Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Mkuu kwanza pole kwa hili sakata.

Kwa mujibu wa hizi sms zenu, majibu yake yanaonesha hiyo pesa ndio imetoka ntolee hatorudisha tena.

Mlikubaliana umuuzie kwa 500k, ila alipokukosa na ukamdirect kwa mdogo wako hili ndio lilikua kosa la kimkakati. Alitumia mwanya huo kufanya hujuma yake.

Baada ya kupata simu alishaamua liwalo na liwe,hata urafiki ukivunjika mkawa maadui basi yeye atakua ametoka na kitu kwenye huo urafiki wenu, yaani yeye atakua winner na ww utakua mpotezaji.

Kabla sijakushauri je una txt zinazoonesha makubaliano yenu kwamba simu utamuuzia kwa 500k?
Bora wewe rafiki alafu ni mdogo mimi namdai dada yangu 1.5 milioni ni story ndefu ila kwa kifupi alinipiga.. upande mmoja nasema nipotezee tu maana ni ndugu upande mwingine hela yangu inaniuma ila kumchana noma
 
Kodi polisi mpe hata 100k chukua simu yako na dogo usimrudishie hata sh. 100
Polisi ata 10k wanachukua mkuu ina depend tu na polisi mwenyewe, nishawakodi sana kipindi niko mkoa flani ni vile tu huyu dogo tumekua marafiki muda mrefu sana nashindwa kumpigia mahesabu makali
 
Bora hata ww anajibu sms zako.Yaan mimi story yako ipo kama ya kwangu kwenye muda sema utofaut wake ni kwamba jamaa aliomba nimkopeshe elfu 50 tu.Mpaka sasa hapokei simu zangu till now na nina hasira balaa.Kila mara nawaza nimfanye nini maana ni rafiki yangu sana.
 
[emoji1787][emoji1787]dah wabongo nuks.kunamshkaji sio rafikiyangu ila imetokea kuwa karibu nae kwakua nafahamiana na kakaake.sasa kunakazi kakaake kamlengesha kwangu ili nimfanyie ilichukua Kama sikumbili.
msenge anakuja ofisini nademu wake kuangalia kazi inavyo enda anashinda hapohapo kazini.nikajiuliza kwanini huyu msenge haendi namrembo kula Bata kazi kukaatu ofisini kwangu wakati viwanja unavuka barabara tuu unaenda kuinjoi

kumbe mshkaji Hana hata mia hela ya vifaa yenyewe anaunga unga ila ukimcheki bonge labosi kumbe tapeli

picha inaanza kazi imeisha nadai changu anasema ngoja kunamtu ananitumia.badae akaniambia nipe msaidizi wako twende sehemu akachukue Nampa msaidizi wangu aende nae mara ananiambia nitakutumia[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]tangu mwaka Jana mwezi wa6 hadileo hajanilipa.laki 7 yangu ilanajua iposiku atakuja tuu.
Daah 700k kwenye business ni loss kubwa mno mkuu pambana nae akulipe iyo hela
 
Bora hata ww anajibu sms zako.Yaan mimi story yako ipo kama ya kwangu kwenye muda sema utofaut wake ni kwamba jamaa aliomba nimkopeshe elfu 50 tu.Mpaka sasa hapokei simu zangu till now na nina hasira balaa.Kila mara nawaza nimfanye nini maana ni rafiki yangu sana.
Hawa marafiki kwakweli dawa yao inachemka🥲
 
Polisi ata 10k wanachukua mkuu ina depend tu na polisi mwenyewe, nishawakodi sana kipindi niko mkoa flani ni vile tu huyu dogo tumekua marafiki muda mrefu sana nashindwa kumpigia mahesabu makali
We sasa hivi mfanyie tu roho mbaya ajue uko serious na hela yako then akili itamkaa sawa otherwise hela yako hupewi na dogo atakufanyia jeuri zaidi na zaidi
 
Chukua ubani Mashtakhaa
choma unuie " Kama mimi Ditto nguku bendu wa zabanga hii simu Samsung Note 10 niliinunua kwa jasho langu na nmedhurumiwa, ikiwa ni haki yangu ntaipata kama sio haki Inshaallah"

afu potezea
mshukuru Mwenyezi Mungu Allah subhanah wa Taala
😅😂
 
Huyu jamaa ananitia hasira sana jamani nais ntamfanya kitu kibaya.

Kuna siku nilipost nauza simu yangu [Samsung Note 10+] kule kwenye jukwaa la matangazo maana nilikua siitumii sasa kwenye harakati za kutafuta mteja nikaamua kumshirikisha huyu rafiki yangu akadai nimuuzie.

Nikasema fresh haina shida ila nikampa condition aje na pesa yote cash maana masuala ya kudaiana hela siyawezi akasema sawa.

siku anakuja kuchukua simu ilikua tarehe 18 December 2022 nakumbuka alinipigia simu kuniuliza nilipo nikamwambia nipo Oysterbay bar xxxxxx akanambia anatokea kuja kuchukua simu kama tulivokubaliana nikamwambia sawa ila sipo nayo apa ipo nyumbani.

Ikabidi nimuunganishe na dogo langu pale home ampe jamaa simu mi nikaendelea kumwagilia moyo.


To cut the long story short

Mshikaji alienda akalipa hela nusu ya tuliokua tumekubaliana 250k/500k.. kwa kuwa dogo anamjua jamaa ni rafiki yangu hakuona haja ya kunijulisha jinsi transaction ilivoenda akampa jamaa simu akaishia zake.

Sasa kesho yake dogo ananikabidhi pesa ndo nagundua jamaa kanifanyia uhuni contrary na makubaliano yetu akanipiga sound kuwa atanilipa hela iliyobakia before 25th December 2022, nikamwambia fresh ila nikamsisitiza anilipe iyo hela maana kashaenda kinyume na makubaliano akasema sawa nisiwaze.

Ilivofika tarehe 25 sikumcheki maana mambo yalikua mengi ukizingatia ni sikukuu nikajua atajiongeza lakini wapi. Nikamcheki tarehe 27 akanambia hajapata hela nimsikilizie akisain boom atanilipa hela yangu yote nikasema fresh..kasain boom tarehe 09 January kumcheki akawa hajibu text wala kupokea simu. Akaja kunijibu kesho yake kuwa hela ya boom yote kalipa kodi ya nyumba hela imeisha akaniahidi nimvumilie aombe hela nyumbani anilipe.

Baada ya apo napigishwa sound kama mtoto tena mjinga nisiejielewa, sijalipwa ata mia na nikimpigia simu hapokei na akipokea anajibu kwa kujihami sana plus text zenyewe ndo anajibu kama hivi jamani pesa yangu mwenyewe inanitesa [emoji22][emoji22]

Watu kama hawa tunadeal nao vp au nivae roho ya unyama nikodi polisi nimuibukie anapokaa nichukue simu yangu then nivunje urafiki.

Kinachoniuma ananijibu kwa dharau sana na anajibu au kupokea simu kwa kujiskia na hajanilipa hata mia kwenye hio hela iliyobakia[emoji22][emoji22]

Nina muda mrefu sana sijawa na stress kias hiki.

Ingekua mchana ndo kanijibu hivi huyu dogo leo angejuta ashukuru Mungu ntaamka hasira zikiwa zimeisha.

Naombeni ushauri na mbinu za kuweza kupata hii hela au simu kutoka kwa huyu rafiki yangu[emoji120]

Mnisamehe kwa uandishi wangu mbovu maana huyu jamaa kanivuruga sana View attachment 2507621
Kwa kweli Dar pazuri, pia ni pori ambalo ukiingia kila aina ya mti unapata na kila aina ya dawa unachimba.

Jamani Samsun Gallaxy Note 10 kwa laki5!

Kiukweli sielewi mwenzangu nawe uliichukua kwa mtu au ulichukua dukani brand new?

Maana mi mwaka 16 niliinunua not 8 kwa m2 cash!

Ninatamani sana hayo matoleo mapya yaliyofuatia!
 
Halafu kanaandika kipumbavu sana
Chukua hatua kali. Mletee noma, unakuaje na urafiki na mtu anaandika sms namna hiyo? Hiyo ni indication tosha kuwa ni kamtu kapumbavu.
Mtoto mdogo anakusuambaje?
Na wewe zembe..nakupa za uso.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]!
 
Anakumudu huyo ndio maana ana ujasiri wa kukujibu kwa nyodo hivyo.
Inaonekana wewe ni mpole mpole hivi hivyo ana hakika huwezi kumfanya kitu.

Jifanye umempotezea kwa muda kumdai. Kama baada ya wiki 2 mualike sehemu mkutane bila kukumbushia deni.
Akija chukua simu uzuge kuangalia, ukiitia mkononi ondoka nayo. Mwambie amalizie deni umpe simu au kama unayo pesa yake aliyotoa mrudishie uchukue simu yako.
Mkuu walikofikia huo mtego hauwezekani tena.

Je kwa mfano akamwalika asije na hiyo simu?

Mbinu alizodhamiria mwenyewe namna ya kumbamba kwangu naona ndiyo sahihi.
 
Back
Top Bottom