JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

wewe hujui status za vyuo, ninawasiwasi na elimu yako eunda ni drs la 12 mwisho.
Hakuna chuo ulimwenguni kama ilivyo Open University. Hata TZ tazama hata waombaji wa kazi kutoka OUT wako makini zaidi kuliko unavyodhani
 
du!!...huyu mamy naona JK anamkamatisha mi title ya lazima kwa kila hali....maana angeweza tu kurudi udsm(baada ya kushindwa kule UN) na kuendelea pale kufanya alichokuwa anafanya pale udsm kabla ya uwaziri...Lakini kwa vile issue inaandaliwa kupewa mkate wa urais(kupitia ccm)hapo 2015....anabambikwa mi title mlima ili tu kumjazia CV yake....ili itakapofika 2015 wamsimamishe kama mgombea mwanamke wa kwanza ccm kugombea urais....Hapa ndipo aliposimamia JK.....Lazima watamsimamisha...ili kukata ngebe za upinzani,udini(maana huyu ni muslim)na maswala ya jinsia(kuwavuta ma mama wote tz)......mtaniambiaga......issue ya wakubwa hii.......
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

[TABLE="width: 655"]
[TR]
[TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
[/TD]
[TD][/TD]
[TD]PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013

O.U.T. is now OUT (Imekwisha). Si UN ilimshinda huyu?
 
suzie,
kwanini ashindwe...? huyo kateuliwa kuwa mkuu wa chuo siyo makamu mkuu wa chuo. hashiriki ktk utendaji wowote wa kila siku wa hapo chuoni , yeye ndo anamangia kazi makamu mkuu , na huyo ndo mtendaji mkuuu . migiro anakuwa tu mkuu wa baraza/bodi

Hapo kwenye Bodi hapo ndo maamuzi yanakofanyika ninauhakika huyu mama hii nafasi kwake ni kubwa sana bora akafundishe maana notes unadesa unawapa wanafunzi lakini hili linalohitaji upana wa mawazo mapya kwa Migiro hajakuzwa hivyo
 
Pale OUT kuna maprof na ma Dr. sio wanasiasa wenye mrengo wa kulia. Hivyo Rose kapandikivzwa!
 
Ngoja tumpe nafasi Dr tuone ana nini cha kutuonyesha.
Kila la kheri mama
 
sawa huyu ni doctor,je profesa tolly mbwete atakuwa kama nani......mkuu wa chuo awe dokta afu msaidizi awe profesa?kweli tz vilaza kibao:target:
ww ndio kilaza maana hata hujui profesa ni mtu wa aina gani, kwa fikra zako uprofesa ni cheo cha kielimu, ----- ww baki hivyo hivyo
 
wewe hujui status za vyuo, ninawasiwasi na elimu yako eunda ni drs la 12 mwisho.
Hakuna chuo ulimwenguni kama ilivyo Open University. Hata TZ tazama hata waombaji wa kazi kutoka OUT wako makini zaidi kuliko unavyodhani


Bado sijakuelewa vizuri..
 
Kutoka naibu katibu kuu wa umoja wa mataifa hadi kwenda ukuu wa chuo?,

mbaya zaid unateuliwa na madokta uchwara?
Hatari sana hii..
 
Kwa upande wng naona ni mama nzr kbs,ILa Mfumo wa Uongozi ktk kila eneo ndani ya Nchi yetu,Umemezwa na KUTOLEWA NA MAAMUZI YA KISIASA ZAIDI.So Hataweza
 
Cheo alichopewa sasa hivi ni cha kisiasa zaidi- kazi yake kuu ni kutoa shahada. Hakihitaji mtu aliyebobea katika masuala ya taaluma-kumbuka akina Al-noor Kassum(SUA), Malecela(OUT),Mwinyi(UDSM) n.k

Nilichanganya, nilidhani amekuwa VC!
 
Aliyetoka Malecela naye ni profesa?
Mkapa ni mkuu wa chuo cha Udom naye ni profesa?
Vp unamjua mkuu wa UDSM?

Kwa mkuu wa chuo udsm hasikiki au kwa vile sio mwanasihasa?
 
Back
Top Bottom