G-Funk
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 2,397
- 5,561
Bora hata mwamba anakulipa hata kwa installment. Watanzania wengi matapeli.
Mkuu MFALME WETU pole sana nimeumia sana sababu dunia ya sasa watu wema ni wachache sana sasa inapotokea mtu uwema unakukosti tena ndio huwa naumia sana
Mimi mwenyewe kama wewe tu yani nakuwaga na uzito sana kudai changu kwa marafiki. Mimi huwa nafikiria labda atajiongeza anilipe bila mimi kuanza pata Usumbufu wa kumdai.. Lakini cha ajabu ndio inakuwaga tofauti kabisa
Jamaa yangu nilipokuwa na kazi nikamuazima 200k kumdai nimeshindwa mpk sasa mwaka umeisha. Majuz kati ndio sijui amejistukia ananiuliza hivi unanidai sh ngapi nikamwambia me sikumbuki maana umepita mda mrefu sana sasa (huku moyoni nasema huyu jamaa Fala nn inamana hakumbuki deni analodaiwa au anajitoa fahamu) amekaa wee badae ananiambia ni laki mbili nmekumbuka ila ntakulipa kwa installment 100/100 😂😂. Me sikumjibu chochote ndio mara naona katuma mia, mia nyingine next month imagine after almost a year now bado deni inalipwa kwa installment 😭😭. Na jamaa usifikiri labda ni jobless nop... muajiriwa kabisa tena kwenye taasisi moja inaheshimika sana ya kiserikali sasa huwa najiuliza hivi ni makusudi au shida nn?
Na sahivi nilivokuwa jobless ndio nahamaki kabisa nikikumbuka hela hyo bs tu sababu ni friend wa muda mrefu not less than 10 yrs.