SHANTI
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 296
- 365
Niliposikia Makonda Kateuliwa kuwa mwenezi wa CCM nilisema wamepata mtu wa kazi na mwenye sauti ya kukisemea cha chama cha Mapinduzi ,ila niayoyaona Makonda anakwenda kuvuruga weledi wa watendaji wa Kazi seriaklini kwa kofia ya kumsemea Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Tujiulize maswali machache?
(1) Makonda anamhoji kamishina wa TRA? au mtumishi wa umma mwenye mamlaka yeyote kwa hadhi gani? wakati mamlaka ya Uteuzi ya mtendaji wa Serikali sio chama cha mapinduzi?
-Mfano: kuna wakati wenyeviti wa CCM walikuwa wanafanya mchezo kama wa makonda wakawa wana waonea madkatari mpaka ikabidi itoke kauli kuwataka viongozi wa chama wasiiingilie majukumu ya taaluma zisizo wahusu kwa sababu wanaleta mkanganyiko.
Vuta Taswira umeajiriwa Tamisemi .TCRA,sijui wapi huko halafu unawajibishwa na katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi? huuu si mzaha unaopitiliza, Job Description haisemi kwamba utawajibika kwa katibu wa CCM inasema utawajibika kwa mamlaka iliyokuteua, hapa elewa neno mamlaka iliyokuteua?
(2) Je, Rais umemkambidhi mamlaka yako Bwana Makonda? Maana anaingilia kila sekta na anatoa maagizo na kuleta mkanganyiko usio na Tija?
Mfano: Mama Samia yeye ni Rais , wa Nchi kiongozi mkuu na M/kiti wa CCM. Akitembelea mradi kwa kofia ya Rais ana mamlaka kamili ya kuwajibisha mtendaji wa serikali kwa sababu yeye ndiye mkuu wa nchi. Vivyo hivyo kwa makamu wa Rais , Waziri mkuu na watendaji wakuu wa serikali inaswihi.
(3) Nauliza Tena mama umemtuma Makonda kwenda kuwaruga watendaji wako wa serikali? washike lipi sasa? Vipi waendelee kupokea maagizo ya makonda au watekeleze mahitaji ya J.D za kazi zao?
(4) Nauliza tena mama wewe hauoni kuna mkanganyiko unaenda kutokea kwa watendaji walio chini yako, hauoni huyu anakwenda kuwachonganisha watendaji na mamlaka zao za kuwajibika? ni kweli watendai na mawaziri wafanye presentation ofisi za chama ?
Ndio maana nauliza umemtuma kueneza itikadi ya chama au kuwavuruga watendaji wa seriakli?
Usipoziba ufa utajenga ukuta, nashauri tu aendelee kukisemea chama ila ajiweke mbali na shughuli za serikali, huyu mtu atabeba majukumu ya cheo chako kwa kivuli kukisemea chama kukusemea wewe Mh. Rais na mwishowe watendaji wataaacha kufanya kazi. Nchi ilikuwa imetulia sasa mmeamua kuwaruga utavuna mlichopanda kwa Makonda.