Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,250
- 44,578
- Thread starter
-
- #81
Tunakaa tunajadili UONGO uliotungwa na mtu badala ya kujikita kwa mambo muhimu ya Taifa letu. Sasa hapa mawazo yetu yote tulikuwa tunajua huyu jamaa ana mwaka kama mmoja tangu ateuliwe kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, kumbe ni mawazo ya mtu anayotunga. Hii ni sawa na ile ya mhindi aliyeua naye kajiua, tunajadili mara jana kaonekana mahakamani. Nadhani Jujuman MUONGO umemjua, ukitaka nitamtaja.
Ni kweli kumwita mtu Muongo si matusi, lakini ni neno lenye makali na kamwe halipaswi kutumiwa na mtu muungwana kama wewe.
Si lazima mtu akisema kitu ambacho 'sio ukweli' basi ni 'uongo'. Uongo ni upotoshaji wa makusudi (mtu anakuwa maekusudia kupotosha) na tena ni tabia inyojirudia mara kwa mara. Kama mtu amesema kitu ambacho si kweli lakini wakati anakisema aliamini kwa dhati ni ukweli basi huyu hatupaswi kumwita muongo.
Tazama Kaka Mdogo alivyorekebisha kiungwana 'ukweli' kuhusu rufani za mahakama kuu (nimeona umekuwa wa mwanzo kumpa 'Thanks' kwenye hii post yake!)
Kama angelikuwa si muungwana angeweza tu kuwaita waliochangia mwanzo kwamba ni waongo!Lakini alichgua njia hii ya kiungwana kwa kusema/kutoa ukweli bila kumwita/kuwaita jina lolote wachangaiaji ambao hawakuwa na habari sahihi juu ya taratibu za rufani katika mahakama ya rufaa.
Hakuna anayesema ukweli na hakuna anayesema uongo! Ukweli ni kuwa Jundu aliteuliwa kipindi cha Mkapa na si hiki cha Jakaya but ni mwishoni kabisa so it could be less than 5 years ago. Cha muhimu hapa ni kuwa ana muda mfupi katika ujaji. Nakumbuka kituo chake cha kwanza kilikuwa Moshi na alikuwa chini ya Jengafibili Mwaikugile ambaye sasa atakuwa chini yake.
Ok.. tukubaliane kuwa alikuwa Wakili wa kujitegemea miaka mitano iliyopita. Watu wakisoma majibu yangu mara zote nimetumia qualification kwa maana ya kwamba info zaidi zikipatikana itasahihishwa. Sasa watu wamefikia kuitana waongo.. kwa sababu tarehe ya uwakili wake haikuwekwa definite.
Jamani msome basi kilichoandikiwa! wengine tunatumia maneno vizuri sana tukitaka kumaanisha tunachotaka kusema tunakisema hivyo hivyo.
Nimesema kwenye taarifa ya kwanza "kama mwaka mmoja"
nilipomjibu Jmushi nikasema "exactly! as far as I know"..
wakosoaji na wanaopenda ligi zisizo na ulazima hawajui maana ya "kama" au "as far as I know"!.
wenzako huwa hawajiumu maneno, ukimuona mtu mwongo unamwita mwongo. Katika kufanya hivyo unaonesha kuwa mtu huyo alikuwa anajua ukweli wa kile anachosema na kwa makusudi ameamua kupotosha kwani uongo hauwezi kuwa uongo hadi ijulikane kuwa ukweli ulikuwa unajulikana.
Ukimuona fisadi usisite kumwita fisadi kama unauhakika kuwa vitendo vyake vinalingana na vile vya kifisadi. Ukimuona mwongo, na unajua kuwa ni mwongo (kwa sababu anajua ukweli lakini kauficha) basi usisite kumwita mwongo.
Ok.. tukubaliane kuwa alikuwa Wakili wa kujitegemea miaka mitano iliyopita.
Jamani msome basi kilichoandikiwa! wengine tunatumia maneno vizuri sana tukitaka kumaanisha tunachotaka kusema tunakisema hivyo hivyo.
Nimesema kwenye taarifa ya kwanza "kama mwaka mmoja"
Hii stori ya pili mfululizo umeleta hapa imepinda (pamoja na Jamiiforums kufungiwa Chuo Kikuu Dar). Sasa uko kwenye shimo la credibility, cha kwanza cha kufanya ukiwa kwenye shimbo ni kusimamisha kuchimba. Ukijitetea tetea ovyo ovyo ndo utaonekana mwongo.
Lakini za Mwanakijiji, sina neno la kutumia nisijeambiwa narudia lilelile (muongo), manake anasema alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Hili la Mwanakijiji ndio ulikuwa upotoshaji mkubwa kiasi watu tukaanza kujadili kitu ambacho si cha kweli,
Basi kama ingeandikwa kwa kuhisi nisingesema kuwa kuna kudanganyana.
Usinipangie, mimi sio mtu wa kujiuma uma, nakupa pongezi panapostahili, na nakurekebisha unapokosea.
Na hili ni kwa yoyote. Huwezi kama mwandishi kama bado unatafuta taarifa useme kuwa Jaji Jandu alikuwa wakili kama mwaka mmoja uliopita ndio akateuliwa kuwa Jaji.
Si uwandishi huo eti, ungetwambia tu "Kikwete kamteua Jandu kuwa Jaji Kiongozi", halafu uombe anayemjua zaidi ama mwenye CV yake. Sasa ukishasema kama mwaka mmoja uliopita alikuwa wakili, ina maana unajua kitu fulani, sasa mwaka mmoja ni wakati wa Kikwete, tunaambiwa alichaguliwa wakati wa Mkapa. Huu sio uwandishi, ni upotoshaji ama kutokujiamini. Kwani ukisubiri upate habari kamili utakosa nini?.
Taarifa yako ilikuwa kamili, unajua usitake kucheza na lugha "kama" mwaka mmoja, ukisema kama mwaka mmoja yaweza kuwa miaka 2 kwa mtazamo wa juu na mwezi 1 mpaka miezi 11 kwa angalizo la chini. Haiwezekani kama mwaka 1 ikawa miaka 3.
Hivyo taarifa yako ulitoa kama vile una uhakika. Kwa hiyo ulikuwa na "details" ukazificha ili tujadiliane kwanza ilhali ukiwa kando unaangalia?.
Sasa ukiendelea na obfuscations kama hizo utaanza kuonekana mwongo, na mimi nitakuja kukuita mwongo!
Umekubali kwamba alikuwa wakili miaka mitano iliyopita halafu unataka kuanza kuuma uma ulimi na kujitetea kwamba uliposema "kama mwaka mmoja" ilitosha ku qualify kujuimisha miaka mitano.
Toka lini "kama mwaka mmoja" ikawa sawa kukadiria kipindi cha miaka mitano na kusababisha mjadala mrefu kuhusu uzoefu?
Hii stori ya pili mfululizo umeleta hapa imepinda (pamoja na Jamiiforums kufungiwa Chuo Kikuu Dar).
Sasa uko kwenye shimo la credibility, cha kwanza cha kufanya ukiwa kwenye shimbo ni kusimamisha kuchimba. Ukijitetea tetea ovyo ovyo ndo utaonekana mwongo.
Habari ulizoleta inaonekana si za kweli, umesema mwenyewe zinaweza kusahihiswa kwa hiyo usisema wanaokusahihisha wanaleta ligi.
Mheshimiwa Kuhani, tuliza boli ama sivyo utafungwa magoli mengi na Mwana Kijiji ameyaeleza aliyokufunga. Under normal procedure Jaji Fakih amepungua viwango vya uteuzi. Kwa heshima yake hatutaki tulete mengi hapa kukuhakikishia wewe usiyeamini, unayeacha ujumbe na kumshambulia mjumbe.