Jinsi ya kumtongoza mwanamke club

Jinsi ya kumtongoza mwanamke club

Za jioni jamani,weekend ndo inaendelea hiyo Na Mimi nimeona bora niwakumbuke majembe yangu.
Kwa wale wenye mtoko Wa club au bar haya hapa mautundu yatakayo kuhakikishia kuondoka Na Mrembo
Utakayevutiwa naye.
Tusonge pamoja,

1.jiandaa
Usafi Na kuvalia kama MTU anaeenda Na wakati Ni muhimu sana.kumbuka unaenda kwenye halaiki ya watu tena club usivae kama unaenda kanisani au bungeni.
Unyunyu utakaokuwa Wa wastani utakupa maksi zaidi.

2.kuwa kidume
Haina maana upige watu,la,jiamini ukiwa club usikae nyuma au kwenye kona,nenda kaunta!!usiiname muda wote,nyanyua kifua,usikae kwa kujibana hakikisha unachukua eneo kubwa iwezekanavyo.

3.kuwa Na furaha.
Wanawake hawawapendi wanaume wenye huzuni,furahia maisha,hii itamvuta mwanamke kwako bila kujielewa!

4.anza kwa kumuangalia machoni
Hakikisha unakutanisha macho! Usimwangalie kama umebanwa Na mlango!!lainisha macho kisha angalia pembeni umpe nafasi ya kukuangalia vizuri, tabasamu!!,akitabasamu,tabasamu zaidi,mambo hayo!

5.Anza kumuandama
Hutakiwi kumfuata Moja kwa Mona alipokaa!msogeree kwa upandeupande la sivyo atakuona tishio!

6.Teka hisia za marafiki zake
Aghalabu demu huja Na rafikize club,jitambulishe pia wafahamu wao
Kuwa mcheshi.

7.muibe toka kwa marafiki zake!!.
Ili uweze kuzama zaidi utahitaji faragha!,omba kuongea nae kando au kama unaujuzi Wa kucheza mziki kama mose iyobo muombe mkacheze, huko unajua cha kufanya,waooo!
Au unaweza kusingizia hapo mlipokaa padogo!yap kisha wahamishie ktk himaya yako
Huko utakuwa huru zaidi
Kama kuchukua contacts Na mengine.

Hitimisho.
Ikiwa utacheza vizuri, kuongezea Na maujanja mengine uwezekano Wa kuosha rungu ni mkubwa sana siku hiyo hiyo!!

Kazi kwenu vidume.
Chaoo!

Hapo kwenye red mkuu ukate kiuno tena? ? Si atakuona kama Kaoge au James Delicious? ?
 
Umenikumbusha siku 1 niko high spirit nina stress zangu kilo 3 nakula bia mdogo mdogo. Mara nikaona mtoto mkali pembeni ametulia kutupa jicho vizuri tukakutana nae alikuwa ananiangalia. Nikampotezea. Baada ya muda nikaenda toilet narudi ktk ngazi nikamuona anashuka nikamsalimia akaitikia ila akawa speed nahisi alikuwa nae anaenda toilet. Basi nitarejea eneo langu kuendelea kugonga vitu vyangu. Mara akarudi akasogea karibu nilipokuwa mie. Wakati naongeza pack nyingine ya bia kutupa jicho akawa kama anataka kucheza lkn hana company n it's like hiyo nyimbo anaipenda. Mzee mzima nikasogea kwake nikamshika mkono tukadance sijui courage nilipata wapi cz unaweza kushushuliwa hivihivi. Basi mtoto tukacheza mdogo mdogo huku anatupia funda kidogo kidogo kinywaji chake. Note alikuwa anakunywa aina ya bia ninayokunywa Mimi pia. Wimbo ulipoisha nikasogeza ile ndoo ya bia zangu akachomoa moja tukaanza kugonga huku story za hapa n pale tukifahamiana. Mzigo kwenye ndoo ukaisha nikaagiza mwingine ukaisha akasema zikiisha ataagiza yeye. Kweli akaleta mzigo mezani huku ngoma kali ikigongwa tunacheza. Huku n huku nikamuuliza Mambo yake mengi akasema yuko chuo flani hapa town blah blah nyingine kibao. Nikachukua namba. Nikatulia. Mida mibovu nikataka kusepa. Akaniuliza Kama nina usafiri nikamwambia hapana nitampigia dereva m1 wa cab atakuja kunichukua mara akasema kwanini nikodi gari atanisukuma mpaka kkoo cz yeye anakaa magomeni. (She was driving) i was like fine from there nitachukua tax yoyote. Akanidrop akasepa. Nami nduki kwangu. Ile namba haikupatikana tena. Siku moja niko Liquid pale chang'ombe namuona mtu anafanya promotion za sigara fulani. Kaja mpaka kwangu anataka kuniuzia sigara ili anipe na zawadi ya lighter. Katika kuniconvince akanisogea karibu si ndio tukakutana macho kwa macho. Duh wacha aone aibu. Ikabidi aniachie lighter tu bure akasepa zake.
 
Hahaha huyu jamaa ananifurahisha na thread zake sana..Next time ufundishe jinsi ya kumtongoza demu mochwar
 
Back
Top Bottom