo, isitoshe yeye ni mwenyekiti. Kama ni kikao cha dharura au kilichopangwa kinahitaji awepo.

  ..... Miye safari iliyonishangaza na kunighafirisha ni ile ya kwenda Marekani kujiombeleza dolla millioni 20 na kuanzisha mazungumzo eti ya kuendeleza mpira wa kikapu. Absolutely infuriating.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Lakini mkuu na hizi nyingine angalia muda alio enda marekani akatembeza bakuli kulee na sijui kama kweli hizi dollar kama kweli kapata au lah....lakini kuna safari ambazo anaweza akatuma wawakilishi kama waziri mkuu au kiongozi mwingine...tunaye makamu wa rais naye kwani hawezi kumwakilisha kwenye shughuli kama hii ya Swaziland?
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo unataka Rais ajifungie ndani kwa kuwa akienda nje kuna gharama za Hotel? International relations ni integral part katika maendeleo ya nchi yeyote. Chukulia mfano mdogo tu wa household. Hivi wewe katika familia yenu kukiwa na sherehe za harusi, kipaimara, arobaini etc utasema huendi kwa kuwa kuna gharama za kupanda mabasi nk?
   
  Last edited: Sep 6, 2008
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Sep 6, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kwani kuna kukata utepe kwenye sherehe za siku ya kuzaliwa?
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  ..........hakuna kukata utepe si ndo hapo ni misosi tu sasa sijui Mungwana kafunga au lah!na hiyo misosi itakuwaje?
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....muhimu: kama anaenda uswazi, watu wa protokali hakikisheni tu anaenda na mkewe maana huko ni noma noma tu.... handsomeboy na big smile yake hachelewi kutunikiwa ati!!
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  Halafu anarudi tena US, after all this!
   
 12. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #12
  Sep 6, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  The worst president ever.Nadhani sasa itabidi 2010 afanye kama mshikaji Putin na mwenzake yaaani Jk ampandishe Membe kuwa mkulu na yeye rudie mahali pake pa enzi Foreign Affairs minister na tutamtambua hatutamuita Vasco Da Gama tena
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 6, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mimi nimetoa thread hii watu wananilaumu kwa hiyo hizi ziara wao kwao wanaona sawa tu.....pigeni faida na hasara za ziara hizi amepaa USA zaidi ya mara 5 kutembeza bakuli nasikia tumeambulia $20milioni angalia gharama tulizo tumia GO and RETURN faida yake ni ipi?Kumwita Bush aje awekeze kwenye madini?atuibie tubaki na mashimo.....
  Rasimali tunazo kibaooooooo uongozi mbovu tunashindwa kuzitumia tusingekuwa tunahangaika hivi kutembeza bakuli kwa weupe........
   
 14. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #14
  Sep 6, 2008
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Aaah kama mtanashati anataka lake liwe litakuwa tu....Mai waifu wake atapewa kituo kimoja cha watoto yatima akatembelee wakati mtanashati anavinjari. Hicho wala sio kikwazo kabisaa.....
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....ebanaeeee!! ila namwonea donge true true miye.... maana 'vinyonyesho' atakavyo kumbana navyo vitakuwa vya kila aina....hadi vile vya rangi ya binzari eti..... udenda lazima umtoke, tuombee mfungo mwema umnusuru tu!! :D
   
 16. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #16
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  kwa hiyo unachotaka kusema ni kwamba kama watoto wako hawajui watakula nini jioni au mke wako hana hela za kulipia hospitali wewe utachukua tuu pesa na kulipa nauli ya daladala kwenda kwenye harusi au arobaini ya watu wengine???? kama hivyo ndivyo unavyomaanisha basi sina la kusema dhidi tuu ya kukubali kwamba watu tuna uwezo tofauti na siwezi kukulaumu kwa hilo kwani kwani hauwezi kufikiria juu ya hapo na hakuna kitu kinachoweza kufanyika zaidi ya kukuacha kama ulivyo.....
   
 17. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #17
  Sep 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini leo (Ijumaa, Septemba 5, 2008) mchana kwenda Swaziland na Sudan kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

  Akiwa nchini Swaziland kwa siku tatu, Rais Kikwete ambaye ameandamana na mkewe, Mama Salma Kikwete, atahudhuria sherehe mbili kubwa za kitaifa za miaka 40 ambazo zinajulikana kama "40th National Double Celebrations" nchini humo.

  Sherehe hizo ni miaka 40 ya kuzaliwa kwa Kiongozi wa nchi hiyo, Mfalme Mswati wa Tatu, na miaka 40 ya uhuru wa nchi hiyo kutoka kwa Waingereza. Sherehe zote mbili zinaangukia na kufanyika kesho, Jumamosi, Septemba 6, 2008.

  Rais amepangiwa kuondoka Swaziland keshokutwa, Jumapili, Septemba 7, 2008, kwenda Sudan ambako atafanya ziara nyingine ya kikazi.

  Akiwa Sudan, Rais Kikwete katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), atafanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Omar El Bashir. Rais anatarajiwa kurejea nyumbani Jumatatu, Septemba 8, 2008.

  Salva Rweyemamu,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.


  05 Septemba, 2008
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  he! kunani tena?
   
 19. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  huyu anazidi kwa aibu! hicyo huko ofisini hakuna kazi ya kufanya? hachoki au hapati air sickness?
   
 20. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Mmesahau kwamba riziki ya mbwa iko miguuni mwake na mgaa gaa na upwa hali wali mkavu? Au tembea tembea Mungu akuone?
   
Loading...