Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Kwa kweli Dar pazuri, pia ni pori ambalo ukiingia kila aina ya mti unapata na kila aina ya dawa unachimba.

Jamani Samsun Gallaxy Note 10 kwa laki5!

Kiukweli sielewi mwenzangu nawe uliichukua kwa mtu au ulichukua dukani brand new?

Maana mi mwaka 16 niliinunua not 8 kwa m2 cash!

Ninatamani sana hayo matoleo mapya yaliyofuatia!
Mkuu njoo nikuuzie galaxy s10 5g kwa 600k ina miezi 2 tu bado mpya kabisa
 
Mkuu MFALME WETU pole sana nimeumia sana sababu dunia ya sasa watu wema ni wachache sana sasa inapotokea mtu uwema unakukosti tena ndio huwa naumia sana

Mimi mwenyewe kama wewe tu yani nakuwaga na uzito sana kudai changu kwa marafiki. Mimi huwa nafikiria labda atajiongeza anilipe bila mimi kuanza pata Usumbufu wa kumdai.. Lakini cha ajabu ndio inakuwaga tofauti kabisa
Jamaa yangu nilipokuwa na kazi nikamuazima 200k kumdai nimeshindwa mpk sasa mwaka umeisha. Majuz kati ndio sijui amejistukia ananiuliza hivi unanidai sh ngapi nikamwambia me sikumbuki maana umepita mda mrefu sana sasa (huku moyoni nasema huyu jamaa Fala nn inamana hakumbuki deni analodaiwa au anajitoa fahamu) amekaa wee badae ananiambia ni laki mbili nmekumbuka ila ntakulipa kwa installment 100/100 😂😂. Me sikumjibu chochote ndio mara naona katuma mia, mia nyingine next month imagine after almost a year now bado deni inalipwa kwa installment 😭😭. Na jamaa usifikiri labda ni jobless nop... muajiriwa kabisa tena kwenye taasisi moja inaheshimika sana ya kiserikali sasa huwa najiuliza hivi ni makusudi au shida nn?

Na sahivi nilivokuwa jobless ndio nahamaki kabisa nikikumbuka hela hyo bs tu sababu ni friend wa muda mrefu not less than 10 yrs.
 
Huyu jamaa ananitia hasira sana jamani nais ntamfanya kitu kibaya.

Kuna siku nilipost nauza simu yangu [Samsung Note 10+] kule kwenye jukwaa la matangazo maana nilikua siitumii sasa kwenye harakati za kutafuta mteja nikaamua kumshirikisha huyu rafiki yangu akadai nimuuzie.

Nikasema fresh haina shida ila nikampa condition aje na pesa yote cash maana masuala ya kudaiana hela siyawezi akasema sawa.

siku anakuja kuchukua simu ilikua tarehe 18 December 2022 nakumbuka alinipigia simu kuniuliza nilipo nikamwambia nipo Oysterbay bar xxxxxx akanambia anatokea kuja kuchukua simu kama tulivokubaliana nikamwambia sawa ila sipo nayo apa ipo nyumbani.

Ikabidi nimuunganishe na dogo langu pale home ampe jamaa simu mi nikaendelea kumwagilia moyo.

To cut the long story short

Mshikaji alienda akalipa hela nusu ya tuliokua tumekubaliana 250k/500k.. kwa kuwa dogo anamjua jamaa ni rafiki yangu hakuona haja ya kunijulisha jinsi transaction ilivoenda akampa jamaa simu akaishia zake.

Sasa kesho yake dogo ananikabidhi pesa ndo nagundua jamaa kanifanyia uhuni contrary na makubaliano yetu akanipiga sound kuwa atanilipa hela iliyobakia before 25th December 2022, nikamwambia fresh ila nikamsisitiza anilipe iyo hela maana kashaenda kinyume na makubaliano akasema sawa nisiwaze.

Ilivofika tarehe 25 sikumcheki maana mambo yalikua mengi ukizingatia ni sikukuu nikajua atajiongeza lakini wapi. Nikamcheki tarehe 27 akanambia hajapata hela nimsikilizie akisain boom atanilipa hela yangu yote nikasema fresh..kasain boom tarehe 09 January kumcheki akawa hajibu text wala kupokea simu. Akaja kunijibu kesho yake kuwa hela ya boom yote kalipa kodi ya nyumba hela imeisha akaniahidi nimvumilie aombe hela nyumbani anilipe.

Baada ya apo napigishwa sound kama mtoto tena mjinga nisiejielewa, sijalipwa ata mia na nikimpigia simu hapokei na akipokea anajibu kwa kujihami sana plus text zenyewe ndo anajibu kama hivi jamani pesa yangu mwenyewe inanitesa [emoji22][emoji22]

Watu kama hawa tunadeal nao vp au nivae roho ya unyama nikodi polisi nimuibukie anapokaa nichukue simu yangu then nivunje urafiki.

Kinachoniuma ananijibu kwa dharau sana na anajibu au kupokea simu kwa kujiskia na hajanilipa hata mia kwenye hio hela iliyobakia[emoji22][emoji22]

Nina muda mrefu sana sijawa na stress kias hiki.

Ingekua mchana ndo kanijibu hivi huyu dogo leo angejuta ashukuru Mungu ntaamka hasira zikiwa zimeisha.

Naombeni ushauri na mbinu za kuweza kupata hii hela au simu kutoka kwa huyu rafiki yangu[emoji120]

Mnisamehe kwa uandishi wangu mbovu maana huyu jamaa kanivuruga sana View attachment 2507621
Mpe 250 yake chukua simu yako simple tu
 
Nilikua na kisamsung J7 pro nikakiangusha kikavujia wino nikawaza kubadili kioo nikaona hapana. Kuna fundi simu namjua miaka mingi namuamin nikampa ile simu nikamuambia nitafutie mteja wewe kama utabadili kioo ama utauza kama skrepa utajua wewe ila utanipa kiasi kadhaa. Siku zinazienda nikagundua kabadili kioo anaitumia yeye ile simu nikakausha. Muda unaenda jamaa kimya mtaan kwangu kuna bro siku akaniambia anaitaka ile simu nimuachie, nikamchek jamaa bwana siku zinakata kama simu haiuziki nipe hivyo hivyo kuna mtu anaitaka akaanzaga kutojibu sms wala simu.

Badae akaja akaniblock yaan simu yangu alafu anaitumia hyo hyo kuniblock nikasema hamna noma. Kuna siku nilitimba ofisin kwake nadhani alinifahamu vizuri nilikiwasha nilimjazia nzi hadi alianza kulia nikamuuliza unajua wap nmetoa hela ya kununua hicho kimeo alafu mwanaume mzma unavimba unatumia simu yangu na hela kutoa hutak, kurudisha simu hutaki mbona alinilipa. Hatuongei hadi leo nampitaga kama kisiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida yake ndio hapo sasa mnakuwa maadui wakubwa 😂😂
 
Kwa kweli Dar pazuri, pia ni pori ambalo ukiingia kila aina ya mti unapata na kila aina ya dawa unachimba.

Jamani Samsun Gallaxy Note 10 kwa laki5!

Kiukweli sielewi mwenzangu nawe uliichukua kwa mtu au ulichukua dukani brand new?

Maana mi mwaka 16 niliinunua not 8 kwa m2 cash!

Ninatamani sana hayo matoleo mapya yaliyofuatia!
Note 10+ bei yake dukani saiv ni 550k [used]
 
Inshu ya urafiki ni ngumu sana mimi nnajamaa yangu askali na kazulumiwa million 3 na rafiki yake na hana cha kumfanya anaishia kunung'unika tu pembeni lakini sio km kumpga hawezi wala kutumia nguvu uwezo anao lakini ananuna tu akikutana na jamaa anatoa macho hila akifanyiwa ujinga na watu tofauti balaa lake sio poa urafiki labda mmekutana ukubwani unaweza kumbadilikia hila wa tangu utotoni huwezi.
 
Nilikua na kisamsung J7 pro nikakiangusha kikavujia wino nikawaza kubadili kioo nikaona hapana. Kuna fundi simu namjua miaka mingi namuamin nikampa ile simu nikamuambia nitafutie mteja wewe kama utabadili kioo ama utauza kama skrepa utajua wewe ila utanipa kiasi kadhaa. Siku zinazienda nikagundua kabadili kioo anaitumia yeye ile simu nikakausha. Muda unaenda jamaa kimya mtaan kwangu kuna bro siku akaniambia anaitaka ile simu nimuachie, nikamchek jamaa bwana siku zinakata kama simu haiuziki nipe hivyo hivyo kuna mtu anaitaka akaanzaga kutojibu sms wala simu.

Badae akaja akaniblock yaan simu yangu alafu anaitumia hyo hyo kuniblock nikasema hamna noma. Kuna siku nilitimba ofisin kwake nadhani alinifahamu vizuri nilikiwasha nilimjazia nzi hadi alianza kulia nikamuuliza unajua wap nmetoa hela ya kununua hicho kimeo alafu mwanaume mzma unavimba unatumia simu yangu na hela kutoa hutak, kurudisha simu hutaki mbona alinilipa. Hatuongei hadi leo nampitaga kama kisiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole aisee mi roho ngumu kama hii ndo sina jamani sjui natoa wap nguvu ya kumjazia mtu inzi maana pesa zangu nyingi zipo kwa washkaji na ndugu, kuna time nakua napelewa pesa ya kufanya kitu flani nawaza izo hela ila nafkia hatma ya kuzikaushia tu nikijua watajiongeza lkn wapii[emoji22]
 
Fanya sacrifice, mwambie ni maisha tu abaki na hela hiyo. Ila unamfuta kwenye circle yako. Kata hadi mawasiliano ya salam na mazoea yoyote. Focus nishati na mawazo yako kwenye vitu vyako vingine. Mungu atafanya kitu kwako.
 
Inabidi ifike wakati uache hizo huruma zako vinginevyo watu watakusumbua sana. Mm ni mpole sana lkn huu ukorofi watu wa hovyo ndio walinifundisha sababu ukikaa kilege lege wanakuchezea. Weka upole pembeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inshu ya urafiki ni ngumu sana mimi nnajamaa yangu askali na kazulumiwa million 3 na rafiki yake na hana cha kumfanya anaishia kunung'unika tu pembeni lakini sio km kumpga hawezi wala kutumia nguvu uwezo anao lakini ananuna tu akikutana na jamaa anatoa macho hila akifanyiwa ujinga na watu tofauti balaa lake sio poa urafiki labda mmekutana ukubwani unaweza kumbadilikia hila wa tangu utotoni huwezi.
huyu jamaa tumekuwa marafiki since tuko na miaka 17 mpaka saiv kwakweli nifikiria jinsi ya kudeal nae nais tu kuchanganyikiwa ndio maana nilkuja kuomba ushauri uku nipate mawazo ya wadau[emoji848] ndo mtu pekee nilkua namchukulia kama rafiki yangu.. yeye peke yake🥲
 
Fanya sacrifice, mwambie ni maisha tu abaki na hela hiyo. Ila unamfuta kwenye circle yako. Kata hadi mawasiliano ya salam na mazoea yoyote. Focus nishati na mawazo yako kwenye vitu vyako vingine. Mungu atafanya kitu kwako.
Ni ngumu sana mkuu ukizingatia ndo rafiki pekee nlokua nae sina mwingine zaid ya washkaji tu🥲

Asante kwa ushauri lakin[emoji120]
 
Mkaushie halafu uwe kama umempotezea siku muombe msaada
Sinaga tabia ya kuomba msaada wa pesa mkuu sanasana yeye ndo huwa namsaidia maana bado yupo chuo.. ukiona nmeomba hela kwa mtu ujue ni sh 100 au 200 ya kuongezea kununua kifurushi na sio vinginevyo.

Bongo watoa misaada ni wachache sana zaidi tu utaishia kuanika shida zako na kudhalilika. Nishaacha izo mambo muda mrefu, labda nimwombe msaada mwingine tofauti na hela ukizingatia suala la hela ndo tunazungushana ivi je nikipata shida nikamwomba pesa atanisaidia kweli🥲
 
Back
Top Bottom