Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Jinsi ya kumdai rafiki yako hela

Nenda na na polisi

Huyo mshenzi kashakudharau.

Huyo sio rafiki usimuute rafiki Hana hata chembe ya urafiki usijipendekeze kwakwe.

Inakera sana mzee fanya haraka.

Wachukue polisi wawili wapooze hata na kilo wewe ubaki na 150k
Asante kwa ushauri mkuu, ndo option pekee nlobaki nayo ntaifanyia kazi [emoji120]
 
Sio rahisi hivyo kama unavyoandika hapa...wewe ungefanyaje? Mtu anajibu kwa sms unampiga humo kwny simu?? Je atamkuta mahali anapotarajia au anapoishi? Hakuna kitu kigumu kama kudai...
Kuhusu uandishi nilimaanisha ana uandishi wa kuashiria ni mtu mjingamjinga. Kwa mazingira aliyoelezea mleta mada ni dhahiri anajua wapi pa kumpata mtu wake. Huyu sio stranger kusema hana abc za wapi atampata. Kwa maelezo yake ni rahisi kumfikia.
Njia ni nyingi za kumnasa akanasika.
 
Mkuu pole sana aisee nimejifunza kutoamini Rafiki wa karibu wala ndugu.

Kwa mimi nilishawahi kukosana na rafiki yangu wa kiti cha kwanza kabisa, kisa ilikua ni madaiano kama wewe ivo ivo, sema alileta pigo za ki-friendly mpaka kwenye busness nikaamua kumtolea uvivu kila mtu ale hamsini zake sahivi Anajuta uko aliko.

Marafiki na ndugu ni wakuchunga sana kwenye biashara uwa Wanaji-less sana aisee
Tunajifunza kutokana na makosa mkuu namimi nimejifunza kutomwamini mtu zaidi ya nafsi yangu tu[emoji120]
 
Kuhusu uandishi nilimaanisha ana uandishi wa kuashiria ni mtu mjingamjinga. Kwa mazingira aliyoelezea mleta mada ni dhahiri anajua wapi pa kumpata mtu wake. Huyu sio stranger kusema hana abc za wapi atampata. Kwa maelezo yake ni rahisi kumfikia.
Njia ni nyingi za kumnasa akanasika.
Kumpata sio ishu kabisa mkuu, shida ni maamuzi ya kuchukua baada ya kumpata ukizingatia ni marafiki wa muda mrefu sana apo ndo kizungumkuti kinapoanzia🥲
 
Police tutazungushana mkuu, mi naona bora nikodi polisi nimlipe 50k nikachukue simu yangu kila mtu ale hamsini zake
Wazo pekee mtafute Polisi mlengeshe kwa Jamaa hata apate mushkeli kwa wa ndani kwa masaaa 3 then muandikishane kua unaichukua simu kwa muda till akimalizia helake then unamrudishia mbele ya Kamanda huku anakua ashapata mabanzi ya kutosha.

Si vizuri kukopesha marafiki, ni vizuri kusadiana kwa kidogo tulichonacho mfano kama rafiki anaomba laki na wewe unajua katika bajeti yako extra ni 10k, then unampa hiyo extra ambapo arudishe au asirudishe kwako haina madhara
 
Mie nakushauri umsamehe, achana naye kabisa we' endelea na mishemishe zako zingine, najua ni ngumu lakini jifanye kama umepoteza, au umetoa sadaka au umemnunulia Girl friend wako zawadi fulani. Wewe ni kijana wa kiume, na unajua wakati mwingine kuna vitu tunakosea au tuna mis calculate maishani mwetu, chukulia kwamba umekosea, umejifunza na endelea na maisha mengine. Mweleze Mungu akuongoze kwenye hili na yaliyobaki yote mwachie yeye. Ninayokueleza nimeyajaribu na inafanya kazi, na imesaidia sana kupunguza stress na hasira. lakini pia kusamehe kuna sana faida kiroho na kiafya kwako wewe.
 
Mie nakushauri umsamehe, achana naye kabisa we' endelea na mishemishe zako zingine, najua ni ngumu lakini jifanye kama umepoteza, au umetoa sadaka au umemnunulia Girl friend wako zawadi fulani. Wewe ni kijana wa kiume, na unajua wakati mwingine kuna vitu tunakosea au tuna mis calculate maishani mwetu, chukulia kwamba umekosea, umejifunza na endelea na maisha mengine. Mweleze Mungu akuongoze kwenye hili na yaliyobaki yote mwachie yeye. Ninayokueleza nimeyajaribu na inafanya kazi, na imesaidia sana kupunguza stress na hasira. lakini pia kusamehe kuna sana faida kiroho na kiafya kwako wewe.
Asante kwa ushauri mkuu, huwa nasamehe sana vitu na kumove on tatizo dogo kanichukulia poa full dharau kwa sana icho ndo kitu kinachoniumiza[emoji22][emoji22]
 
Mie kwanza nina nuksi na ninajijua nina nuksi nikikopesha silipwi na nikikopa sipewi,, na nikimuamini mtu naishia kulizwa.

Jana nilikuwa na shida ya 20 nijazie niwe na laki nipeleke pahala looh nilisota na sikupata[emoji16],

Shoga yangu akaja kunikopa hile 80 kwa madai atanipa jioni nikampa lkn hadi leo kimya, nilimpa na ninashida zaidi yake,
 
Kama hana risiti nenda polisi wape mchongo wao wale na wewe urudishiwe simu na 250k aliyokupa itakuwa zawadi yako.
 
Asante kwa ushauri mkuu, huwa nasamehe sana vitu na kumove on tatizo dogo kanichukulia poa full dharau kwa sana icho ndo kitu kinachoniumiza[emoji22][emoji22]
1. Samehe hiyo hela.
2. Kata mazoea naye yoyote yale(unaelewa sijui nikisema KATA? Kata kwa kumaanisha).
3. Usije ukarudi nyuma na kumrudisha kwenye circle yako.
4. Ikitokea akakulipa ipokee hiyo hela kama unapokea kutoka kwa mteja tu au mtu usiyemfahamu.
5. Mind your own business, mfute kabisa kwenye kila angle!
 
Hakika mimi ni mpole na nina huruma sana na sio kuwa najisifia, suala la kuchukua maamuzi magumu lilishanishinda ila naona linaniponza inabidi nilitaftie tiba.

Kuna uzi nilipost kule mmu kuwa natafuta rafiki wa kike wote waliokuja pm hawakukidhi vigezo nilivokua naitaji. But karibu, njo ujinufaishe na upole wangu Unique Flower [emoji28]
Vigezo vipi hivyoo??😆naogopa kuweka emji za love naogopa
 
1. Samehe hiyp hela.
2. Kata mazoea naye yoyote yale(unaelewa sijui nikisema KATA? Kata kwa kumaanisha).
3. Usije ukarudi nyuma na kumrudisha kwenye circle yako.
4. Ikitokea akakulipa ipokee hiyo hela kama unapokea kutoka kwa mteja tu au mtu usiyemfahamu.
5. Mind your own business, mfute kabisa kwenye kila angle!
Ushauri mzuri sana mkuu. Shukran [emoji120]
 
Kesi iyo..

Mi nishaachana na madogo wapumbavu kama hao wengine eti anakuzungusha ikipita mwaka anahisi umesahau anakuja Tena kwa shida ..Hivi karibu jamaa jirani nimempa 30k achukue ishu fulani maana anauza chips aliniambia trh 20 December atanipa ila mpaka leo hajanilipa na Yale mawasiliano ya awali kakata ..

Dunia Ina tatizo hili la kutokuwa muaminifu sijui kwa nn..
Hahahahahah ukitaka kugombana na mtu dai chako 🤣🤣🤣
 
Huyu jamaa ananitia hasira sana jamani nais ntamfanya kitu kibaya.

Kuna siku nilipost nauza simu yangu [Samsung Note 10+] kule kwenye jukwaa la matangazo maana nilikua siitumii sasa kwenye harakati za kutafuta mteja nikaamua kumshirikisha huyu rafiki yangu akadai nimuuzie.

Nikasema fresh haina shida ila nikampa condition aje na pesa yote cash maana masuala ya kudaiana hela siyawezi akasema sawa.

siku anakuja kuchukua simu ilikua tarehe 18 December 2022 nakumbuka alinipigia simu kuniuliza nilipo nikamwambia nipo Oysterbay bar xxxxxx akanambia anatokea kuja kuchukua simu kama tulivokubaliana nikamwambia sawa ila sipo nayo apa ipo nyumbani.

Ikabidi nimuunganishe na dogo langu pale home ampe jamaa simu mi nikaendelea kumwagilia moyo.


To cut the long story short

Mshikaji alienda akalipa hela nusu ya tuliokua tumekubaliana 250k/500k.. kwa kuwa dogo anamjua jamaa ni rafiki yangu hakuona haja ya kunijulisha jinsi transaction ilivoenda akampa jamaa simu akaishia zake.

Sasa kesho yake dogo ananikabidhi pesa ndo nagundua jamaa kanifanyia uhuni contrary na makubaliano yetu akanipiga sound kuwa atanilipa hela iliyobakia before 25th December 2022, nikamwambia fresh ila nikamsisitiza anilipe iyo hela maana kashaenda kinyume na makubaliano akasema sawa nisiwaze.

Ilivofika tarehe 25 sikumcheki maana mambo yalikua mengi ukizingatia ni sikukuu nikajua atajiongeza lakini wapi. Nikamcheki tarehe 27 akanambia hajapata hela nimsikilizie akisain boom atanilipa hela yangu yote nikasema fresh..kasain boom tarehe 09 January kumcheki akawa hajibu text wala kupokea simu. Akaja kunijibu kesho yake kuwa hela ya boom yote kalipa kodi ya nyumba hela imeisha akaniahidi nimvumilie aombe hela nyumbani anilipe.

Baada ya apo napigishwa sound kama mtoto tena mjinga nisiejielewa, sijalipwa ata mia na nikimpigia simu hapokei na akipokea anajibu kwa kujihami sana plus text zenyewe ndo anajibu kama hivi jamani pesa yangu mwenyewe inanitesa [emoji22][emoji22]

Watu kama hawa tunadeal nao vp au nivae roho ya unyama nikodi polisi nimuibukie anapokaa nichukue simu yangu then nivunje urafiki.

Kinachoniuma ananijibu kwa dharau sana na anajibu au kupokea simu kwa kujiskia na hajanilipa hata mia kwenye hio hela iliyobakia[emoji22][emoji22]

Nina muda mrefu sana sijawa na stress kias hiki.

Ingekua mchana ndo kanijibu hivi huyu dogo leo angejuta ashukuru Mungu ntaamka hasira zikiwa zimeisha.

Naombeni ushauri na mbinu za kuweza kupata hii hela au simu kutoka kwa huyu rafiki yangu[emoji120]

Mnisamehe kwa uandishi wangu mbovu maana huyu jamaa kanivuruga sana View attachment 2507621
Mtu unamdai halafu anakukazia namna hii, sijawahi kuona hilo.
 
Huna rafiki tena futa hilo haraka huko kichwani. Nilikuwa na mtu wa aina hio nilimfutaga mpaka kesho haamini na nilishamfanyia favour kibao kama ndugu. Alikujaga kuniletea dharau za kichoko sana
huyu jamaa tumekuwa marafiki since tuko na miaka 17 mpaka saiv kwakweli nifikiria jinsi ya kudeal nae nais tu kuchanganyikiwa ndio maana nilkuja kuomba ushauri uku nipate mawazo ya wadau[emoji848] ndo mtu pekee nilkua namchukulia kama rafiki yangu.. yeye peke yake🥲
 
Back
Top Bottom