Jinsi ya Kusajili kampuni katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

hapo kwenye taasisi za mikopo nahitaji msaada wa maelezo flani flani ila ningependa kujua km kuna gharama kwa ajili ya hyo huduma ni kiasi gani?
 
Asante sana Bwana ANJOA CPN kwa ushauri wako mzuri.
Sijaelewa unaposema Katiba.
Najua Memorandum and Articles of Association ndio inayofungua kampuni hasa kwa mfano ya mtu na mke wake. Hiyo katiba ni lazima iwepo?
 
Last edited by a moderator:
Asante sana Bwana ANJOA CPN kwa ushauri wako mzuri.
Sijaelewa unaposema Katiba.
Najua Memorandum and Articles of Association ndio inayofungua kampuni hasa kwa mfano ya mtu na mke wake. Hiyo katiba ni lazima iwepo?

Nadhani alikosa tafsiri nzuri ya kiswahili lakini nadhani alimaanisha Memorandum and Articles of association maana vitu hivi ni kama katiba😆😜
Nahisi tu hivyo wanaweza kujibu wenyewe
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Anjoa hebu niweke wazi hapa, majina haya yanakubalika kuwa business name?
1)kawe procesing company
2)migomba company
3)migomba enterprises
kama yanakubalika vipi nayo lazima uainishe mtaji? je madhara ya kuandika mtaji mdogo ni upi?
 
Last edited by a moderator:
Ndio mkuu. Katiba ni memorandum and articles of association. Asante sana mkuu.
Asante sana Bwana ANJOA CPN kwa ushauri wako mzuri.
Sijaelewa unaposema Katiba.
Najua Memorandum and Articles of Association ndio inayofungua kampuni hasa kwa mfano ya mtu na mke wake. Hiyo katiba ni lazima iwepo?
 
Mkuu, business name haihitaji mtaji. vile vile si vema majina unayoyakusudia kuyaweka wazi jukwaani wajanja watayachukua. Naomba tuwasiliane mkuu.
Mkuu Anjoa hebu niweke wazi hapa, majina haya yanakubalika kuwa business name?
1)kawe procesing company
2)migomba company
3)migomba enterprises
kama yanakubalika vipi nayo lazima uainishe mtaji? je madhara ya kuandika mtaji mdogo ni upi?
 
Karibu sana mkuu. Kama upo hapa Dar ni vema ungefika ofisini kwetu, tutaongea kwa kirefu zaidi. Ushauri utapata bure.
hapo kwenye taasisi za mikopo nahitaji msaada wa maelezo flani flani ila ningependa kujua km kuna gharama kwa ajili ya hyo huduma ni kiasi gani?
 
ZINGATIA HAYA UNAPOTAKA KUSAJILI KAMPUNI

1. Jina. Unapotafuta jina jitahidi jina liwe linatamkika kirahisi ili isikusumbue katika marketing lakini kikubwa ni maana ya jina. Kuna maneno mengine ni matusi kwa lugha nyingine, hivyo jitahidi sana kufanya utafiti wa kina wa jina hilo.

2. Mtaji: Maamuzi ya mtaji kiasi gani kiandikishwe ni jambo la msingi sana. Wengi hupenda kuweka mtaji mdogo ili kupunguza gharama za usajili na kodi, vema, lakini hicho kisiwe kigezo mama cha kukuamulia mtaji uwe kiasi gani. Tambua kwamba mtaji unawakilisha ukomo wa kuwajibika kwa kampuni katika wajibu wake.

3. Wanahisa: Wanahisa mnatakiwa kuwa watu mnaofahamiana vema, wenye mrengo unaofanana na mnaelewana. Tofauti na hilo itasababisha kuchelewa kwa maamuzi muda wote na kuhatarisha ustawi wa biashara.

4. Uandishi wa katiba: Ni hatari kutegemea mtu yeyote asiye na utaalam wala ujuzi wa kuandika katiba akuandikie. Kibaya zaidi wengine huandika wao wenyewe hata kama hana utaalam na uzoefu huo. Hata kwa wanasheria, si kila mwanasheria anaweza kukuandikia katiba iliyo standard. Kitu kibaya zaidi watu hudhani kwamba unaweza kuchukua katiba yoyote na kubadili majina tu kisha ukaendelea na usajili.

Hawaangalii mpangilio wa maneno na malengo, hawazingatii kama katiba ina vipengele vya kuruhusu mambo Fulani Fulani kufanyiwa mabadiliko, Hawazingatii ni namna gani founders wanalindwa na katiba, na mengine mengi. Hivyo unashauriwa kuwatumia wataalam wenye uzoefu kufanya kazi hiyo.

Kwa huduma za uhakika na weledi katika masuala hayo yote, waone Anjoa company limited. Pia tunatoa usaidizi katika kusajili NGO, Huduma za kihasibu, kuandika michanganuo ya biashara, na usaidizi kwa wale wanaotaka kuanzisha taasisi za mikopo n.k

Wasiliana nasi kwa namba 0759-692024 au 0688-510564,
Email: anjoa_limited@yahoo.com,
Au fika ofisini kwetu Dar es Salaam Kinondoni – Manyanya, mtaa wa Togo, Jengo la Tiger tower ghorofa ya pili.
 
hii imekaa poa, gharama ni kiasi gani rafiki, kuandaa memorundum ya kampuni na kusajili jina?
 
Jaman naomba msaada tunahitaji kuanzisha kampuni na kubwa zaidi bei ya kuandaa "memorandum and article of company" ni shingap? Pamoja na gharama zingine?
 
Ni kweli we need something like that, nihakika huenda ndo ikawa tiketi ya kusafirisha rushwa kuzimu online nani atakaye niomba rushwa.......... mimi nitaunga mkono hata kama bunge litakapoona vitu kama hivi visiwe vya kwenda ana kwa ana mala nyingine ni usumbufu na kupoteza fedha
 
Ndugu wanajamii forums hivi kusajili saccos nako inabidi niende brela? je kwenye jina la saccos naweza kutumia limited mwishoni mwa jina la saccos? je hiyo process inaweza kugharimu kiasi gani?
 
0753 125 474.....wanajamvi kuna huyu mdau kanitapeli na wadau wangu watatu tulimpa laki sita sita....wiki ya tatu sasa hapokei simu...na office yake magomen kafunga....alikuwa yanapatikana CRDB vijana branch. nako imekuwa shida kumpata......ilkuwa atufanyie mchakato Wa kufungua kampuni brela na kuandika mkataba Wa kampuni
 
0753 125 474.....wanajamvi kuna huyu mdau kanitapeli na wadau wangu watatu tulimpa laki sita sita....wiki ya tatu sasa hapokei simu...na office yake magomen kafunga....alikuwa yanapatikana CRDB Lumumba nako imekuwa shida kumpata......ilkuwa atufanyie mchakato Wa kufungua kampuni brela na kuandika mkataba Wa kampuni

Weka na jina lake kabisa alilokuwa anajitangazia tumsake
 
Back
Top Bottom