Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,483
- 40,002
Sawia, Muruwa kabisa
toleo hilo lina makoa mengi ya herufi n.k najaribu kulisahihisha na kuliweka sawa. We will update it asap.
Sawia, Muruwa kabisa
Hakijaonekana bado. Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa vyama vya upinzani, kinaweza kuendelea kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama chochote, ili mradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa nchi yetu unataka yasemwe. - Nyerere
Kwa kuweka kitabu hiki hapa, sijui mmewakosesha wahusika mapato kwa kiasi gani. Na sijui swala la copyright linakuwaje. Pale Great thinkers infringe copyright.
not really.. hii haikuwa kwa ajili ya faida.... ni public domain..
Nilikuwa nimeamua kuchukua likizo na JF lakini imenibidi nikatize likizo yangu kwa sababu ya hii thread. Asante sana Mkuu SubiriJibu umenikumbusha mbali na hapa natokwa machozi nikitafakari hatma ya nchi yangu niipendayo Tanzania inavyonajisiwa hivi sasa na viongozi limbukeni. Mungu atusaidie, amina.
nashukuru lakini humo zimo zaidi habari za TANU kuliko Azimio la Arusha lenyewe, kama unalo ningefurahi kulionaAzimio la Arusha liko kwenye hii link hapa https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=8737&stc=1&d=1268215518
Nilikuwa nimeamua kuchukua likizo na JF lakini imenibidi nikatize likizo yangu kwa sababu ya hii thread. Asante sana Mkuu SubiriJibu umenikumbusha mbali na hapa natokwa machozi nikitafakari hatma ya nchi yangu niipendayo Tanzania inavyonajisiwa hivi sasa na viongozi limbukeni. Mungu atusaidie, amina.
- Wakipewa nafasi na sisi wananchi, ambao kama unayosema ni kweli basi ni malimbukeni kuliko hata hao viongozi, kwa sababu wanachanguliwa na sisi wananchi, au? Likizo imeisha mkuu? karibu sana tumkome nyani!
FMEs!
Natafuta kitabu kilichoandikwa na J.K. Nyerere, "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" kwa Kiswahili au Kiingereza.
Jitihada za kukipata mitaa ya Dar zilishindikana baada ya kuambiwa 'udaku' kwamba kimepigwa marufuku kinamna. Madukani mwa vitabu mwote nilimopita kukiulizia waliniona juha, kana kwamba 'kila mtu anajua' kitabu kilipigwa marufuku.
Madai hayo ni ya kweli au uzushi tu wa uchaguzi?
Shida yangu ni nakala moja tu ya kitabu hicho kwa ajili ya rejea ya kitaaluma.
Natanguliza shukrani.
Mlenge
=============
UPDATE:
Kwa msaada wa mkuu SubiriJibu kitabu kimepatikana, nakala inaweza kupatikana chini hapa
Viongozi wetu wakuu hawawezi kukiuka Uamuzi na msimamo wa Chama kizima, halafu wadai kuungwa mkono na viongozi wa chini yao au na wanachama kwa jumla. Kwa kweli tunatazamia kuwa viongozi hao watapingwa kwa nguvu kabisa, na kama hapana budi kufukuzwa. Huko ndiko kuwajibika. Bila hivyo viongozi wetu watafanya wapendavyo bila kuwa na wasiwasi. Watapinda, watapuuza, watavunja maamuzi na msimamo wa chama bila kuwa na hofu yoyote. Wenye hofu watakuwa ni viongozi wa chini na wanachama wa kawaida watakaofanya ujasiri wa kuwapinga viongozi wakuu. Maana hao wataonekana kuwa ni wakorofi na wachochezi, na watachukuliwa hatua za nidhamu! .
Kukubali kufanywa vikaragosi vya viongozi ni dalili ya woga, si dalili ya heshima; na woga na heshima ni vitu viwili mbali mbali. Maadili mema hayatudai tuwaogope viongozi wetu.
Hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa.
Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa vyama vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza nchi yetu badala CCM au ambacho kingekilazimisha Chama Cha Mapmduzi kusafisha uongozi wake kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao.
Lakini bado sijakiona chama makini cha upinzani; wala,dalili zozote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, Chama hili kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini, hili si jambo la kutarajia bila ya hofu na wasi wasi!
Mlenge,
Kama uko DSM ningekushauri umtafute Walter Bgoya. Yeye alichapisha kitabu cha Mtei. Kama walivyosema waungwana hapo awali, kitabu cha Mwalimu kilichapishwa Zimbabwe baada ya kufanyiwa mizengwe na wenye madaraka kisichapishwe DSM. Ninavyo vyote vya Kiswahili na Kiingereza lakini bahati mbaya niko mbali ya DSM.
Mwalimu anaendelea kusema katika UWHT..
Na kuendelea kugongomelea msumari:
na kutupa elimu hapa:
Na kama nabii pweke jangwani akasema:
Na kama Musa mbele ya wana Waisraeli walioasi nyikani akasema:
MM Ulianza kupiga type ili uweze kutuletea hiyo nakala hapa? kwa kweli mzee kama umefanya hivyo nikupongeze huu ni moyo wa pekee kuhakikisha watu wanaijua kweli labda siku moja hiyo kweli itawaweka Huru. Ubarikiwe sana mkuuNadhani sasa kiko kwenye posti ya kwanza..
MM Ulianza kupiga type ili uweze kutuletea hiyo nakala hapa? kwa kweli mzee kama umefanya hivyo nikupongeze huu ni moyo wa pekee kuhakikisha watu wanaijua kweli labda siku moja hiyo kweli itawaweka Huru. Ubarikiwe sana mkuu
Hoja ya pili wanayoisema ni ile ya kura ya maoni. Wanasema: "Kuhusu suala la kura ya maoni, Serikali iliona kwamba utekelezaji wake ni sawa na kufanyya uchaguzi mkuu,jambo ambalo ni gharama kubwa. Aidha, kwa kuzingatia kuwa kura ya maoni hupigiwa suala linalohitaji jibu NDIYO au HAPANA, ni vigumu kupata swali lililo wazi kwa wananchi ambao hawana uzoefu wa utaratibu huu wa kura ya maoni.
Ni vigumu kuelewa kwa nini watu walio tayari kuwabebesha wananchi mzigo wa Serikali Tatu za kudumu, wanahofu gharama za kura ya maoni ya mara moja! Na kama viongozi wetu ni wapumbavu kiasi cha kwamba hawawezi kutunga swali "Je, unataka Serikali Tatu?" Au "Je, unataka Serikali ya Tanganyika?" kazi hiyo wangeweza kuwaachia wataalamu wenye uwezo zaidi. IIa wasiwatukane Watanzania, ambao miaka yote hii wamekuwa wakipiga kura za NDIYO au HAPANA, kwamba ati wakiulizwa swali kama hili watashindwa kulijibu.