Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,356
1. Ni agizo la kibiblia, mahali fulani Yesu alisisitiza umuhimu wa kuwalisha wenye njaa, kufariji wagonjwa na KUTEMBELEA WAFUNGWA (Bila kujali kama wamefungwa kwa haki au kwa kuonewa). Jela ni mahali pa upweke sana, siku moja ya ubaoni si kama ya uraiani ambayo huenda haraka na kuisha, kufunga safari kumwona jamaa aliye huko kutamfanya ajue kuwa kuna watu bado wanamjali.
2. Kwa nchi ambayo haki ni ya kulenga kwa manati lazima ujue kuwa jela ni kama msikiti, siku zote kupo wazi na ni kwa ajili ya yeyote hivyo hata wewe unaweza kujikuta uko ubaoni muda wowote. Ukweli mchungu ni kuwa wahalifu wengi walio jela ni maskini wenye kesi ndogondogo (au za maembe kama baadhi ya wafungwa wanavyoziita) ambao walishindwa kumalizana na polisi njaa kabla mambo hayajawa mambo. Kanuni ya 'Karma' inajitokeza hapa, wakumbuke nao wakukumbuke.
3. Jela baada ya Mungu ni askari magereza, mheshimu sana unaenda kumwona mtu wako.
4. Wenzio hukaa na sura zile zile kila siku, kuona sura yako ngeni anayoifahamu kutampa tumaini japo kiduchu, unaweza kumnunulia chochote unachoona kinafaa.
5.Ni darasa zuri kwa watoto, nenda nao unapoenda kuona wafungwa na mahabusu. Kutawafanya wajue kuwa kuna maisha mengine tofauti na haya na sheria ni tofauti kabisa. Zaidi kutajengea nidhamu maishani.
6. Taratibu za ubaoni si ngumu, itakuchukua takribani dakika 45 hivi mpaka kumuona mfungwa au mahabusu wako kulingana na msongamano wa siku hiyo, si muda mwingi kulinganisha na thamani ya safari yako kwa huyo unaemuona. Siku ni wikiendi na siku za sikukuu kuanzia saa mbili hadi saa kumi, usisahau kuzima simu yako.