Mlima simba
JF-Expert Member
- Dec 28, 2017
- 3,707
- 6,628
Nakujibu mimi..hakuna mwanasiasa aliyezuiliwa kufanya mikutano..na wanasiasa wote wanafanya kazi na mikutano kwenye majimbo yao ya uchaguzi..kilichozuiliwa ni tabia ya wanasiasa kutoka eneo moja kwenda jingine ambapo ni kituo cha kazi cha mwingine..lengo ni kuruhusu mazingira ya utendaji ya mwingine na pia kuzuia vurugu..
Hatua za ununuzi wa ndege zilipitia michakato halali..bungeni kuna kamati ya bajeti na miundi mbinu..hizo zilipitisha..si lazima zipitishwe kwa kelele
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umejibu vizuri sana, naomba unijuze jimbo ambalo Vicent Mashinji wa Chadema anaweza kufanya mkutano na ni jimbo lake pasipokukamatwa na police maana yeye kutwa kukamatwa ila pole pole anadunda tu na anazunguka nchi nzima pamoja na doctor Bashiru.
Vivyo hivyo naomba nitajie jimbo La pole pole au doctor Bashiru ambalo kwao wote ni haki yao na ni majimbo yao ya kufanyia siasa.
Lingine kila mwanasiasa anatakiwa afanye siasa kwenye jimbo lake ndicho katika katiba yetu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyotuelekeza au ni matakwa tu ya mtu??
Mkuu nilikuwa sijui kuwa kamati husika inaweza tunga sheria na kuipitisha bila kujadiliwa na wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania na ikawa sheria .
Nimesema hivyo kutokana na kamati yako ya bunge iliyopitisha bajeti ya ujenzi wa uwanja wa chato na hiyo hiyo kamati kuidhinisha ununuzi wa ndege kwa malipo ya fedha taslimu.