JK aikwepa Mei Mosi... Rais Kikwete hatahudhuria Mei mosi


K

Keil

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2007
Messages
2,214
Likes
7
Points
135
K

Keil

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2007
2,214 7 135
Rais Kikwete hatahudhuria Mei mosi

na khamis mkotya

RAIS Jakaya Kikwete, hatakuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha sherehe za Mei mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa.

Mwaliko wa sherehe hizo ulipelekwa kwake na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Uamuzi huo wa Rais, umeelezwa kwamba umetokana na majukumu mengi ya kitaifa yanayomkabili.

Kutokana na uamuzi huo, TUCTA imeeleza kusononeka kwa maelezo kuwa kuwapo kwa Rais katika maadhimisho hayo ni muhimu.

Pia Rais Kikwete amelalamikiwa kwamba amekataa kauli mbiu iliyokuwa imependekezwa na TUCTA kwa ajili ya sherehe za mwaka huu.

Kauli mbiu iliyopelekwa kwa Rais ilikuwa ikisema: “Maisha bora yanawezekana tukiutokomeza ufisadi.” TUCTA wanadai kwamba maneno hayo hayakumfurahisha Rais Kikwete.

Aidha, TUCTA imeeleza kushangazwa na uamuzi wa Rais kukataa kuhudhuria mkutano wa 96 ulioitishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO), utakaofanyika Geneva, Uswisi.

Imeelezwa kwamba kiongozi huyo ameahirisha kwenda huko kutokana na kubanwa na vikao vya bajeti inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni Juni mwaka huu.

Naibu Katibu wa TUCTA, Nicholas Mgaya, alitoa maelezo hayo alipozungumza na MTANZANIA ofisini kwake jana, kuhusu maandalizi ya sherehe za Mei mosi.

Mgaya alisema mwaliko ulipelekwa kwa Rais Kikwete Februari, mwaka huu kupitia Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana.

Kwa mujibu wa Mgaya, wiki mbili zilizopita Shirikisho, kupitia wizara hiyo, lilipata taarifa kuwa Rais hatoweza kushiriki, badala yake atawakilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

"Tumesikitishwa hatua hiyo kwa kuwa inaonyesha anaanza kujitenga na wafanyakazi. Tunakubali Waziri Mkuu, lakini kwa shingo upande," alisema na kuongeza;

Kuhusu mkutano wa Geneva, Mgaya alisema Rais Kikwete alikuwa amealikwa na kwamba alipewa hadhi ya kufungua mkutano huo utakaofanyika Juni, mwaka huu kutokana na nafasi yake ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Kwa mujibu wa Mgaya, mwaliko wa ILO kwa Rais Kikwete kushirikia katika mkutano huo ilikuwa ni nafasi nzuri inayoijengea sifa Tanzania.

"Hatujaridhika na sababu zilizotolewa na Ikulu kwamba Rais hatahudhuria mkutano huo. Ina maana Rais hana wataalamu hadi asimamie bajeti mwenyewe?,” alihoji.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, amejibu malalamiko ya TUCTA kwa kusema Rais ameona kuwa baada ya kuhudhuria Mei mosi mwaka 2006 mkoani Shinyanga na mwaka 2007 mkoani Mwanza, ameona sasa ni busara kutoa nafasi kwa mmoja wa wasaidizi wake.

“Rais ana kawaida ya kutoa maelekezo ili awakilishwe katika shughuli mbalimbali. Hivi karibuni utakumbuka alifanya hivyo kwa kuwakilishwa na Makamu wa Rais nchini Uingereza na Denmark,” alisema.

Rweyemamu alisema ni kweli Rais alialikwa katika mkutano wa ILO, lakini kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi ya kitaifa, ameomba asihudhurie, badala yake ameshauri apangiwe ziara ya kutembelea makao makuu ya chombo hicho kwa wakati mwafaka.

Alisema ameomba asihudhurie mkutano huo kwa vile Juni kutakuwa na vikao vya bajeti, na yeye akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri, anapaswa kuwapo wakati huo, bajeti ya nchi ni kitu nyeti sana,” alisema Rweyemamu.

Kuhusu kauli mbiu, Mkurugenzi huyo alikanusha vikali madai ya kufutwa ile iliyohusu ufisadi.

“Rais hawezi kufuta kauli mbiu, wataitumia hiyo hiyo waliyoipendekeza,” alisema.

Source: Mtanzania

Ukiona mtu aliyekuwa na kiherehere cha kujikweza mbele ya wafanyakazi anaanza kuvuta miguu basi elewa kwamba nchi inaelekea kumshinda. Hana majibu ya Risala ya Wafanyakazi, Tume ya mapendekezo ya mishahara mpaka leo hii haijulikani report yake na kibaya zaidi dongo ya kauli mbiu limemuweka pabaya kwa kuwa lina ukweli kwa 100%. TUCTA wanatakiwa waendelee kivyao na warushe madongo hewani hata kama hakutakuwa na kiongozi wa serikali ili mradi msg itakuwa sent and delivered. Atakaeona dongo limemgusa basi atajua namna ya kulikwepa ama kujiweka mbali nalo, lakini JK hana ubavu wa kulikwepa. Tunachotaka sasa ni TUCTA iwe kiini cha mabadiliko ya fikra kwa watanzania kwa kuwa ina matawi sehemu zote mpaka vijijini. Huko ndiko kuliko na kura zinazowapa kiburi CCM kiasi kwamba wanaona kelele za mpangaji haziwanyimi usingizi japo siku hizi naona wanakesha hata kama hawakubali hilo!
 
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
92
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 92 0
RAIS Jakaya Kikwete, hatakuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha sherehe za Mei mosi zitakazofanyika kitaifa mkoani Iringa.

Mwaliko wa sherehe hizo ulipelekwa kwake na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA). Uamuzi huo wa Rais, umeelezwa kwamba umetokana na majukumu mengi ya kitaifa yanayomkabili.
Sasa rais wa jamhuri tena yetu ya Tanzania, anapoanza kukwepa wafanyakazi wa jamhuri something is not right, lakini hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja very soon tutayajua yanayojiri huko ndani maana hapa something is not very right............ na fumbo mfumbie mjinga maana mwerevu.......!

Yaaani sasa mkulu hataki tena zile ziara za wizarani na masokoni, na mahospitalini, kulikoni?
 
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
9,390
Likes
464
Points
180
Njowepo

Njowepo

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
9,390 464 180
Ninachojua mimi waziri hausiki kuandaa budget ila kuna wanaoiandaa uku wakizingatia mapendekzo the anaipitia iyo draft kabla ya kuwa presented.
Amekwepa majukumu si anajua na vimeo na wafanyakazi!
Ila ajue running from the problem is not the soln
 
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2006
Messages
4,124
Likes
90
Points
145
Mtu wa Pwani

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2006
4,124 90 145
mwaka huu umetukalia vibaya....
 
Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Messages
887
Likes
17
Points
35
Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2008
887 17 35
Sasa rais wa jamhuri tena yetu ya Tanzania, anapoanza kukwepa wafanyakazi wa jamhuri something is not right, lakini hakuna siri ya zaidi ya mtu mmoja very soon tutayajua yanayojiri huko ndani maana hapa something is not very right............ na fumbo mfumbie mjinga maana mwerevu.......!

Yaaani sasa mkulu hataki tena zile ziara za wizarani na masokoni, na mahospitalini, kulikoni?
Ameona za nje zinalipa zaidi
 
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,011
Likes
38
Points
145
Mpita Njia

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,011 38 145
Safari imeanza hiyo, tunaisubiri ripoti nyingine ya REDET tuone ameporomoka kiasi gani
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
80
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 80 0
kikwete mwaka huu atakimbia mengi, na atawakimbia wengi.
na angeenda kwenye mkutano wa mei mosi angesema nini? samahanini lakini kila niliyemchagua kwenye nafasi ya uwaziri fisadi?
lazima kwa hali ilivyo akwepe watu. na bado....ndo kwanza mwanzo huu
 
Bubu Msemaovyo

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2007
Messages
3,435
Likes
58
Points
145
Bubu Msemaovyo

Bubu Msemaovyo

JF-Expert Member
Joined May 9, 2007
3,435 58 145
Kukataa kuwa mgeni wa heshima wa sikukuu ya Mei Mosi kule Iringa pia kunaweza kuwa ni kwasababu ya kuwa kweli yuko kwenye masuala ya budget lakini pia hii ina ashiria ni kwakiasi gani safari za nje zimeathiri kazi zake hapa nyumbani. Hivi kwa sasa Mkulu ana ruti ya nchi gani kwa mwenye taarifa.
 
Single D

Single D

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2007
Messages
459
Likes
5
Points
35
Single D

Single D

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2007
459 5 35
Hana jipya la kuwambia wafanyakazi,maana Maisha bora yameyeyuka.Falsafa yake inatumika tena kumkaanga.EPA haina majibu,Mawaziri wake wanajiziulu n.k

Nyongeza ya mshahara kwa njia ya kisayansi(aliunda tume kutafiti) imekwama?Maana tume ilifanya utafiti na mapendekezo yametolewa hayatekelezeki.Na TUCTA wanahitaji kima cha chini 315k

Kukimbia wajibu si kusuluhisha tatizo.
 
T

think BIG

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
236
Likes
13
Points
35
T

think BIG

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
236 13 35
Yaaani sasa mkulu hataki tena zile ziara za wizarani na masokoni, na mahospitalini, kulikoni?
hahahah .. I like this, ile ilikuwa nguvu ya soda sasa yamemshinda!

Kwani kwa sasa atawambia nini wafanyakazi!! ripoti ya Kamati ya kurekebisha mishahara imeingia mitini, mishahara kwa wafanyakazi wa sekta binafsi vurugu tupu!! huku kila kukicha NBS hawachelewi kutoa report yao ya mwezi, kama ifuatavyo:

Tanzania`s inflation rose marginally to 9.0 per cent in March from 8.9 per cent in February due to higher food prices, the National Bureau of Statistics said yesterday.

Balaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
 
IsayaMwita

IsayaMwita

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2008
Messages
1,123
Likes
11
Points
135
IsayaMwita

IsayaMwita

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2008
1,123 11 135
Watanzania, tusimlaumu sana JK kwani taabu hizi zote na mzigo huu kaachiwa na Mkapa, kuwa miwaziri mizi, ujue kama asingeiteua kweli angejiweka pabaya, sasa tunamtaka aende pale Iringa akaseme nini jamani? Kikwete ana nia njema tuu ila hawa maswahiba zake ndiyo wanamuangusha
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
80
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 80 0
Mkuu lazima akwepe safari, manake safari za nje zinamsubiri nyingi kweli kweli.
amealikwa kwenye mkutano wa Maendeleo ya Afrika, JAPANI kama sikosei atakuwa huko kuanzia kati kati ya mwezi Mei.
baada ya hapo mkutano wa G8 utakaofanyika huko huko Japan June sijui Julai.
atapata nafasi ya kufanya kazi za ndani saa ngapi?
 
K

Kipanga

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
679
Likes
12
Points
0
K

Kipanga

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
679 12 0
.. Anakimbia kivuli chake tu hapo hana jipya kama ni dereve gari limemshinda kitonga mnategemea nini?

Bora asiende tu kwenye hiyo Mei mosi hatakuwa na jipya la kuwaambia Wa-Tz...Alitaka kazi watu wamempa kazi lakini anaelekea kuchemka kabisaaaaa
 
Power to the People

Power to the People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2007
Messages
1,200
Likes
253
Points
180
Power to the People

Power to the People

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2007
1,200 253 180
Nani anajua kama kuna waajiriwa wa makampuni binafsi wameanza kupokea mishahara aliyoilazimisha Chiligati ama ilikuwa kuwafanya watu wajinga.
 
H

Hamad Yussuf

Member
Joined
Mar 31, 2008
Messages
25
Likes
0
Points
0
H

Hamad Yussuf

Member
Joined Mar 31, 2008
25 0 0
Msanii amepatikana, ipo siku atakiri hadharani kwamba mambo yameshamshinda, na wapambanaji tupo tutampokea kijiti ili kukifikisha pale watanzania wanapotaka kifike, arobaini yake naona haiko mbali inakaribia sana tu washikaji.
 
M

Mbangaizaji

Senior Member
Joined
Jul 23, 2007
Messages
121
Likes
26
Points
35
M

Mbangaizaji

Senior Member
Joined Jul 23, 2007
121 26 35
Si Mwaka jana aliwaahidi kufanyia kazi yale mapendekezo yao ya kungeza mishahara na akaunda tume. Ripoti akapewa ila hamna kilichofanyika zaidi ya kuweka mikaganyiko especially kwa wafanyakazi binafsi.SasaMei Mosi hii ataenda kuwasanii nini?
Ila nimeipenda hiyo kauli mbiu ya mwaka huu"Maisha Bora yanawezekana tukitokomeza(tukiwafilisi) maufisadi"
 
T

Tuandamane

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2008
Messages
1,220
Likes
2
Points
135
T

Tuandamane

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2008
1,220 2 135
Watanzania, tusimlaumu sana JK kwani taabu hizi zote na mzigo huu kaachiwa na Mkapa, kuwa miwaziri mizi, ujue kama asingeiteua kweli angejiweka pabaya, sasa tunamtaka aende pale Iringa akaseme nini jamani? Kikwete ana nia njema tuu ila hawa maswahiba zake ndiyo wanamuangusha
lakini aliposema tumuache apumzike na kuwa hatamgusa alikuwa akifikiri nini, kama kaamua kununua kesi basi asikwepe kwenda mahakamani
 
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2007
Messages
3,741
Likes
40
Points
145
Pundit

Pundit

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2007
3,741 40 145
Watanzania, tusimlaumu sana JK kwani taabu hizi zote na mzigo huu kaachiwa na Mkapa, kuwa miwaziri mizi, ujue kama asingeiteua kweli angejiweka pabaya, sasa tunamtaka aende pale Iringa akaseme nini jamani? Kikwete ana nia njema tuu ila hawa maswahiba zake ndiyo wanamuangusha

Hivi kuna kitu kama "kuachiwa" mawaziri?

Kikwete angetaka angeanza na baraza jipya kabisa na kuacha wote walioserve katika serikali ya Mkapa.

Tafuta kingine cha kumtetea.
 
M

Mama

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2008
Messages
2,858
Likes
23
Points
0
M

Mama

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2008
2,858 23 0
Watanzania, tusimlaumu sana JK kwani taabu hizi zote na mzigo huu kaachiwa na Mkapa, kuwa miwaziri mizi, ujue kama asingeiteua kweli angejiweka pabaya, sasa tunamtaka aende pale Iringa akaseme nini jamani? Kikwete ana nia njema tuu ila hawa maswahiba zake ndiyo wanamuangusha
Si alituahidi atashughulikia hayo mambo, inakuwaje hadi leo hajayashughulikia, kila siku kamati!! nachoka kabisa. Atapata mzigo huu wa lawama na asipoangalia vizuri atatakiwa awajibishwe kwa kutoa ahadi hewa. Kama alijua hawezi kufuatilia mambo kwa nini aliahidi?ilikuwa danganya toto ili tumpe urais?

Tanzania inabidi tujifunze kuwajibika...asipowajibishwa JK basi hata marais wanaofuata hata wakitoka upinzani watafanya madudu haya. Tunataka utawala wa sheria, and everyone especially leaders have to be responsible for his actions, unless never run for leadership.
 

Forum statistics

Threads 1,235,417
Members 474,534
Posts 29,221,348