Kama watanzania, tusikubali kurubuniwa na vyama vya siasa au wanasiasa. Chambua kila suala kwa kina na bila upendeleo

DaudiAiko

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
302
274
Wanabodi,

Jamii yoyote inaweza kulaaniwa na Mwenyezi Mungu au kulogwa na ibilisi. Mapenzi yangu kwa watanzania yanaweza yakawa yamezidi hata katika kipindi ambacho ishara zote zimeshindwa kuni pumbaza, hata katika kipindi ambacho matukio yanazidi kuthibitisha kwamba imani bila hatua thabiti ni batili.

Hata kama umeamua kununa au kujiuliza maswali mengi, ni vyema kutambua kwamba siku zote, fikra njema huzaa maamuzi yenye baraka. Tusijidangaye kwamba fikra njema huokotwa baharini, bali fikra njema na zenye uwezo wa kuleta tija na matokeo chanya hulenga kutatua changamoto bila upendeleo wowote.

Haya bwana, hili lisizue gumzo mitaani lakini mwanzo sio lazima uwe mgumu kwa wenye upeo na mtazamo mpana. Tusifikirie kwamba umaarufu na ubabe ndio njia pekee ya hoja ya yeyote kusikilizwa na kufanyiwa kazi. Kama wino umeisha na imekubidi uandikie makohozi basi elewa kwamba kuwa na mitazamo ambayo haiegemei upande wowote na yenye kutatua changamoto yoyote kwenye jamii yetu ni chachu katika kuwezesha utekelezaji wa maoni.

Nawasihi watanzania wenzangu kuzingatia uelewa wa kina kuhusu suala lolote wanalo amua kutoa mchango. Sambamba na hilo, uelewa huu hautoshi kama jazba na upendeleo hutawala kwenye mdahalo yoyote. Siasa ni moyo kwenye kila nchi na kama wananchi, hatuna budi kutanguliza utanzania kwanza na sio uchama. Unapoona chama tawala hakija watendea wananchi haki, kuwa kipaumbele kutoa mchango bila upendeleo kwa manufaa ya watanzania wenzako. Upendeleo wa chama chochote katika mdahalo wowote, haswa baada ya maamuzi yanayo bomoa, huonyesha udhaifu kifikra na nia ambayo sio njema kwa watanzania. Kutetea mifumo batili ya uongozi na maamuzi sio picha ambayo chama chochote cha siasa kinatakiwa kuonyesha kwa wananchi. Ubabe na ugandamizi kwa wenye maoni mbadala sio afya katika suala zima la kuwa na demokrasia imara. Tupende uchambuzi huru, tusiegemee upande wowote bila kuwa na sababu za msingi, midahalo ifanywe kwa staha na kwa manufaa ya Tanzania kama nchi na sio kwa matakwa ya chama chochote cha siasa au mwanasiasa yeyote
 
Hakuna staha kwa watu wapumbavu na wenye akili zilizo oza. Mpumbavu mjibu kipumbavu
 
Issue muhimu ni kusikiliza kila kitu iwe ni kutoka kwa mwanasiasa au hata wewe mwisho mimi ndiye wa kuamua lipi pumba na lipi ni mchere.

Kwenye haya maisha kuna aina tofauti za waongeaji wabaya, wazuri nk, ila katika kuhagua ni suala la mtu mmoja mmoja.
 
Back
Top Bottom