Jinsi ya kusoma ukurasa wa mtandao bila matangazo ya biashara

Natty Bongoman

JF-Expert Member
Oct 10, 2008
403
191
Habari wanaJF.

Siku hizi matangazo ya biashara kwenye kurasa nyingi za mitandaoni yamezidi - hadi kufunika ulichofungua kurasa kusoma. Matangazo mengine yanafunguka katikati ya shughuli. Iko njia ya kusoma hizi kurasa bila bugudha kwa kutumia mfumo wa browser READER'S MODE. Browser ni program unayotumia kuingilia na kuperuzi mtandao, kwa mfano FIREFOX, EDGE, IE nk. Hii 'reader mode' imewekwa kama chaguo kwa mfumo wa kitufe.

Mfano, unafungua kurasa upo kama hivi (picha chini)
1647120891363.jpeg


HII NI FIREFOX - ukibonyeza kitufe namba 1 (picha ya karatasi lenye maandishi)
ukurasa utakuja kama hapo pichani chini
1647121007008.jpeg

Sasa upande wa kulia unaweza hata badilisha ukubwa wa herufi ama kusomewa ama ...
- kurudi ukurasa wenye matangazo ya biashara unabonyeza kitufe kile kile (1)

Nyongeza:
  • kitufe namba 2 picha ya kwanza - ndo cha ku bookmark (kutunza anuani ya ukurasa) ukitaka kurudi kwenye ukurasa uliotunza moja moja bila kuusaka.
  • kitufe namba 3 picha ya kwanza - ukibonyeza menu itakuja, ukichagua 'bookmarks' utaikuta ile anuani ulotunza (kwa mfumo wa link), ukibonyeza ukurasa ulotunza unafunguka pale pale ulipoachia...
kwa hiyo, kwa mfano unaingia JF mara nyingi, na kila wakati unaanzia kule google hadi ufike ku log in... unaweza tunza ukurasa wa JF kwa ku bookmark - afu kila unapotaka kuingia JF unabonyeza bookmark ... pia kwa mfano kifaa ni chako huna haja ku log off - basi pale unapo log ukibonyeza box linasema 'keep me logged...' afu uka bookmark - basi utakuwa unaingia JF moja moja bila ku log in kila wakati.
 
Sasa ukiwa unasoma bila kuona hayo matangazo mwenye site atakula wapi maana mnapogusa matangazo mnamfanya mmiliki wa site hiyo aendelee kuwapa mambo mazuri zaidi
 
njia rahisi nikuweka extension ay abp kwa browser yako umemaliza

1647764938118.png
 
Back
Top Bottom