RayB
JF-Expert Member
- Nov 27, 2009
- 2,751
- 196
Naendelea kukipitia lakini nimeipenda pale waroho wa madaraka walipokuwa wanang'ang'ani kundelea kuwepo;
" Plato, Myunani wa kale, alipendekeza kuwa mafilosofa ndio wanaofaa kuwa watawala wa nchi, maana wana sifa mbili muhimu: kwanza, Wana uwezo wa kutawala, na pili, hawapendi kutawaIa. Kwa hiyo, Jamhuri ya Plato itakuwa na sheria ya kuwalazimisha mafilosofa kutawala kwa zamu; na mtu zamu yake ya kutawala ikisha, atafurahi sana kurudia shughuli zake za falsafa ambazo ndizo hasa anazozipenda.
Lakini nchi zetu hazitawaliwi na mafilosofa wa Plato; watawala wetu ni wanasiasa wa kawaida ambao wanapenda sana kutawala hata kama hawana uwezo wa kutawala; na ambao wako tayari hata kuhonga ili wachaguliwe kuwa watawala, na wakisha kuchaguliwa hawatoki bila kulazimishwa. Si busara kuwaachia wao wenyewe ndio wawe waamuzi wa lini waache kuwa watawala."